Mafunzo ya imani kwa binadamu kwa kuubiri ukweli.
Mara nyingi napenda kusikiliza maubiri ya neno la Mungu toka kwa wachungaji tofauti hapa duniani.
Lakini napenda mchungaji anayetumia maandiko ya biblia kama nguzo yake ya kuubiri amani.
Mungu ambariki na kuwaonyesha njia watumishi wake walio wengi kulisambaza nene lake.
Ndio maana roho mtakatifu aligawa nguvu za lugha tofauti ili neno lisambae duniani kote.
Kazi ya kulisambaza neno la Mungu pande zote duniani ni kazi ya kila mmoja wetu.
Kuna kitu kimoja ambacho kinanionya kutojaji imani ya dini ya binadamu mwingine yeyote, kwa sababu yeye au mimi tuna utashi wa kuwa upande wa imani wowote bila kulazimishwa na mtu yeyote.
Imani ni njia ya binadamu kujenga mahusiano kati yake na Mungu.
Imani ndio njia yenye nafasi ya matumaini kwa kila mtu kufanya mahamuzi ya kujijenga katika mahusiano yenye ushawishi wa nafsi yake na Mungu.
Tulipewa nafsi yenye imani ili kulitangaza neno lake Mungu kutoka katika masoma au mafundisho yaliyopo katika vitabu vitakatifu katika biblia.
Vitabu vitakatifu vinavyotumika kufundisha yale yaliyo na hekima ili kutufungulia upendo wa kweli toka kwa Yesu kristo.
Upendo wa mafundisho ya Yesu kristo ni njia yenye mafunzo yake kwa upeo na busara na amani.
Yesu alikuja na kutufundisha yale yaliyo mema ili kutufungulia njia ya faraja katika safari ngumu hapa duniani.
Mafundisho yake yote yalikemea mabaya na kukataa kurudia maneno mabaya.
Mungu alikemea matendo mabaya kwa kutufundisha kutenda yaliyo mema.
Mfano kitabu cha waamuzi mlango wa 13 kinatufundisha hivi...
MLANGO 13
1 Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini.
2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake;
7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
8 Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.
9 Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye.
10 Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile.
11 Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi.
12 Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini?
13 Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari.
14 Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.
15 Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.
16 Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana.
17 Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza?
18 Huyo malaika wa Bwana akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu?
19 Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia.
20 Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi.
21 Lakini malaika wa Bwana hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa Bwana.
22 Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemwona Mungu.
23 Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
24 Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni