VIFO VILIVYOTOKEA KWA WANA HABARI WA AZAM MEDIA
Sipati picha kwa majonzi yaliyomo ndani ya moyo wangu kutokana na ajali, iliyosababisha vifo vya watu saba miongoni mwao wafanyakazi watano wa Azam Media.
Najaribu kuvuta picha kwa vijana mafundi wachapakazi hodari jinsi ndoto zao na mipango yao katika taasisi ya habari chini ya movuli Azam Media Group.
Maisha ni sawa na universe ilivyo na umbo kubwa na umbali husiogawanyika na namba yeyote.
Unaanza mipango yako vizuri bila woga lakini huwezi tazama mbele kuna nini.
Nikijaribu Najaribu kuinua macho yangu juu na kupeleka fikra zangu za ujana kwa vijana wenzangu Azam Media.
Basi nabaki katikati ya fikra na kunyamaza kimya huku simanzi za machozi zikinijia kwa mbali.
Maswali mengi yamejikita katika fikra za ubongo wangu kutokana na tukio hilo la ajali.
Mawazo mengi yanakuja mbele yangu, lakini sipati picha katika fikra zangu, nini kilichotokea na kupelekea kubaki kimya.
Sisi ni binadamu na yale yote yaliyotokea tunayaona sisi tuliobaki hapa duniani.
Lakini vijana hawa.
1. Salim J Mhando
2. Silvanus W Kassong
3. Charles Wandwi
4. Florence B Ndibalema
5. Said H Hassan
Tuwawashia mishumaa ya maombolezi kwa wote watano
Safari yao ya hapa duniani ndio imefika mwisho.
Majonzi na maumivu ya simanzi zinabaki kwetu tulio hapa duniani.
Nashindwa kuendelea kuandika chochote zaidi ya kuwaombea wale wote waliofariki.
Nanyamaza kimya na kuangalia dunia inavyo songa mbele kwa spidi.
Na
Kennedy Kimaro.