Saturday, August 4, 2007
HAWA NDIO ZE COMEDIAN TZ
HAWA JAMAA WANAPENDWA ZAIDI HAPA BONGO KWA VICHEKESHO VYAO LAKINI MMMMMM MIMI SIMO IPO SIKU
NITUKUBONYEZA NINI HIYO SIRI WEWE POZI KWENY BLOG HIII
Posted by Unknown at 8/04/2007 03:08:00 PM
Dumia Isiyo na Njaa
Maono yetu ni ulimwengu ambao hauna njaa na ukosefu wa lisha bora- ulimwengu ambamo kila mtu anaweza kuhakikishiwa kuwa atapata chakula anachohitaji ili awe na lishe bora na mwenye afya. Maono yetu ni ya ulimwengu ambao mbali na kumpa kila mtu maslahi na heshima yake kama mja, utavilinda vitu hivi. Huu ni ulimwengu ambapo watoto watakua, wajifunze na kunawiri, huku wakiishia kuwa watu katika jamii walio na afya nzuri, wenye kuitumikia na kuijali.
Ijapokuwa mafanikio katika kupunguza matatizo ya njaa ya lishe bora yameonekana ulimwenguni kote, bado tungali nyuma katika kufanikiwa kuwa na ulimwengu ambao watu wake hawana njaa. Tunaona elimu na taarifa za masuala yaliyofungamana na njaa ulimwenguni, usalama wa chakula na lishe bora kama masuala muhimu katika kufanya maono haya ya kilimwengu yafaulu. Kwa hali hii, tunazielekeza juhudi zetu kwa vijana na walimu wao. Je, endapo kila mwaka, kwenye siku kuu ya Chakula Ulimwengu (tarehe 16, Oktoba) watoto ulimwenguni kote watafahamishwa kwa pamoja vifaa vinavyofanana vya kufunzia kuhusu njaa na utapiamlo pamoja na yale yatakikanayo kufanywa, wataweza kukua wakitambua jinsi ulimwengu wetu unavyotegemea mambo mengine? Je, endapo watafundishwa masomo kutoka sehemu tofauti tofauti za ulimwengu,kutoka tamaduni na hali mbalimbali wakakuwa tayari kufanya kazi pamoja ili kutatua matatizo ya njaa na usalama wa chakula? Je, kunazo njia ambazo kwazo kizazi cha vijana chaweza kukuzwa ili wawe wananchi wanaotegemewa na walio wa kilimwengu?
Tunaamini kwamba majibu kwa maswali haya yote ni “NDIYO” kama walimu mpo katika hali nzuri ya kuweza kuwafanya vijana wawe ni watu wanaojali na wanaojitolea kijiunga katika vita dhidi ya njaa. Ubunifu, mawazo fikira, pamoja na maguvu ya vijana huwakilisha rasilmali muhimu ya kuendelea kukuza jumuiya na mataifa yao. Nyinyi, walimu wao, mwaweza kusaidia katika kuleta mageuzi kupitia kwa ujulishaji, kubadilishana maarifa, kuhimiza ushiriki, na kuwaonyesha vijana kuwa wanalo jukumu muhimu katika kufaulisha kuwepo kwa ulimwengu usio na njaa.
Tungependa kuwapa moyo kujiunga na walimu pamoja na wanafunzi ulimwenguni kote ili kujihusisha katika shughuli za Kulisha Akili, Kupambana na Njaa.
Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani
Journée mondiale de l'alimentation
Washiriki katika du Projet Kulisha Akili, Kupambana na Njaa
Shukrani
Kudhamini
Wasiliana nasi
Pata faili la mtindo wa PDF
Posted by Unknown at 8/04/2007 03:03:00 PM
Blogger Beta non-spam review and verification request: http://kennedytz.blogspot.com/
Blogger Help
to me
show details
Aug 3 (2 days ago)
Hello,Your blog has been reviewed, verified, and cleared for regular use so thatit will no longer appear as potential spam. If you sign out of Blogger andsign back in again, you should be able to post as normal. Thanks for yourpatience, and we apologize for any inconvenience this has caused.Sincerely,The Blogger Team
Posted by Unknown at 8/04/2007 03:03:00 PM
Thursday, August 2, 2007
Monday, July 30, 2007
Sunday, July 29, 2007
JENGO LITAKOLIPIKU KITEGA UCHUMI LIPO KARIBU NA POSTA MPYA
Posted by Unknown at 7/29/2007 10:17:00 PM
SALAMA AKIWA STUDIO ZA CHANNEL FIVE [5]
Mwanadada Salama akiwa kwenye Kipindi chake cha Planet Bongo Mwana dada huyu ni machaahari katika
kutoa kasoro nyimbo za kizazi kipya, hiyo stairi ya kuwapa changamoto wanamuziki katika kuwa makini
kwenye kurekodi. Wewe msomji unasemaje kuhusu Salama na Speed yake hiyooo.... mmmmm naishia hapo
Posted by Unknown at 7/29/2007 09:47:00 PM
Friday, July 27, 2007
HUYU NDIYE MBUNGE WA VIJANA ALIYEKUWA NA MIKAKATI MIKUBWA KWA VIJANA LAKINI AMETANGULIA MWENZETU AMINA
HEKIMA YA MWANA WA MUNGU NI AMANI YA UPOLE II TAYARI KUSIKILIZA MANENO YA WATUINA HURUMA WALA
HAINA HILA YOYOTE VITA MAPIGANO NA TAMAA ZISIZOFAA ZAONYESHA ZAONESHA HATUNA HEKIMA.
SOMA HILI SOMO LINA SEMAJE
Hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko na kila tendo baya. Lakini hekima itakayo juu, kwanza ni safi,
tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina,
haina unafiki, Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Vita vyatoka wapi,
na mapigano yaliyo kati yenu yatoka wapi? Si humu katika tamaa zenu zifanyavyo vita katka viungo vyenu?
Mwatamani wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. mwafanya vita na kupigana wala
hamna kitu kwa kua hamwombi! Hata mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya,ili mvitumie kwa tamaa zenu
NDUGU MPENDWA TAFAKARI NA UFIKIRIE VIZURI NINI KINCHOSEMWA HAPO
Posted by Unknown at 7/27/2007 10:24:00 PM
Wednesday, July 25, 2007
UNAPOTAKA KUSHINDANA NA MASHINE BAADA YA KUNYWA POMBE JE ITAKUWAJE ??
Ebwana weweee kwenye Hiyo motokaa kulikutwa mizinga ya yule jamaa aliyenyanyua mikono juu[konyagi]
Inasemekana dreva na abiria wake walitaka kumshusha mikoni chini, katika kushindana ndiyo yakotokea Hayo
Jamani Magari yananunuliwa kwa bei mbaya lakini kuyaaribu ni dakika chache tuuu
Madereva Hacheni kulewa huku mnadrive ni Hatari ya Danger mmmmmm mimi simo
Lakini wote walitoka salama hila majeraa modogo tu ya kukumbukia walichofanya Tena hospital haikuwa
mbali sana na palipotokea ajari. Yote hayo yalitokea usiku wa manane
Posted by Unknown at 7/25/2007 09:01:00 PM
TEMBA AKIWA KAZINI KAMA WENGINE HAPA DUNIANI
Ebwana maisha ni Kutafuta shilingi Huyo ndugu yangu ni Mjalisimali kweli. Kila siku inapoanza yeye na kiti chake Kuanzia saa kumi
na mbili ya alfajiri lazima afungue hiyo biashara ya kuuza vocha za simu Kwa wapita njia wa mtaa wa Jogoo kalibu na LONG SHOOT
Na anapatikana kwenye eneo hilo mchana wote, mpaka wakati wa Dunia inapoliacha jua kunzunguka upande mwingine
Huyo jama jina la tatu ni TEMBA Yupo hapa Bongo kutafuta hili hawe Tajiri wa kesho na si leo
Wapo wengi tu wenye mawazo kama yake hapa Dar Mungu yupo nao wale wote wenye kutafuta kama TEMBA
YEYE ANASEMA WAMSAIDIE ILI APATE KIBANDA CHA KUFANYIA BIASHARA YAKE ILI YULE MKUU WA MKOA ........
Mimi naishia hapo wewe teta ktk Maoni
Posted by Unknown at 7/25/2007 07:28:00 PM
Sunday, July 22, 2007
WAKAGUZI WA MAGARI WAKIWA KAZINI
HUWA INASAIDIA HAWA JAMAA WAKIWA PEMBENI YA BARABARA INABIDI WAKAE KILA BAADA YA HUREFU FURANI HIVI
AFANDE AKIWA KAZINI

KUPAKI KAMA HIVI NI HATARI PIA LAKINI MMMM NDIO DAR HIYO
Posted by Unknown at 7/22/2007 11:01:00 PM
USALAMA KAZINI HAKUNA KATIKA KAZI KAMA HII
Huyu jamaa anafanya kazi katika mazingira ya hatari Lakini afanye nini kama akikataa Mwingine atafanya kama yeye
Kama kijikampuni kingekuwa kinajari hayo
Wangenunua Gari ya Lifti Ebwana ndio Tanzania hiyo Wewe unasemaje ???? Tuma comment
Posted by Unknown at 7/22/2007 11:01:00 PM
Labels: Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved, Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved.
Friday, July 20, 2007
NI MABADILIKO MAKUBWA PIA KATIKA SERIKARI
Hakina Michuzi na wamo Picha za kwanza wakiwa na Jaji Mkuu Mpya

Hebu Tupia mawazo Majina ya Jaji Mkuu wetu.
Augustino Ramadhani Wewe kama wewe unasemaje? Tuma maoni yako tutatete....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Jakaya Kikwete amemteua jaji Augustino Ramadhani kuwa jaji mkuu wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu kiongozi, jaji augustino ramadhani anachukua nafasi ya jaji barnabas samatta ambaye mkataba wake umemalizika. Kabla ya uteuzi huo jaji Augustino Ramadhani alikuwa jaji wa mahakama ya rufani ya Tanzania.
Thursday, July 19, 2007
UKUTA MREFU ZAIDI DUNIANI
Posted by Unknown at 7/19/2007 10:26:00 PM
Tuesday, July 17, 2007
HUYU NDIYE ALIYETANGULIA AMINA NAKUMBUKA BAMBATAA YA MAMA NONINO

Namfahamu Mh. Amina Chifupa tangu akiwa mwanafunzi wa Makongo Sekondari na hasa alipoanza kutangaza na kituo maarufu cha redio cha Clouds. Lakini hasa nilimfahamu sana Mh. Amina Chifupa wakati nikisoma naye chuo cha uandishi wa Habari cha ROYAL ambacho sasa kinajulikana kama ROYAL COLLEGE OF TANZANIA ambapo tulikuwa darasa moja na mimi kuwa kiongozi wake.Kwa kifupi kabisa naweza kusema kwamba, kuingia bungeni kwa Mh.Amina Chifupa kuliendelea kunipa mwanga wa ni aina gani ya mtu Amina ameamua kuwa. Alionyesha ujasiri mkubwa katika umri mdogo na hasa alipolivalia njuga suala la Madawa ya kulevya.Hamasa kubwa alioionyesha kwa vijana sina shaka kwamba ametuachia mtihani mkubwa wa kumuenzi hasa katika mtiririko wa shughuli ambazo alikuwa amejipangia kuzitekeleza kwa niaba ya vijana kama muwakilishi jasiri, aliyedhamiria, mwenye moyo wa machungu ya dhati na asiye woga kujua hatima ya kinachomkera.Taifa la Tanzania limepoteza mrithi wa jamii, Vijana wamepoteza nguzo na chachu ya hamasa, Wazazi wamepoteza mlezi na mrithi lakini kubwa zaidi umma umepoteza mwelekeo na mtazamo sawia.Serikali yetu inayo kazi kubwa ya kumuenzi Mh. Amina Chifupa na pengine haitasaidia kumuenzi kwa kumuandika kwenye vitabu, kumjengea mnara na mambo kama hayo.......Serikali imuenzi amina katika vita aliyoianzisha dhidi ya udhalimu wa madawa ya kulevya ambacho ndicho chanzo cha kuwa na vijana mazezeta.....Mh. Amina alikereka sana na uharibifu usio huruma dhidi ya vijana. Nawapongeza radio Clouds ambayo Mh. Amina aliitumikia kabla ya majukumu ya kitaifa kwa kumuenzi kwa maombolezo kiofisi lakini huu uwe mwanzo tu, hakika akina Masoud Kipanya, Gadner Habash, Joseph Kusaga, Luge Mutahaba na timu nzima ya redio hiyo itafanya kitu kikubwa sana ambacho kitabakia kumbukumbu ya kudumu juu ya Amina Chifupa."Hakika Mwanadamu atakufa na hakika ikifika haipingiki" Hukumu ya kiini hasa cha kifo cha Mh. Amina tumuachie Mweny-enzi Mungu mwenye haki juu ya vyote vilivyomo.MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA AMINA CHIFUPA.

Posted by Unknown at 7/17/2007 10:05:00 PM
Labels: Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved, Ipyana Mwakamela said... posted by Chemi Che-Mponda
Sunday, July 15, 2007
MAISHA POPOTE PALE YANAENDELEA
Posted by Unknown at 7/15/2007 09:21:00 PM
Labels: Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved, Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved.
Saturday, July 14, 2007
MAISHA NI KUANGAIKA LEO WEWE KESHO NANI?
Posted by Unknown at 7/14/2007 02:13:00 AM
Labels: Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved, Copyright 2007 kennedy blog. All rights reserved.


































