| WATU wanane, akiwamo bi harusi mtarajiwa aliyekuwa akisafiri kuhudhuria Kitchen party, wamekufa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu, likiwamo basi lililokuwa limebeba maiti.
Watu saba kati ya hao walikufa papo hapo baada ya basi la Meridian kuligonga kwa nyuma basi dogo la Toyota Hiace lililokuwa limembeba bibi harusi mtarajiwa, mama yake mzazi, nduguze, mpambe wake na jamaa waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga, juzi jioni.
Polisi wamemtaja msichana huyo kuwa ni Irene Stephen Hizza (22) aliyekuwa mkazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam aliyekuwa akisoma katika Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini. Mpambe wake pia alikufa katika ajali hiyo.
Jana alasiri bwana harusi mtarajiwa, Ramadhani Lukuta alilieleza HabariLeo Jumapili kuwa Irene na wenzake walikuwa wakienda Tanga kwa ajili ya sherehe za kumuandaa bibi harusi, maarufu kama Kitchen party.
Kwa mujibu wa mkazi huyo wa Dar es Salaam, aliyekuwa mkewe mtarajiwa anatarajiwa kuzikwa leo katika Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza mkoani Tanga na kwamba miili mingine mitatu ingesafirishwa jana jioni kuletwa Dar es Salaam.
Ilikuwa imepangwa kwamba harusi baina ya Irene na Lukuta ingefanyika Aprili 26. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Simoni Sirro alisema jana kuwa basi la Meridian liliigonga Hiace hiyo juzi saa moja usiku katika Kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni.
Aliwataja marehemu wengine kuwa ni mpambe wa bibi harusi, Latifa Undole (23) aliyekuwa akisoma CBE Dar es Salaam, Dafroza Mapunda (23) aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam, na George Hizza (11) aliyekuwa akisoma darasa la sita katika Shule ya Mtakatifu Maria, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Polisi, marehemu wengine ni Neema Chedi (26) mkazi wa Dar es Salaam aliyekuwa akifanya kazi Mamlaka ya Bandari, dereva wa Hiace, Zuberi Mohammed (35), mama Masatu (45) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Mariam aliyekuwa akiishi Dar es Salaam.
Kamanda Sirro alisema watu 12 walijeruhiwa katika ajali hiyo, watatu wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tisa wamelazwa katika Hospitali ya Korogwe. Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, basi la Meridian lililokuwa likiendeshwa na Edward Temu (35) lilikuwa limebeba maiti aliyekuwa akisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kamanda Sirro alisema, kabla ya ajali hiyo, Hiace hiyo ilikuwa mbele ya basi la Meridian yote yakiwa katika mwelekeo mmoja na kulikuwa na lori mbele yao. Alisema, wakati yakiendelea na safari, dereva wa Hiace alipunguza mwendo kuepuka kugongana uso kwa uso na basi la Scandnavia aina ya Isuzu Nissan lililokuwa kwenye mwendo mkali.
Sirro alisema baada ya basi hilo dogo kupunguza mwendo, basi la Meridian lililokuwa kwenye mwendo mkali liligonga kwa nyuma na kusababisha Hiace hiyo iligonge lori aina ya Fuso na gari hilo dogo likapinduka.
Kwa mujibu wa Mwandishi Wetu wa Tanga, waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Anna Alli (48), Anase Meridiani (30), Sophia Vicent (22), Aisha Rashid (29), Barnabas Vallerian (44), Anna Mhina (48), Nora Msindai (22), Sekuza Nyamwanga (30) na Laurance Ndiu (30), wote wakazi wa Dar es Salaam. Wengine ni Doris Mhina mkazi wa Tanga na Samweli Shirima (22) mkazi wa Rombo mkoani Kilimanjaro.
WATU wanane, akiwamo bi harusi mtarajiwa aliyekuwa akisafiri kuhudhuria Kitchen party, wamekufa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu, likiwamo basi lililokuwa limebeba maiti.

|