Matumbo ya Watanzania yapasuka wakiwa ndani ya ndege
Post toka nukta77 Tuesday, February 10, 2009
Madawa ya kulevya : WaTanzania wawili wafariki nchini Ethiopia
Tarehe 24 ya mwezi Januari niliandika kuhusu habari ya MTanzania aliyekuwa amelazwa akiwa mahututi katika hospitali ya Polisi ya Hayat iliyopo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kutokana na kupasukiwa tembe kadhaa za dawa za kulevya.
Habari zilizoandikwa katika shirika moja la habari nchini Ethiopia zinathibitisha kuwa kitengo cha Polisi cha nchini humo kimeripoti kuwa WaTanzania wawili wamefariki katika kisa hicho cha kupasukiwa na tembe za dawa za kulevya. Polisi walitaja umri wa vijana hao kuwa ni miaka 27 na 32 na mmoja alikuwa akisafiri kuelekea China wakati mwingine alikuwa akirudi toka huko kuelekea Tanzania. Mmoja wa marehemu hao alizidiwa na tembe kupasukia tumboni, jambo lililowasababisha askari kufanya uamuzi wa kuwachunguza abira wengine na ndipo walipomgundua MTanzania wa pili akiwa na madawa tumboni.
Miili ya marehemu hao ilisafirishwa siku ya Jumapili hadi Tanzania kwa ushirikiano wa kitengo cha Polisi cha Ethiopia na ubalozi wa Tanzania uliopo nchini humo.

The two died as some of the capsules burst into their stomachs. More than 42 drug capsules were found in the stomach of one of them who was traveling from China to Tanzania on Ethiopian Airlines - alisema askari aliyekuwa akitoa taarifa za vifo hivyo.Aina ya dawa zilizokutwa tumboni mwa vijana hao ni Heroin katika mfumo wa tembe ambapo mmoja alikuwa na tembe 17.