Friday, March 27, 2009

Buriani Prof.Ken Edwards (Brother Joshua Mkhululi

Buriani. Prof.Ken Edwards (Joshua Mkhululi) Mungu akulaze pema peponi.
22 January 1945 - 18-March-2009
Wengi wameguswa na msiba huu wa marehemu Prof.Ken Edwards maarufu pia kwa jina
la Kaka Joshua Mkhululi,Mwana wa Afrika halisi aliyezaliwa jamaika 22-January 1945 na kufariki Arusha,Tanzania 18-March 2009.
Marehemu Prof Ken Edwards atakumbukwa daima milele kwa mchango wake mkubwa
katika jamii ya watanzania na wafrika wenziwe kwa ujumla,kuanzia elimu ya juu mpaka katika maisha ya kawaida ya jamii ya watanzania,ambayo Prof.Ken alijichanganya na kujumuhika.
Prof.Ken Edwards alikuja Tanazania 1976 na kujiunga katika tahasisi ya elimu ya juu kabisa
CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM,ikimbukwe katika miaka hiyo ya 1976 nchi hilikuwa
katika uhaba mkubwa wa mahitaji ya mwanadamu kama vile vyakula mchele,unga na sukaari ulipatikana madukani kwa foleni! Prof.Ken alikubali kuwa pamoja na watanzania
akiamini kabisa kuwa Tanzania na Afrika ni kwao katika ardhi walikotoka mababu zake
miaka 500 hiliyopita,ambao walichukuliwa katika bishara ya utumwa.
Kipindi hicho chote kugumu kwa watanzania prof.ken alishea mda wake kwa kuwa pamoja
na watanzania na juhudi zake ziliweza kuanzishwa duka la ushirika la wafanyakazi wa chuo kikuu cha UDSM ambako yeye mwenyewe alikubali kuacha usomi wake! na kusimama dukani pale UDSM na kuhakikisha kuwa kila moja anapata jaapo kilo ya sukari na unga!
hili liliwashangaza wengi! Proffessor kushea maisha ya kawaidana watu wa maisha ya chini!
Prof.Ken Edwards !Mwanamichezo
Prof.Ken akuishia hapo bali alikuwa na moyo wa upendo kwa watanzania na wafrika kwa ujumla ! alitumia mda wake mwingi wa ziada kwa kushiriki kaatika maendeleo ya jamii
na alijua wazi KANDANDA ni mchezo unawaunanisha wanadamu wengi bila kujua tofouti zao ziwe za kikabila,dini,koo n.k,linapofikia swala la jamii na michezo Prof:Ken anauweka pembeni usomi na uprofesa wake na anarudi chini kushea na wafrika wenziwe na matunda
yake !alianzisha timu ya mpira (Kandanda) ya Vijana wa KUNDUCHI MTONGANI wakati huo Kunduchi hakukuwa na majengo yaliyo sasa bali kulikuwa USWAHILINI,Prof.Ken alikubalika na Vijana na wazee wote wa Kunduchi na kule ni Maarufu kwa jina la Kaka Ken(brother Ken)
au Kaka Mkhululi.
Prof.Ken na UAFRIKA
unapokuja katika swala la uafrika hapa ndipo utagundua kuwa Kaka Ken au Brother Mkhululi
Alikuwa ana upendo wa Afrika na kuwapenda wa afrika wenzie zaidi ya wafrika,hapa ndipo palipo mfanya Prof.Ken Edwards kufikia jina la Kaka Joshua Mkhululi,kwani alikuwa anaamini kabisa katika moyo wake wote kuwa kama si biashara haramu ya utumwa iliwafanya babu zake kupelekwa utumwani visiwani Karibeani,yeye angezaliwa Dar,au Arusha,Kama si Kigoma na Dodoma,labda Kilwa,Lindi au Mtwara na Penginepo Mwanza!
Swala hili la UAFRIKA ndilo liliomfanya Kaka Ken au Joshua Mkhululi kuja Tanzania kutumia elimu yake! kuchangia maendeleo katika ARDHI ambayo ni asili yake na aliamini kuwa AFRIKA NI KWAO,kwani ELIMU YAKE ingemweza kufanya kazi na kuishi mahala popote duniani,lakini alikubali KURUDI NYUMBANI,TANZANIA,na Afrika kwa Ujumla.
Mchango wa Prof.Ken kuanzia UDSM kama Proffessor! Kunduchi kama mwanakijiji na Baba
Mwanzilishi wa timu ya kandanda ya vijana,Kariakoo kama rafiki na mbwiga wa Ras,
ARUSHA kama Mzazi Mwanzilishi wa ESAMI! ambako aliishi na Familia yake Mke na watoto!
Prof.Ken alikuwa mstari wa mbele kwa kuwapa changa moto WASOMI NA WATAALAMU
wenye hasili ya Kiafrika ambao wamezaliwa nje ya bara la afrika kurudi nyumbani kuja
kuchangia maendeleo ya ardhi waliotoka mababu zao AFRIKA.
Mwisho Kabisa tunatoa pole kwa familia ya marehemu Prof.Ken Edwards pamoja na wote walioguswa na msiba huu.
Maelezo ya hapo juu yanatambulisha mchache aliyochangia Prof.Ken Edwards katika maisha ya kawaida lakini yapo mengi.Kuanzia Arusha,Dar-Es-Salaam,Tanzania.
Accra,Ghana,Mbabane,Swaziland na kungineko.
Ukalale Pema Peponi Prof.Keneth Edwards aka Joshua Mkhululi,Ulizaliwa Ugenini Jamaika
umefia Nyumbani ,Arusha ,Tanzania,Afrika.Wewe ni shujaa na Mwafrika wa kweli uliyejitoa muhanga kwa kuchangia elimu yako na usomi na utalaamu wako wa Afrika
Upendo wako kwa bara hili la Afrika! utakuwepo Daima Milele na Milele
Jah Rastafari:
NB:
Shukurani Kaka Makunja kwa picha na machache

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu