AJALI ZAIDI YA WATU 10 WATEKETEA MOTO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Oct-
Watu zaidi ya 10 wameteketea kwa moto katika ajali ya basi la abiria
la DELUXE EXPRESS linalofanya safari zake kati ya ya Dar es Saalam na
Dodoma, baada ya basi hilo kupasuka tairi la mbele na kupinduka katika
Bonde la Bamba katika halmashauri ya mji Kibaha.
Kwa mujibu wa taarifaya Mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi,BW. ANDREW
ISAACK LWALI amesema majeruhi ambao wamepokelewa ni 34 ambapo wanaume
26 na wanawake 8 na kati yao kuna watoto wanne ambao ni wawili wenye
jinsia ya kike na wawili wa kiume ambao walikuwa na miaka kati ya
miezi sita na miaka 12.
DOKTA LWALI ameongeza majeruhi 32 walipatiwa huduma ya kwanza kwa
baadhi yao kushonwa na baadhi yao kufungwa POP na matibabu mengine
madogo ya kawaida ambapo wengi wa majeruhi waliondoka mara baada ya
matibabu, wakati wengine wawili ambao ni wanawake wamelazwa mmoja
akiwa ni Mama mjamzito BI. SIKUZANI HAMIS ambaye ni muuguzi katika
hospitali ya Makole mkoani Dodoma ambaye amevunjika mbavu.
Wakati majeruhi mwingine BI. CECILIA NGIRAO ambaye anasumbuliwa na
maumivu ya kiuno ambayo yamesababishwa na ajlai hiyo, na wanaendelea
kupatiwa matibabu baada ya kufanyiwa uchunguzi, aidha amesema mpaka
sasa hakuna maiti yoytote ambayo imefika hospitalini hapo kutokana na
wengi wao kubakia majivu na mifupa na inasadikika watu zaidi ya kumi
wameuwawa na moto huo.
Akizungumzia uwezo wa hospitali kupokea wagonjwa wengi kwa mara moja,
amesema wamekuwa wakati mwingine wakipata wakati mgumu kutokana na
kutokuwepo na madawa ya dharura ya kukabiliana na majanga kama hayo,
na hivyo kuwalazimu kutumia dawa ambazo zilikuwa kwa ajili ya wagonjwa
wa kawaida kwa kutribia majeruhi, lakini kwa ujumla wamefankiwa
kukabiliana na wimbi hilo la wagonjwa wa mara moja kutokqana na uzoefu
mkubwa waliuonao kutokana na ajalai kutokea mara kwa mara katika
barabra kuu ya Morogoro.
Naye abiria BW. MASHAKA MNYANYINDI amesema chanzo cha ajali hiyo ni
kupasuka kwa tairi ya mbele ya basi walilokuwa wamepanda, wakati huo
dereva wao alikuwa ana jaribu kulipita gari, na ndipo waliposikia
tairi yao ikipasuka na basi lao kuanza kuyumba hali ambayo ilimfanya
dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kutumbukia bondeni ambapo
lilibiringika mara mbili na kuanza kuwaka moto.
BW. MNYANDINDI amesema kilichomuokoa yeye ni kukaa katika viti vya
nyuma ya basi hilo, ambapo yeye na baadhi ya waliosalimika walitoka
katika sehemu fulani ya basi hilo ambayo ilikuwa wazi.
Mpaka naondoka katika hospitali ya Tumbi jioni hii, hakuna hata maiti
moja ambayo ilikuwa imewasili hospitalini hapo na niliweza kushuhudia
wafanyakazi wa chumba cha maiti wa hospitali ya Tumbi wakichukua
mabeseni na machela na kulega wakielekea eneo la tukio ambapo
inasemekana baadhi ya marehemu wanweza kuzikwa katika eneo la tukio.
Mwisho.