Thursday, February 23, 2012

WATU wawili wafariki mkoani Pwani


Na John Gagarini, Kibaha

WATU wawili wamekufa mkoani Pwani kwenye matukio mawili tofauti
likiwemo la wananchi wenye hasira kali kumwua kwa kumpiga Bw Idrisa
Ugandi (26) mkulima na mkazi wa Kiomboni Visiwani Wilayani Rufiji
baada ya kumtuhumu kuvunja na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya
shilingi 935,000.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana mjini
Kibaha na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Bw Ernest Mangu alisema kuwa
marehemu alikuwa na wenzake wanne ambao walikimbia kusikojulikana.


Kamanda Mangu alisema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 21 mwaka huu
majira ya saa 5:00 asubuhi huko Kijiji cha Mlanzi wilayani Rufiji.


Akielezea juu ya tukio hilo alisema kuwa marehemu na wenzake walivunja
nyumba ya Bw Salum Hija akiwa na wenzake na kufanikiwa kuiba vitu
mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu sh 800,00, simu mbili za
mkononi zenye thamani ya sh 80,000, redio ndogo yenye thamani ya sh
25,000, suruali moja aina ya Jeans sh 15,000, kanga doti moja sh 8,000
na kitenge doti moja 7,000.


Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye kituo cha afya
Mlanzi kusubiri uchunguzi wa daktari na ndugu wa marehemu kwa mazishi
pia hakuna mtu aliyekamatwa kuhusinana na tukio hilo na polisi
wanaendelea na uchunguzi.


Wakati huo huo mtoto Makia Karimu mwenye umri wa miaka (6) Mkazi wa
Bungu wilayani Rufiji amekufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati
akitembea kwa miguu.


Kamanda Mangu alisema kuwa tukio hilo lilitokea Kiiji cha Bungu majira
ya saa 1:30 usiku barabara kuu ya Dar es Salaam Kilwa ambapo aligongwa
na mwendesha pikipiki aliyetambuliwa kwa jina la Raphael aliyekimbia
akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T 419 aina ya Sanlg, chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi.


mwisho.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu