Maisha ya vijana wa sasa.
Ebu tubige stori fupi kidogo ya maisha ya vijana wa sasa.
Kila asubuhi baada ya kujiweka sawa kwa safari ya kibaruani.
Nilipata chai ya asubuhi kama kawaida. Nikabeba simu zangu mbili na funguo za gari yangu.
Nilitoka nje ya nyumba yangu kuelekea kwenye gari yangu.
Mama watoto na watoto wakaja kunifungulia Gqeti kama kawaida yao.
Wakati ninarudi nyuma na gari, uku niki seti redio station moja ili kupata taarifa za kila siku.
Kukawa na watangazaji katika kipindi kimoja cha asubuhi wakitafakari yaliyondikwa kwenye magazeti ya siku hiyo.
Kikubwa kilikuwa ni mwanasheria ambaye ni mwana siasa wakati alipogoma kutoka ndani ya mahakama kuepushwa kukamatwa na polisi.
Wakati huo mtangazaji mmoja a akitoa stori ya kibaka au mwizi sugu aliyekimbizwa mitaa ya kawe na kufananisha suala la yule mwanasiasa
Stori ilianza hivi, yule mwizi alipokuwa akakimbizwa na raia wenye uchungu wa kuibiwa kila mara nyakati za usiku wa manane.
Wakawa wanamkimbiza yule mwizi kimya kimya ili wamshikishe nidhamu ya kutorudia tabia ya wizi.
Yule mwizi kwa mwendo kasi akakatiza karibu na kituo cha polisi cha kawe.
Alipoangalia kwa mbele akawaona askari wamesimama eneo la mapokezi.
Moyoni akasema liwalo na liwe maisha ni matamu, nikipoteza muda nitapata kichapo cha nguvu na kupoteza maisha hapa.
Basi yule mwizi akaongeza mwendo kuelekea upande walipo askari polisi kituo cha kawe eneo la mapokezi na kusima nyuma yao.
Mtangazaji akaendelea kusimulia stori ya kibaka mwizi sugu.
Ndipo wale raia wema ilibidi wasimame gafla kwa kutoamini nini kilichotokea hadi mwizi kukimbilia upande wa kituo cha polisi.
Wale raia wema wakashauliana mmojawapo aende kuchukua yule mwizi sugu toka mikononi mwa polisi.
Ndipo njemba mmoja alichomoka na kuelekea alipo mwizi sugu katika kituo cha polisi.
Alipofika katika eneo ambapo yule mwizi mwizi chini ya ulinzi wa askari polisi
Askari polisi wakamuliza yule raia mwema? Una shida gani kijana!
Naye akamjibu, nimekuja kuchukua ndugu yangu huyo hapo
Huyu ndugu yetu ana matatizo ya akili siku nyingi.
Kwa sauti kubwa yule mwizi akajibu, Muongo Muongo mimi ni mwizi na wanataka kuniua.
Wakati polisi wakiwa katika mshangao kwa yote yanayotokea
Mara yule raia mwema akawa anajeuka upande mwingine ili kurudi nyuma gafla chuma kizito kikaanguka kutoka mfukoni mwake.
Basi yule mwizi akasema unaona askari chuma alichobeba anataka kuniua huyu.
Kumbe yule mwizi naye anajua kazi ya askari ni kuleta amani pale palipo na machafuko.
Kazi ya askari kusikiliza pande zote mbili zenye malalamiko ili kufanya uchunguzi na kujua nani ni mkosaji.
Askari alichofanya ni kuwakamata wote wawili na kuwakilisha chini mapokezi kwa muda.
Najua unanishanga Kwanini wote wawili na si akamatwe yule mwizi sugu.
Wakati huyu ni mwizi na amekuwa akifanya wizi leo na siku zote za ujana wake.
Yule askari akaja na karatasi za kuandika ripoti ya kesi iliyopo mbele yake.
Wa kwanza kuitwa kutoa maelezo yake ni yule mwizi sugu kwa yeye ndiye wa kwanza kufika kituo cha polisi.
Askari akaanza.. Unaitwa nani ndugu yangu.
Mwizi akajibu.. Naitwa... .
Una miaka mingapi!
Mwizi akajibu kumi na saba!√
Unaishi wapi
Mwizi akajibu kivukoni!
Kwanini umekuja hapa katika kituo cha polisi!
Mwizi.. Kimya
Askari akamgeukia tena yule mwizi sugu na swali lile lile.
Mwizi Sugu Kimya tena..
Basi askari polisi akumweleza kama huna jibu basi nitakukabizi kwa ndugu yako.
Yule mwizi sugu akajibu
Wataniua Watamuua.. Huyu siyo ndugu yangu kwanza simjui huyu huku akilia
Ndipo yule askari polisi akamuuliza swali lile mara ya tatu
Mwizi akajibu
Yeye ni mwizi na kazi zake mchana ni
mpiga debe wa daladala na usiku wanajikusanya na kuiba katika nyumba za watu au vifaa katika magari.
Askari akamwambia weka sahihi yako katika maelezo haya.
Mwizi sugu akachukua peni na kumwaga wino au sahihi katika maelezo yake.
Askari akamchukua na kumweka ndani mpaka siku inayofuata.
Jaribu kuwaza askari polisi alifanya maamuzi gani kwa yule raia mwema.
Mwisho
Kennedy Kimaro
@kennedytz2