Saturday, September 1, 2007

MREMBO ATAKAYEIPELEKA TZ KATIKA MISS WORLD TUTAMPATA LEO USIKU









Harakati za kutafuta mrithi wa taji la urembo la Taifa ` Vodacom Miss Tanzania 2007` linaloshikiliwa na mrembo Wema Sepetu aliyetokea katika Kanda ya Kinondoni linaanza leo katika shindano la kumtafuta malkia wa kitongoji cha Dar City Centre linalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza. Kufanyika kwa shindano hilo ndio ishara kamili ya uzinduzi wa mashindano ya urembo ya mwaka huu ambayo yanafanyika chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom. Mratibu wa shindano la Miss Dar City Centre, mkurugenzi wa kampuni ya Ellies Production, Eliude Pemba alisema jana kuwa maandalizi kwa ajili ya kinyang`anyiro hicho yamekamilika jumla ya warembo 17 wanatarajiwa kuchuana kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Rehema Mhinzi. Alisema kuwa kampuni yake imepanga kutoa zawadi ya gari aina ya Starlet yenye thamani ya sh. milioni sita kwa mrembo atakayefanikiwa kuibuka mshindi kwenye shindano hilo. Eliude aliitaja zawadi ya mshindi wa pili kuwa ni fedha taslimu sh. 300,000, mshindi watatu sh. 200,000, mshindi wanne sh. 150,000, watano akiondoka na sh. 100,000 huku kifuta jasho ikiwa ni sh. 20,000 kwa washiriki wengine waliobakia. Alisema kuwa pia kutakuwa na shindano dogo la kuwania taji la balozi wa hoteli ya Ubungo Plaza, ambapo mshindi atazawadiwa fedha taslimu sh. 300,000 na kupata ajira ya miezi sita yenye thamani ya sh. milioni 1.5. Aliongeza kuwa wamiliki wa hoteli hiyo wamesema kuwa balozi huyo akiweza kuimudu vyema kazi atakayopatiwa katika kipindi cha miezi sita, atapatiwa ajira ya kudumu pamoja na kuongezewa mshahara na kuwa sh. 300,000 kwa kila mwezi. Alisema kuwa shindano hilo linatarajiwa kupambwa na burudani kutoka kwa bendi mahiri ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia maarufu kama `Wazee wa Ngwasuma`, Hafsa Kazinje anayetamba na kibao chake cha Presha alishorikiana na Banana Zoro pamoja na kikundi mahiri cha wasanii wenye vipaji cha Tanzania House of Talent (THT). Aliwataja warembo wanaotarajiwa kuwania taji hilo kuwa ni Janeth Projest, Amata Chishato, Latifa Warioba, Sylvia Benedict, Witness Tresphory, Catherine John, Mariam Jerry na Doris Likwelile. Wengine ni Asha Hassan, Rihama Hussein, Immaculatie Ngerezah, Flora Mvungi, Leylat Jeruisy, Neema Mathias, Seprise Joseph na Martha Malissah. Warembo watatu watakaoshika nafasi za juu kwenye shindano hilo watakiwakilisha kitongoji hicho kwenye mashindano ya Kanda ya Ilala yatakayofanyika baadaye mwezi Juni.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu