Daniel Arap Moi aunga mkono Mwai Kibaki
Rais wa zamani Daniel arap Moi ametangaza msimamo wake kuhusu nani atakayemuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao na chaguo lake ni aliyekuwa mpinzani wake na sasa Rais Mwai Kibaki.
Akihutubia waandishi wa habari mjini Nairobi, Bwana Moi alisema kuwa Rais Kibaki anastahili kuungwa mkono kutetea kiti chake na kutawala kwa zamu ya pili.
Bwana Kibaki alikuwa mpinzani mkubwa wa Rais Moi ambapo waligombea urais mwaka wa 1992 na 1997.
Bwana Moi alitawala Kenya hadi mwaka wa 2002 ambapo, kisheria, hangeweza kugombea tena kiti hicho.
Alimuunga mkono mwanasiasa chipukizi, Uhuru Kenyatta wa chama cha KANU ambacho kilikuwa kimetawala Kenya kwa karibu miaka 40.
KANU kiling'olewa madarakani kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1963.
Bwana Moi aliwaambia wandishi wa habari kuwa Rais Kibaki hakuwa na ukabila na kwamba alikuwa anakuza umoja wa taifa na kuzingatia ajenda ya maendeleo.
Aliukosoa muungano wa ODM kwa kukosa utengamano. Chama cha KANU ni moja wapo wa vyama washirika wa muungano huo wa ODM.