Showing posts with label Imeandikwa na BBC Swahili. Show all posts
Showing posts with label Imeandikwa na BBC Swahili. Show all posts

Sunday, October 21, 2007

Simu kutoka angani

Hivi karibuni abiria wanaweza kuanza kutumia simu zao za mikononi wakiwa katika safari za ndege wanaposafiri katika anga ya nchi za Ulaya.





Mipango imeandaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kutumia teknolojia inayowezesha simu za mkononi kupigwa bila kusababisha athari zozote za mawasiliano ya ndege.
Wasimamizi kote barani Ulaya wameitisha mashauriano kuhusu uwezekano wa kutumika kwa teknolojia hiyo.
Endapo itaidhinishwa, huduma hiyo itawezesha simu kupigwa tokea angani wakati ndege ikiwa umbali wa mita 3000 juu.
Mashirika ya ndege yatahitaji kuamua endapo yanataka kutumia teknolojia, endapo ruksa itatolewa na idara za usimamizi za nchi husika.
Je mfumo huu unafanyeje kazi?
Kiwango cha ushirikiano kati ya nchi za Ulaya itakuwa na maana kwamba simu za mkononi zinaweza kupigwa wakati ndege zikiruka katika anga za mataifa ambayo bado hayajaidhinisha utekelezaji wa teknolojia hiyo.
Kwa wakati huu matumizi ya simu za mkononi yamepigwa marufuku kwenye ndege kwasababu ya kuwepo kwa ushahidi kwamba zinaweza kuingilia na kuvuruga mawasiliano na mifumo ya kuongozea ndege.
Utafiti uliochatangazwa mwaka 2003 na CAA ulipata matokeo kwamba mawimbi ya simu za mkononi yanavuruga uongozaji wa ndege kwa takriban nyuzi tano.
Hatua tofauti
Msemaji wa taasisi ya usimamizi wa mawasiliano nchini Uingereza ya Ofcom, ameeleza kwamba bado kuna hatua kadhaa kabla ya idhini ya mwisho haijatolewa kuwezesha mpango huo kusambazwa kikamilifu.
Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa anga ya Uingereza (CAA), na ile ya Ulaya, European Aviation Safety Agency, yanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba usalama wa ndege na abiria unazingatiwa kabla ya mifumo hiyo kuanza kutumika.
Mawasiliano ya simu za mkononi katika ndege imekuwa kikwazo kwa abiria wengi.
Taasisi ya usimamizi wa ndege imesema kwamba teknolojia hiyo inaweza kuanza kutumika mwaka ujao wa 2008.
Mfumo unaopendekezwa unatumia kituo cha ndani ya ndege ambacho kinarusha mawimbi kwenda simu za mkononi za abiria.
Vituo vya kurushia mawimbi vya simu za mkononi vilivyoko ardhini vitapokea na kusambaza mawasiliano kwa njia ya satellite kuunganisha na vile vya ndani ya ndege.Simu zitatozwa kupitia mitandao ya kawaida ya abiria.
Kwa kuanzia mfumo wa simu utakaotumika ni 2G pekee, japokuwa Ofcom imesema endapo kutakuwa na mafanikio, kutakuwa na uwezekano wa kuzindua kwa mfumo wa kisasa zaidi wa 3G na mingineyo mipya itakayoundwa siku za usoni
Bonyeza hapa kupata bbc Habari

Tuesday, August 28, 2007

Daniel Arap Moi aunga mkono Mwai Kibaki


Rais wa zamani Daniel arap Moi ametangaza msimamo wake kuhusu nani atakayemuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao na chaguo lake ni aliyekuwa mpinzani wake na sasa Rais Mwai Kibaki.
Akihutubia waandishi wa habari mjini Nairobi, Bwana Moi alisema kuwa Rais Kibaki anastahili kuungwa mkono kutetea kiti chake na kutawala kwa zamu ya pili.
Bwana Kibaki alikuwa mpinzani mkubwa wa Rais Moi ambapo waligombea urais mwaka wa 1992 na 1997.
Bwana Moi alitawala Kenya hadi mwaka wa 2002 ambapo, kisheria, hangeweza kugombea tena kiti hicho.
Alimuunga mkono mwanasiasa chipukizi, Uhuru Kenyatta wa chama cha KANU ambacho kilikuwa kimetawala Kenya kwa karibu miaka 40.
KANU kiling'olewa madarakani kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1963.
Bwana Moi aliwaambia wandishi wa habari kuwa Rais Kibaki hakuwa na ukabila na kwamba alikuwa anakuza umoja wa taifa na kuzingatia ajenda ya maendeleo.
Aliukosoa muungano wa ODM kwa kukosa utengamano. Chama cha KANU ni moja wapo wa vyama washirika wa muungano huo wa ODM.

Wednesday, July 4, 2007

Mwandishi wa BBC Gaza aachiliwa





.


Allan Johstone baada ya kuachiliwa
Sikiliza Dira ya DuniaMwandishi wa BBC katika Gaza, Alan Johnston, aliyeachiliwa usiku wa kuamkia leo baada ya takriban miezi minne ameshukuru juhudi za Kimataifa za kutaka aachiliwe.
Akizungumza kwa njia ya simu na wenzake wa BBC kutoka Ubalozi wa Uingereza mjini Jerusalem baada ya kuondoka GAZA, Bw Johnston amesema kuwa kwa bahati aliweza kuipata Redio na hivyo kuweza kufuatilia jitihada zilizokua zikifanywa kutaka aachiliwe, jambo ambalo lilimpa matumaini.
Hapo awali, akionekana mwenye afya nzuri ingawa mchovu , alielezea majuma kumi na sita ya kuzuiliwa kwake katika chumba kifinyu kama kuzikwa mzima.
Na wazazi wa Alan wameelezea idhaa ya Kiswahili ya BBC kwamba wamepata faraja kubwa isiyoelezeka kufuatia kuachiliwa kwake.
Babake Alan Bwana Graham Johnstone amesema asingependa mwanawe kurudi mashariki ya kati.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu