Saturday, November 29, 2008

Je tunakaa kama marafiki wapendwa au kama marafiki wanafiki

Play cheza Bonyeza chini
Mtoto wa kiume amepewa fundo kwenye koo lake ili anapopatwa na matatizo au mwenzako anapopatwa matatizo uonyeshe ujasili wako kwako au kwa mwenzako. Inabidi ule ubini-adamu wako ufanyike pale kwenye tatizo bila kujali nini utapata au nini utapoteza
Kumbuka sifa zimegawanyika katika sehemu nyingi, na kila mtu anapata sifa kutokana na juhudi zake mwenyewe au kutokana na tafu toka kwa rafiki mwema asiye taka kusifiwa kutokana na alilolifanya kwa mwenzie.
Kumbuka umepewa fundo ili usiwe unapayuka kila unaloliona unatakiwa uwe Dume kwelikweli na sio mpayukaji kwa kile wewe unachokiona kipo katika mwelekeo usioupenda wewe na sio wenzio. Kumbuka maisha ni mzunguko na maisha ni kujifunza kila siku na ujue hakuna aliye kamilika kwa kila kitu, jua mengi tunajifunza wakati unafanya kazi ila kinachotakiwa ni je! Wanakijiji wenzio ni wale wenye upendo kwako au ndio wengi wenye roho ya korosho. Kuweni rafiki wema wanakiji wenzangu na si rafiki mnafiki ili mwenyezi mungu atupe zaidi mema kuliko chuki binafsi kati yetu hapa duniani
Wenu
rafiki nipendaye kuwa mwema na si mnafiki
Cheza wimbo huu hapa

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu