Mramba na Daniel Yona waenda Mahakama Kuu
Al-Albadir ya"Rushwa Ni Adui wa Haki" na The Ngoma Africa Bandi
Kutokana na matukio ya hivi juzi kuwa mkondo washeria haumbagui mtu wa tabaka lolote hapa Tanzania kama utakuwa umekwenda kinyume au unashukiwa kuw aumekwenda kinyume cha sheria ya uvunjwaji wa katiba basi mkondo wa sheria utakuzoa!!!Matukio hayo ya kufikishwa mahakamani baadhi ya waheshimiwa na watumshi wa umma,wafanyibiashara wakubwa ndiko kunawafanya walio wengi kubaki mdomo wazi! na kujiuliza tumefikaje hapa? na tunaenda wapi?
Tukijalibu kutafuna kichwa na kusugua mawazo ya kupata jibu nilijaribu kuwatupia jicho na sikia wanamziki wetu katika baadhi ya nyimbo zao na kujiuliza hivi kweli haya wanayoimba yapo? au ndio kama wasemavyo waswahili kama hayapo! basi yanakuja!
Katika wimbo wao "RUSHWA NI ADUI WA HAKI" ulipo katika santuri "Anti-Corruption squard" Bendi ya The Ngoma Africa yenye makao yake ughaibuni Ujerumani,www.myspace.com/
unatia simanzi na uchungu,kwa maneno yaliopo ndani ya wimbo huo ambayo naweza
kusema maneno ya mistari ya tungo hizo kuwa ni darubini hiliyokuwa inaonyesha mfumo na mwenendo wa mlolongo wa rushwa,labda wimbo huo ulikuwa wito?pengine onyo na taadhari,pengine wimbo huo uliwakilisha kilio cha wengi! hatimaye naweza kuhuita au kuhutaja wimbo huo ni sawa na utabiri,labda ni al-albadir yaani kumshitakia mungu kama mtu kaibiwa na hamjui mwizi wake tujaribu kusikiliza wimbo huo hapa www.myspace.com/thengomaafrica