Ben Komba/Pwani-Tanzania/24/01/ 2012
Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Pwani, imeshukuru umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania kwa kuweka mikakati ya kukuza kiwango uandishi nchini, kwa kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusiana na kada hiyo kwa wanachama wake wote nchini.
Mratibu wa Klabu ya waandishi wa Mkoa wa Pwani, BI.MARGARET MALISA amesema hayo pembeni mwa warsha siku ya nne ya uandishi wa habari za vijijini ambayo yaliwashirikisha waandishi 18 kutoka vyombo vyenye uwakilishi Mkoani Pwani, ambapo amefafanua hatua hiyo ya kutoa mafunzo kuhusiana na uandishi wa habari za vijijini yatakayowawezesha kuandika habari kwa weledi.
Aidha ameaasa viongozi wa klabu za waandishi nchini kutekeleza majukumu yao kwa uwazi ili kujenga mshikamano na amani ndani ya klabu hizo, amewasisitizia kufuata taratibu zilizopo katika kuendesha klabu hizo ziweze kufikia malengo waliyojiwekea katika kudumisha maadili ya uandishi wa habari.
BI.MALISA akizungumzia kuhusiana na vikao vya kikatiba, amesema ni muhimu kuwepo kwa mikutano ya kikatiba ambayo inatoa fursa kwa wanachama kupata taarifa ya mapato na matumizi, na kuwekana sawa na kushauriana juu ya masuala mbalimbali yanayoziikabili klabu za waandishi wa habari nchini.
Mwezeshaji BW.ALLAN LAWA ameelezea adhima ya umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi wa habari nchini katika kuhakikisha wanayanyua viwango vyao katika uandishi wa habari za vijijini, katika kuchochea maendeleo ya kilimo nchini.
Amewasihi waandishi wa habari ambao tayari ni wanachama wa klabu za waandishi wa habari kutowabagua wenzao na ikiwezekana kuwashawishi ambao sio wanachama kujiunga nao, katika kuzipa nguvu klabu za waandishi nchini na kuepuka kuogopa mawazo mapya.
END.