Saturday, January 28, 2012

"Uzinjibari ":Siasa na Chaguzi-Dokezi la Watongowaji Kiswahili Omani.


"Uzinjibari ":Siasa na Chaguzi-Dokezi la Watongowaji Kiswahili Omani.

Hivi majuzi nilibahatika tu kusoma andiko la Bi Nafla Kharusi ,wa University ya Oman ,lenye kichwa cha hapo juu
ambalo limechapishwa  mapema tarehe 4 ya mwezi wa january 2012 .
Andiko hilo ni la kiuchunguzi na utafiti kina lilimenivutiya sana kwa sababu limeweka wazi na kudhirihisha mengi
kwa ufupi yanayozungumzwa kindani ndani kuhusu fikra za waarabu wa Zanzibar huko Arabuni pamoja na
waarabu wenye jinsia za mchanganyiko wa asili za Oman na afrika mashariki na ya kati.
 
Andiko hilo kwa kweli linakhusu sana "mindsets"/dhamirisho za Wazanzibari-waarabu waishio Omani,mahusiano yao
ya kila leo ya kijamii na changamoto za ujanisibisho wao ikiwa  ni Uafrika,Utanzania  au Uaarabu.
Suala la Utwii/Loyalty/Alligiance yao inatilia nguvu wapi katika suali la Utaifa ? 
 
Andiko lake Bi Nafla Kharusi ni zuri kulisoma kwa  sababu linachambua mengi na kutoa muangaza wa mambo tofauti
kuhusu zile "Mindsets" au fikra za waarabu  hawa amabao mimi ninawagawa kwa mafungu yafuatayo :
A)Arab-Zanzibaris  (B) Zanzibari-Arabs (C) Arab-Arab Forever (D) Waarabu-Wabara,
katika Tanganyika ,Rwanda,Burundi,na Congo etc.
 
Ninawagwa hivyo kwa sababu ya vile wanavyojinasibu na kujitekeleza zile identity  zao , kwa namna hi au ile
na wakati mwingine kujitokeza moja kwa moja na identity crises zilizowasakama vichwani katika maisha yao
ya kila leo .
Ingawaje wengi  wao maisha yao yametulia baada ya miaka nenda miaka rudi ya dhiki hadi kujaaliwa kupatwa
na faraji kwa kiasi fulani katika nchi za "kwao" arabuni ,lakini bado wangali katika kulega lega kuyakubali  yale
mabadiliko ya dharba na ukweli halisi ulivyo wa kijamii na mahusiano ya kibinaadam ya kileo.
 
Nafla Kharusi ameonyesha  kuwa zipo tofauti  nyingi za kimawazo na hekma  za vikundi hivyo ikiwa ni
kwa upande wa kimatabaka na hata kiitikadi  kuhusu mahusiano msingi ya kijamii.
Waarabu wa kundi la ( D ) yaani wale wasio iishi visiwani  fikira zao ni kinyume sana na zile za waarabu
A,B,C - waliokuwa wakiishi Zanzibar na hasa wale waishiyo Arabuni kwa hivi sasa.
 
Waarabu wa nje ya Unguja na Pemba /Zanzibar  yaani wa nchi jirani za Afrika Mashariki na ya Kati
wanaamini kwamba :
(A) ".... waarabu wa Zanzibar ni majeuri na wenye kupendeleana/nepotism na
wanapenda kujifanya wao wote  ni wajuwaji wa kila kitu".
 
(Nafikiri muandishi ametumia neno nepotism kusudi/kihikmatu badala ya kusema moja kwa moja kua ni watu
wabaguzi au ni mafashisti wa moja kwa moja )
 
(B) "... waarabu wa Zanzibar wanaoishi Arabuni ,wengi wao wanajifanya wao waarabu kuliko
hao waarabu wenyewe na wanajipenkeza ili kunyenyekea kupata promotions ..."
 
".....wakati mwingine hujidai kama hawajui kiswahili au hata kuwakataza watoto wao
kusema lugha ya Kiswahili hadharani na kuifanya lugha kama ni aibu .."
 
Katika page 10 kuna mmoja amejifakharisha kwa kusema hivi na ninanukua .
 
(C) " No I am not a Zinjibari.I am an Arab and an Omani.My tribal name reflects that.
So what if I speak Swahili ? So what if I was in Africa ?
If I was born in China,would I be considered Chineese ?
If a European was born in  Oman ,would he be considered an Arab ?Impossible !!
 
Matamshi kama haya ndio yale niliyokuwa nikiyazungumza mara nyingi kuhusu lile suala zima la
kitaifa na utwii /alligiance /loyalty ya watu wenye mindsets kama hizi ,jee kweli wanaweza kuwa na Imani
na pendo safi kwa  Uzanzibari nchi ya Afrika na Uaafrika  na Utaifa  wa Utanzania?
Nijiuliza masuala hayo kutokana  na namna wanavyojifakharisha ujinsiya wao kuliko ziwa la mwanzo
lililopitiya limini mwao lugha ya Kiswahili .
 
 
 
Katika page 15 yupo mmoja aliyesema hivi na ninanukua.
 
"Why should I speak Swahili ?
It is an alien languadge. I am an Arab not a Zinjibari.I think like an Arab .
Arab blood runs through me.
Arabic is my languadge,it expresses best my Arab Culture ".
 
Kimsingi sioni ubaya wowote wa mtu kama huyu kujivuniya kabila lake na Uaarabu wake .
Jambo hilo kwangu mimi halina utata kabisa kabisa,lakini cha kushangaza ni kwamba,wakati
wenyeji asili wa kiafrika nchini Tanzania - Bara na Visiwani wanapo jivunia Uaafrika wao kwa
mapana na marefu huwa wanatiliwa nongwa na kutaka kulazimishwa Wajinasibu kwa  ule
"Uzanzibari  wa kupinga kila kitu cha watu wa Bara " na kufikia kikomo kuwa  eti ni maajabu
kwa muafrika wa Msumbiji kuwa Mkaazi au raia wa Zanzibar - sababu ? eti ni Mmakonde au
ni Mmasai .
Yaani mindsets za hawa hawa wanaojivuniya  Uaarabu wao ,wao wanaona kuwa ni haramu kwa
Mmasai au Mmakonde kuwa Mkaazi wa Unguja au Pemba  au hata kua raia Mzanzibari .
Wao huwa wanasahau kuwa wapo Wazanzibari wengi kote duniani na wengi wao wachukuwa
tajnisi za uraia wa nchi hizo wanako ishii. Panapo kuja habari a Mmasai na Mmakonde ,mara
huwa wanazungumza kwa limi mbili za fitina na itikadi-chuki kwa njama za kuzidisha kwa kutumia
Uisilamu dhdi ya Wakristo na unafiki mwingineo .
 
Njama kama hizi za kupinga Uafrika na itikadi-chuki dhidi ya watu wengine wa bara la afrika ndizo 
zilizosababisha  ILE MISIBA YOTE MIKUBWA YA KABLA NA BAADA MAPINDUZI YA 1964.
 
 
 
YALIYO ANDIKWA NA BI S.KHARUSI ,hayashangazi  lakini yanasisimuwa na hata kudokeza  au
kuonyesha baadhi ya sababu a kwa nini palifanyika Mapinduzi Zanzibar dhidi ya Usultani na Ubwenyeye na kwa bahati
mbaya iliyowafika baadhi ya Waarabu na makabila mengine ya Wazanzibari -waliokuwemo na wasiokuwemo kwenye
ile misiba mikubwa iliyotokea ambayo inshaala haitatokea tena .
 
Cha Kustaajabisha ni kwamba ikiwa leo baada ya miaka 48 tokea Mapinduzi ya 1964 ,bado kuna baadhi ya
watu walio na hisia za kikabila/tabaka za kujiboresha kuliko binaadam wengine .Jee usalama na amani utapatikana
vipi wakati kuna watu ambao wanawaona Wamasai  au Wamakonde si binaadamu waliotimia au kustahiki kuwa
na haki sawa za Ukaazi au Urai wa Zanzibar? Wazanzibari  wangapi wanaoishi BARA  
  
Jee kule kuwepo kwa Wazanzibari  njee katika nchi mbali mbali kwa salama na amani haiwi ni somo pekee
la kuwafunguwa macho watimba kwiri kuhusu nini  mahusiano ya Kibinaadam na haki na usawa wa Binaadam ?
 
Au ndio  baada ya "Dhiki " ya yale yote yaliyotokea Wakati wa ; na baada ya MAPINDUZI ,
wameyasahau kwa sababu  sasa baada ya kupatikana hizo"Faraji " ndio Ujeuri na Madharau dhidi ya binaadam
wengine ndio unajitokeza tena pengine  Umezidi?
 
Jee wapo miongoni mwa hao waitwao "Wa Juni -Julai " ambao wanataka kujionyesha na kunyanyasa binaadam
wengine kwa sababu ya maposho ,mishahara minene na kwa sababu za asili na jinsia zao ?
 
Lugha na yanayosemwa katika  Paper ya utafiti kina ya  Bi Nafla Kharusi ,na ukifanisha na mengi
yanayozungumzwa  katika Zanzinet is very alarming kwa sababu za ule mgando wa kisiasa na Mindsets
za kijabari/ujeuri wa  kikale kabisa  ,lazima wajuwe Ubwenyeye huo umhapitiwa na wakati .
 
20 pages za Bi Nafla Kharusi ,zinasema mengi kiutfiti kina na kwa ufupi ,ni somo kwa wale wote wenye
uwezo wa  kuelewa  usayansi wa muandaliyo na ufananuzi wa fikra za jamii fulani ,jinsi wafikirivyo na muamko wao
wa hali ya mahusiano ya kijamii .
 
Waliobahatika kusoma wamesoma ;wale ambao bado basi ninahakika Wataweza kufaidika na  kutafakari kina
kwa utaalamu ulio andikwa hapo na yale yaliyodhihirishwa na  muandishi wa Paper Hiyo.
Nampa heko Bi Nafla Kharusi ,kwa jitihadi yake ya kuona ya ndani ya dhamirisho za Wazanje -Zinjibari,yeye
amepata mengi kwa sababu ya ustadi pekee kwa vile yeye ni "Mwandani" wa jamii anaekubalika na wale wote
waliohojiwa katika utafiti wa andiko lake .
 
 Wenu  mtafiti
     A.HASHIM

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu