Uchaguzi wa Kenya 2007 | |||||||||||||||||||||
Shughuli za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika Disemba 27 zimepamba moto, jumla ya wagombea saba wa urais na wa ubunge. Baada ya takriban miaka mitano katika madarakani, rais Mwai Kibaki, hivi karibuni alivalia kanzu ya kiislamu kwa mara ya kwanza hadharani katika sherehe za Idd. Mawaziri wake pia wamekuwa katika harakati za mikakati ya kuwafikia wapiga kura na kujakikisha wanawafurahisha kuvutia kura zao. Rais Kibaki anapigania wadhifa kwa awamu ya pili akiwa anatumia ilani ya uchaguzi yenye maswala 10 muhimu.
Mpinzani wake mkuu na aliyewahi kuwa swahiba, Raila Odinga, hata hivyo anaahidi katiba mpya katika kipindi cha miezi sita baada ya kuingia madarakani - swala ambalo lilisababisha yeye kuhitilafiana na rais Mwai Kibaki. Na vile vile amemwajiri Dick Morris, mshauri wa zamani wa maswala ya kisiasa wa rais Bill Clinton yeye pia, anayesifika kwa kumwezesha Clinto kushinda uchaguzi wa Marekani mwaka 1996. Mtaalam wa kuwajenga wanasiasa, Bw Morris baada ya kuwasili Kenya alisema kwamba wanasiasa wote wawili Clinton na Odinga wana sifa aliyoiita "mgombea wa watu" na kusema kwamba wote wanaelekeza nguvu zao kwa maswala yanayowagusa wananchi. Wakati Bw Kibaki alipoingia madarakani mwaka 2002, haraka haraka utawala wake ulitangaza elimu ya bure kwa wanafunzi wote wa shule za msingi. Kura za maoni zimekuwa zikionyesha kwamba rais Kibaki anatakiwa kufanya kazi kwa jitihada kama anataka kuwashinda wapinzani wake kupata awamu ya pili ya madaraka. Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga kutoka chama cha Orange Democratic Movement (ODM), pia amekuwa akitangaza ahadi zake za uchaguzi. Ahadi yake ya katiba mpya itaunda wadhifa wa waziri mkuu, kukabidhiwa baadhi ya madaraka na kukomesha utaratibu wa sasa wa kutegemea sana serikali kuu. Lakini baadhi ya wadadisi wa maswala ya kisiasa wamehoji, baada ya kuhangaika kwa miaka zaidi ya 10, je Bw Odinga anaweza kuaminika kupunguza madaraka ya rais kumpa waziri mkuu? Kinyang'anyiro cha kura Wakati huo huo katika mji mkuu Nairobi, ni kitovu cha shughuli zote za kisiasa na vigogo wote wanajiandaa kwa mapambano makali kugombea kura milioni 1.2 za watu waliojiandikisha. Wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa wametimuliwa mitaani wamerejea tena na kubanana njia na watumiaji wa barabara. Uchafu uliokuwa umesafishwa umeanza kukusanyika tena pole pole katika mitaa ya jiji la Nairobi. Baadhi ya wajumbe wa timu ya kampeni ya rais Kibaki, katika faragha wametetea kurejea kwa wafanyabiashara hao kwa matumaini kwamba hatua hiyo itavutia kura kwa rais Kibaki. Wafanyabiashara hao walisema wanatumia vyema fursa iliyojitokeza kabla mambo hayajabadilika, waliieleza BBC. "Tunajua ni kazi rahisi kwasababu ya uchaguzi... itakapofika Januari, hatutakuwepo hapa tunabangaiza tu kwa sasa." Katika jitihada za kujijenga zaidi kwa wafanyabiashara wa mitaani, rais Kibaki ameahidi kuwajengea masoko mapya endapo atachaguliwa tena. Msemaji wa serikali Dr Alfred Mutua amesema kwamba wafanyabiashara hao wamerejea Nairobi tu kwasababu ujenzi wa soko lao haujakamilika. Faida za maandalizi ya uchaguzi Baadhi ya wakenya wanapata faida za kipindi cha kuelekea uchaguzi: juma lililopita serikali ilitangaza nyongeza ya asilimia 16 ya mshahara kwa watumishi wa umma, malipo yakirejeshwa juma miezi sita. "Hii siyo sehemu ya kampeni, lakini endapo wanadhani ni jambo zuri na wakampigia kura rais Kibaki, hakuna tatizo kwa hilo," waziri anayeshughulikia utumishi kwa umma, Moses Akaranga alisema wakati akitoa tangazo hilo. Na kipindi fulani, katika hatua ambayo waangalizi wamesema imepangwa kuvutia kura za vijana, George Saitoti, ghafla alikumbuka kwamba wanafunzi 600,000 waliomaliza masomo ya sekondari, hawana vyeti vyao vya kuhitimu - vikiwa vimeshikiliwa na shule walikosoma kwa kushindwa kulipa ada. Waziri wa elimu aliagiza shule husika kutoa nyaraka husika - ambazo bila wasomi kuwa nazo hawawezi kutafuta ajira rasmi, akionya kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa walimu watakaoshindwa kufuata maagizo hayo. Msako wa kura
Vile vile mambo yalikuwa siyo rahisi kwa chama cha ODM ambacho kina uwingi watu wenye sifa za kugombea - wote wakiwania tikiti za chama hicho. Tatizo kama hilo pia linakikumba chama cha ODM-Kenya, ambacho kiongozi wake Kalonzo Musyoka alikuwa namba tatu kwa muda mrefu katika kura za maoni ya wagombea kiti cha urais. Hatma ya patashika zote hizi ni upigaji kura utakaofanyika siku ya Alhamisi tarehe 27.Endelea kufuatilia habari za uchaguzi kupitia matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC. | |||||||||||||||||||||