Mimi kama mwananchi wa kawaida ndani ya nchi yangu Tanzania.
Najaribu kuvuta taswira ya matukio yanayoendelea kutokea ndani ya nchi yetu Tanzania pande za Kibiti.
Tutazame katika upande wa imani zaidi kuliko kuanza kuhukumu kila mtu.
Ebu tuangalie ni nani anayetenda mambo haya, yasiyokuwa na mwelekeo katika tabia mila na tamaduni za kitanzania.
Mtazame huyu Mtanzania mwenye makabila zaidi ya mia na kitu.
Huyu Mtanzania aliye zaliwa na kukua Katika desturi za mchanganyiko wa makabila mbalimbali yanayofundisha malezi yenye kuheshima.
Huyu Mtanzania aliyesoma katika shule zenye mchanganyiko wa makabila na jinsia tofauti.
Huyu Mtanzania aliyesoma lugha ya Kiswahili kama lugha moja ya mawasiliano kwa wote.
Huyu Mtanzania, huyu Mtanzania anayeishi katika nchi yenye amani, yenye upendo na ukarimu kwa wageni.
Huyu Mtanzania mwenye umoja wa kitaifa uliojengwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nyakati hizo Nyerere alijenga umoja wa kitaifa kwa watanzania kupitia vijiji vya ujamaa na kujitegemea.
Hapa kilizaliwa kitu kinaitwa nguvu kazi kwa kila raia wa kawaida.
Wenye elimu zao, walifanya kazi katika serikali na mashirika mengine binafsi.
Yote ni kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa kawaida.
Wewe Mtanzania amka sasa na fungua macho yako, tazama mbele kwa umakini ili uepushe hizi uchocheezi wa kibaguzi.
Unaofanywa na wauaji wa raia wa tanzania kwa tamaa au chuki binafsi zinazoendelea kunyesha na watu wachache.
Tambua kile ambacho kinachoonekana sasa kama mauaji ya raia wenye haki ni hatari kwa kizazi hiki na kinachokuja.
Tambua yanayoendelea kupoteza haki kwa wenye haki na wasio na hatia ni kinyume na haki za binadamu duniani kote.
Jenga imani yako kwa kujenga upendo kwa wote
Kemea chuki yako uliyoijenga katika fikra zako kwa kuwaua wenye haki.
Jaribu kuitupa hiyo chuki yako mbali kama maandiko haya chini...
Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.
Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake.
Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.
Kama ulipewa uhai na muumba wa mbingu na nchi, basi basi kumbuka nawe ipo siku yako ya mwisho kama unavyo fanya kwa wengine wenye haki ya kuishi kama unavyoishi wewe.
Kazi ya shetani ni kuibomoa imani na kuupoteza ufalme wa Mungu.
Naye asema hivi..
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Tusimame kama watoto wa Baba na Mtanzania mwananchi wa kawaida mwenye upendo na nchi yake.
Kwa pamoja tutokomeze ili janga kubwa linalo chepukia katika maadili yetu.
Tusipo kemea na kulipinga leo, kesho litakuwa ni chaka kubwa la mateso kwetu.
Wenu
Kennedy Kimaro
www.kennedytz.blogspot.com