Friday, March 9, 2012
Naibu waziri aibiwa morogoro
Wajanja wamemliza naibu waziri mamilioni na kutoweka na nyaraka za serekali, huku wakiziacha silaha za waziri ndani ya chumba.
Posted by Unknown at 3/09/2012 10:40:00 PM
Nguvu ya raia inapofanya kazi na jeshi la polisi ni kulinda amani na si ...
Posted by Unknown at 3/09/2012 10:19:00 PM
Thursday, March 8, 2012
Siku ya wanawake Duniani
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/8/2012 8:10:29
Wanawake katika mkoa wa Pwani wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko mkoani Pwani, na hasa yakipata baraka za wanawake inawezekana.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, BI. MWANTUMU BAKAR MAHIZA ameyasema hayo wakati wa kilele cha siku ya wanawake iliyofanyik kimkoa katika wilaya ya Kisarawe yakiwa na kauli mbiu inayosema “ushiriki wa mtoto wa kike; ni chachu ya maendeleo endelevu”.
Ambapo ameongeza kuwa ikiwa kinamama wakiamua kutilia maanani elimu kwa mtoto wa kike na hasa katika kuhakikisha hapati mamba za utotoni na ndoa za umri mdogo kwa wazazi au walezi kuweka tama zao pembeni na kumkwamua motto wa kike mwenye kuhitaji elimu ili kuepukana na utegemezi.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, BI. MAHIZA amewaonya watoto wa kike kuacha kujilengesha kwa mafataki kwa kuvaa nguo ambazo kwa makusudi ya kuvutia wanaume na hasa ikizingatiwa wanaume wana hulka ya kutamani anapoona baadhi ya maeneo ya mwili yakiwa bila staha.
Onyo hilo limefuatia baadhi ya wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari Kibuta, iliyopo katika kata ya Kibuta, Tarafa ya Sungwi kijiji cha Kibuta kuingia kutoa burudani wakiwa wamevalia sketi zao katika makalio, na kuzaa mjadala mkubwa kwa waliohudhuria.
Awali akisoma risala ya kijiji, Mwananchi BI. FORTUNATA MAGESA ameiomba serikali kuangalia suala la huduma za jamii wilayani Kisarawe hususan katika kijiji cha Kibuta, ambapo upatikanaji wa wa huduma za maji kuwa mtihani mkubwa katika eneo lao na hivyo kuwasababishia dhiki kubwa kwao.
END.
Posted by Unknown at 3/08/2012 10:25:00 PM
Wednesday, March 7, 2012
Wanaharakati wanapokuja juu kwa mambo ya msingi na haki kwa kila kitu
Posted by Unknown at 3/07/2012 12:16:00 AM
Tuesday, March 6, 2012
Madokta wasusia vikao vya makubaliano
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka madaktari kurejea katika vikao vya makubaliano
Posted by Unknown at 3/06/2012 11:47:00 PM