Thursday, March 8, 2012

Siku ya wanawake DunianiBen Komba/Pwani-Tanzania/3/8/2012 8:10:29

Wanawake katika mkoa wa Pwani wametakiwa kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko mkoani Pwani, na hasa yakipata baraka za wanawake inawezekana.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, BI. MWANTUMU BAKAR MAHIZA ameyasema hayo wakati wa kilele cha siku ya wanawake iliyofanyik kimkoa katika wilaya ya Kisarawe yakiwa na kauli mbiu inayosema “ushiriki wa mtoto wa kike; ni chachu ya maendeleo endelevu”.

Ambapo ameongeza kuwa ikiwa kinamama wakiamua kutilia maanani elimu kwa mtoto wa kike na hasa katika kuhakikisha hapati mamba za utotoni na ndoa za umri mdogo kwa wazazi au walezi kuweka tama zao pembeni na kumkwamua motto wa kike mwenye kuhitaji elimu ili kuepukana na utegemezi.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, BI. MAHIZA amewaonya watoto wa kike kuacha kujilengesha kwa mafataki kwa kuvaa nguo ambazo kwa makusudi ya kuvutia wanaume na hasa ikizingatiwa wanaume wana hulka ya kutamani anapoona baadhi ya maeneo ya mwili yakiwa bila staha.

Onyo hilo limefuatia baadhi ya wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari Kibuta, iliyopo katika kata ya Kibuta, Tarafa ya Sungwi kijiji cha Kibuta kuingia kutoa burudani wakiwa wamevalia sketi zao katika makalio, na kuzaa mjadala mkubwa kwa waliohudhuria.

Awali akisoma risala ya kijiji, Mwananchi BI. FORTUNATA MAGESA ameiomba serikali kuangalia suala la huduma za jamii wilayani Kisarawe hususan katika kijiji cha Kibuta, ambapo upatikanaji wa wa huduma za maji kuwa mtihani mkubwa katika eneo lao na hivyo kuwasababishia dhiki kubwa kwao.

END.

0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu