Monday, July 24, 2017

Maisha ya vijana katika jiji la Makonda Dar es Salaam.

Maisha ya leo ni tafu Kwa vijana wa leo.
Najua unanishanga kunisikia nikisema jinsi nilivonena hapo juu.

Wewe Mtanzania tazama jinsi ulivyo kama wewe unavyo starehe kwa kujikimu na kutatua ukata wa maisha hapa ndani ya jiji la Makonda.

Najaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya maisha yetu yalivyogawanyika katika tabaka mbalimbali zenye tofauti ya maslahi.

Kabla ya kujikita katika gumzo na stori iliyopita mbele ya macho yangu na kuniweka katika tabaka la mawazo.

Najaribu kukuvuta mawazo yangu, ili nawe ufanye utafiti wenye njia iliyo na mistari sambamba yenye kukuonesha miangaiko wanayopitia wasio na uwezo katika jiji la Makonda.

Najua mawazo yako yatakimbilia kwa maskini walio wengi wanajulikana kama ombaomba wa mitaani.

Funga na fungua macho yako katika mtazamo wenye fikra zenye wigo mpana.

Tazama kwa umakini mkubwa kuwa jamii yenye umaskini si ombaomba tu.

Kuna watoto wengi wanaishi katika mazingira mgumu duniani kote.

Kuna watoto wanaofanyishwa kazi ngumu majumbani na maeneo yenye vita za wenyewe kwa wenyewe.

Tupia jicho lako utazame watoto wanaozaliwa na kutopewa malezi na wazazi wao na kupelekea kuwa watoto wa mitaani.

Jaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya familia maskini katika maisha ya kila siku jinsi wanayopata taabu za chakula nguo na mahitaji yao kwa ujumla.

Tazama maisha yako na uleule upande wa pili tupia jicho kwa familia maskini.

Jitazame chai yako ya asubuhi gharama yake ni shilingi ngapi!

Jitazame chakula chako cha mchana Chips kuku na vingine vya thamani bei yake ni kiasi gani.

Tazama wangapi wanakwenda kunachangia mchango angalau kidogo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Jaribu kuelewa ni nani mchango wako katika familia zisizojiweza katika maisha yao kila siku.

Ebu twende na mimi bega kwa bega upate kujua kipi ninacho.

Jumapili nikiwa katika gari eneo la Mataa ya kuelekea Msasani, wakati huo taa nyekundu zimewaka upande wetu.

Magari yanayotokea mjini kuelekea msasani yalikuwa yanapita,  upande mwingine kuna mistari ya pundamilia ya watembea kwa miguu kukatiza barabara.

Kukawa na kijana mmoja ukimtizama utamuona ni wa kawaida tu.
Cha ajabu uyo kijana mawazo yake hayakuwepo pale alipo.

Basi yule kijana akawa anavuka barabara bila ya kujali kuna gari linakuja au vipi?

Kufumba na kufungua gafla gari ikafungwa breki miguuni kwa yule kijana.

Ikabidi arudi nyuma ili gari lipite, tulipo mwambia kulikoni ndugu yetu huna macho.

Yule kijana akajibu ni maisha ndio yanafanya hivi.

Hapa tangu asubuhi sijaonja chochote kinywani.

Mchana umeshapita naungalia hivi hivi.

Kingine kinachonitesa hapa kwamba sijui nitafika vipi Mbagala wakati nipo msasani na sijui nipo katika dunia hii au vipi.

Sina hata sentano hapa mfukoni, ni taabu na shida katika maisha yangu.

Nakumbuka mimi ndio gari ya kwanza mbele, niliyaona yote yakitokea

Basi haraka nikatoa shilingi elfu moja na kumpa yule kijana.

Sikutegemea kitu alichokuwa akifanya yule kijana.
Alipiga magoti na kunishukuru huku machozi yakimtoka na akionyesha mikono juu kumshukuru Mungu.

Wakati huo taa za barabarani zinawaka kijani nasi tuliondoka.

Lakini njiani nikawa na uchungu wa moyo

Itaendelea
Wako
Kennedy Kimaro

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu