Tuesday, September 12, 2017

https://youtu.be/tirS_O1uVyw

Sunday, September 3, 2017

Monday, July 24, 2017

Maisha ya vijana katika jiji la Makonda Dar es Salaam.

Maisha ya leo ni tafu Kwa vijana wa leo.
Najua unanishanga kunisikia nikisema jinsi nilivonena hapo juu.

Wewe Mtanzania tazama jinsi ulivyo kama wewe unavyo starehe kwa kujikimu na kutatua ukata wa maisha hapa ndani ya jiji la Makonda.

Najaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya maisha yetu yalivyogawanyika katika tabaka mbalimbali zenye tofauti ya maslahi.

Kabla ya kujikita katika gumzo na stori iliyopita mbele ya macho yangu na kuniweka katika tabaka la mawazo.

Najaribu kukuvuta mawazo yangu, ili nawe ufanye utafiti wenye njia iliyo na mistari sambamba yenye kukuonesha miangaiko wanayopitia wasio na uwezo katika jiji la Makonda.

Najua mawazo yako yatakimbilia kwa maskini walio wengi wanajulikana kama ombaomba wa mitaani.

Funga na fungua macho yako katika mtazamo wenye fikra zenye wigo mpana.

Tazama kwa umakini mkubwa kuwa jamii yenye umaskini si ombaomba tu.

Kuna watoto wengi wanaishi katika mazingira mgumu duniani kote.

Kuna watoto wanaofanyishwa kazi ngumu majumbani na maeneo yenye vita za wenyewe kwa wenyewe.

Tupia jicho lako utazame watoto wanaozaliwa na kutopewa malezi na wazazi wao na kupelekea kuwa watoto wa mitaani.

Jaribu kuvuta picha na kuangalia jinsi ya familia maskini katika maisha ya kila siku jinsi wanayopata taabu za chakula nguo na mahitaji yao kwa ujumla.

Tazama maisha yako na uleule upande wa pili tupia jicho kwa familia maskini.

Jitazame chai yako ya asubuhi gharama yake ni shilingi ngapi!

Jitazame chakula chako cha mchana Chips kuku na vingine vya thamani bei yake ni kiasi gani.

Tazama wangapi wanakwenda kunachangia mchango angalau kidogo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Jaribu kuelewa ni nani mchango wako katika familia zisizojiweza katika maisha yao kila siku.

Ebu twende na mimi bega kwa bega upate kujua kipi ninacho.

Jumapili nikiwa katika gari eneo la Mataa ya kuelekea Msasani, wakati huo taa nyekundu zimewaka upande wetu.

Magari yanayotokea mjini kuelekea msasani yalikuwa yanapita,  upande mwingine kuna mistari ya pundamilia ya watembea kwa miguu kukatiza barabara.

Kukawa na kijana mmoja ukimtizama utamuona ni wa kawaida tu.
Cha ajabu uyo kijana mawazo yake hayakuwepo pale alipo.

Basi yule kijana akawa anavuka barabara bila ya kujali kuna gari linakuja au vipi?

Kufumba na kufungua gafla gari ikafungwa breki miguuni kwa yule kijana.

Ikabidi arudi nyuma ili gari lipite, tulipo mwambia kulikoni ndugu yetu huna macho.

Yule kijana akajibu ni maisha ndio yanafanya hivi.

Hapa tangu asubuhi sijaonja chochote kinywani.

Mchana umeshapita naungalia hivi hivi.

Kingine kinachonitesa hapa kwamba sijui nitafika vipi Mbagala wakati nipo msasani na sijui nipo katika dunia hii au vipi.

Sina hata sentano hapa mfukoni, ni taabu na shida katika maisha yangu.

Nakumbuka mimi ndio gari ya kwanza mbele, niliyaona yote yakitokea

Basi haraka nikatoa shilingi elfu moja na kumpa yule kijana.

Sikutegemea kitu alichokuwa akifanya yule kijana.
Alipiga magoti na kunishukuru huku machozi yakimtoka na akionyesha mikono juu kumshukuru Mungu.

Wakati huo taa za barabarani zinawaka kijani nasi tuliondoka.

Lakini njiani nikawa na uchungu wa moyo

Itaendelea
Wako
Kennedy Kimaro

Friday, July 21, 2017

Maisha ya vijana wa sasa.

Ebu tubige stori fupi  kidogo ya maisha ya vijana wa sasa.

Kila asubuhi baada ya kujiweka sawa kwa safari ya kibaruani.
Nilipata chai ya asubuhi kama kawaida. Nikabeba simu zangu mbili na funguo za gari yangu.

Nilitoka nje ya nyumba yangu kuelekea kwenye gari yangu.

Mama watoto na watoto wakaja kunifungulia Gqeti kama kawaida yao.

Wakati ninarudi nyuma na gari, uku niki seti redio station moja ili kupata taarifa za kila siku.

Kukawa na watangazaji katika kipindi kimoja cha asubuhi wakitafakari yaliyondikwa kwenye magazeti ya siku hiyo.

Kikubwa kilikuwa ni mwanasheria ambaye ni mwana siasa wakati alipogoma kutoka ndani ya mahakama kuepushwa kukamatwa na polisi.

Wakati huo mtangazaji mmoja a akitoa stori ya kibaka au mwizi sugu aliyekimbizwa mitaa ya kawe na kufananisha suala la yule mwanasiasa

Stori ilianza hivi, yule mwizi alipokuwa akakimbizwa na raia wenye uchungu wa kuibiwa kila mara nyakati za usiku wa manane.
Wakawa wanamkimbiza yule mwizi kimya kimya ili wamshikishe nidhamu ya kutorudia tabia ya wizi.

Yule mwizi kwa mwendo kasi akakatiza karibu na kituo cha polisi cha kawe.

Alipoangalia kwa mbele akawaona askari wamesimama eneo la mapokezi.

Moyoni akasema liwalo na liwe maisha ni matamu, nikipoteza muda nitapata kichapo cha nguvu na kupoteza maisha hapa.

Basi yule mwizi akaongeza mwendo kuelekea upande walipo askari polisi kituo cha kawe eneo la mapokezi na kusima nyuma yao.

Mtangazaji akaendelea kusimulia stori ya kibaka mwizi sugu.

Ndipo wale raia wema ilibidi wasimame gafla kwa kutoamini nini kilichotokea hadi mwizi kukimbilia upande wa kituo cha polisi.

Wale raia wema wakashauliana mmojawapo aende kuchukua yule mwizi sugu toka mikononi mwa polisi.

Ndipo njemba mmoja alichomoka na kuelekea alipo mwizi sugu katika kituo cha polisi.

Alipofika katika eneo ambapo yule mwizi mwizi chini ya ulinzi wa askari polisi 

Askari polisi wakamuliza yule raia mwema? Una shida gani kijana!

Naye akamjibu, nimekuja kuchukua ndugu yangu huyo hapo

Huyu ndugu yetu ana matatizo ya akili siku nyingi.

Kwa sauti kubwa yule mwizi akajibu, Muongo Muongo mimi ni mwizi na wanataka kuniua.

Wakati polisi wakiwa katika mshangao kwa yote yanayotokea

Mara yule raia mwema akawa anajeuka upande mwingine ili kurudi nyuma gafla chuma kizito kikaanguka kutoka mfukoni mwake.

Basi yule mwizi akasema unaona askari chuma alichobeba anataka kuniua huyu.

Kumbe yule mwizi naye anajua kazi ya askari ni kuleta amani pale palipo na machafuko.

Kazi ya  askari kusikiliza pande zote mbili zenye malalamiko ili kufanya uchunguzi na kujua nani ni mkosaji.

Askari alichofanya ni kuwakamata wote wawili na kuwakilisha chini mapokezi kwa muda.

Najua unanishanga Kwanini wote wawili na si akamatwe yule mwizi sugu.

Wakati huyu ni mwizi na amekuwa akifanya wizi  leo na siku zote za ujana wake.

Yule askari akaja na karatasi za kuandika ripoti ya kesi iliyopo mbele yake.

Wa kwanza kuitwa kutoa maelezo yake ni yule  mwizi sugu kwa yeye ndiye wa kwanza kufika kituo cha polisi.

Askari akaanza.. Unaitwa nani ndugu yangu.

Mwizi akajibu.. Naitwa... .

Una miaka mingapi!

Mwizi akajibu kumi na saba!√

Unaishi wapi

Mwizi akajibu kivukoni!

Kwanini umekuja hapa katika kituo cha polisi!

Mwizi..  Kimya

Askari akamgeukia tena yule mwizi sugu na swali lile lile.

Mwizi Sugu Kimya tena.. 

Basi askari polisi  akumweleza kama huna jibu basi nitakukabizi kwa ndugu yako.

Yule mwizi sugu akajibu

Wataniua Watamuua.. Huyu siyo ndugu yangu kwanza simjui huyu huku akilia

Ndipo yule askari polisi akamuuliza swali lile mara ya tatu

Mwizi akajibu

Yeye ni mwizi na kazi zake mchana ni

mpiga debe wa daladala na usiku wanajikusanya na kuiba katika nyumba za watu au vifaa katika magari.

Askari akamwambia weka sahihi yako katika maelezo haya.

Mwizi sugu akachukua peni na kumwaga wino au sahihi katika maelezo yake.

Askari akamchukua na kumweka ndani mpaka siku inayofuata.

Jaribu kuwaza askari polisi alifanya maamuzi gani kwa yule raia mwema.

Mwisho
Kennedy Kimaro
@kennedytz2

Tuesday, July 11, 2017

Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; 

Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 
ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 

ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. 

Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu. 

Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. 

Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; 

ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe. 

Sunday, July 2, 2017

Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema

Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.

Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema,

Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?

Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.

Saturday, July 1, 2017

Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu.

Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.

Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;

Thursday, June 29, 2017

SIPATI PICHA NA MATUKIO YA KIBITI

Mimi kama mwananchi wa kawaida ndani ya nchi yangu Tanzania.

Najaribu kuvuta taswira ya matukio yanayoendelea kutokea ndani ya nchi yetu Tanzania pande za Kibiti.

Tutazame katika upande wa imani zaidi kuliko kuanza kuhukumu kila mtu.

Ebu tuangalie ni nani anayetenda mambo haya, yasiyokuwa na mwelekeo katika tabia mila na tamaduni za kitanzania.

Mtazame huyu Mtanzania mwenye makabila zaidi ya mia na kitu.

Huyu Mtanzania aliye zaliwa na kukua Katika desturi za mchanganyiko wa makabila mbalimbali yanayofundisha malezi yenye kuheshima.

Huyu Mtanzania aliyesoma katika shule zenye mchanganyiko wa makabila na jinsia tofauti.

Huyu  Mtanzania aliyesoma lugha ya Kiswahili kama lugha moja ya mawasiliano kwa wote.

Huyu Mtanzania, huyu Mtanzania anayeishi katika nchi yenye amani, yenye upendo na ukarimu kwa wageni.

Huyu Mtanzania mwenye umoja wa kitaifa uliojengwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nyakati hizo Nyerere alijenga umoja wa kitaifa kwa watanzania kupitia vijiji vya ujamaa na kujitegemea.

Hapa kilizaliwa kitu kinaitwa nguvu kazi kwa kila raia wa kawaida.

Wenye elimu zao, walifanya kazi katika serikali na mashirika mengine binafsi.
Yote ni kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa kawaida.

Wewe Mtanzania amka sasa na fungua macho yako, tazama mbele kwa umakini ili uepushe hizi uchocheezi wa kibaguzi.

Unaofanywa na wauaji wa raia wa tanzania kwa tamaa au chuki binafsi zinazoendelea kunyesha na watu wachache.

Tambua kile ambacho kinachoonekana sasa kama mauaji ya raia wenye haki ni hatari kwa kizazi hiki na kinachokuja.

Tambua yanayoendelea kupoteza haki kwa wenye haki na wasio na hatia ni kinyume na haki za binadamu duniani kote.

Jenga imani yako kwa kujenga upendo kwa wote

Kemea chuki yako uliyoijenga katika fikra zako kwa kuwaua wenye haki.

Jaribu kuitupa hiyo chuki yako mbali kama maandiko haya chini...

Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. 

Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. 

Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. 

Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Kama ulipewa uhai na muumba wa mbingu na nchi,  basi basi kumbuka nawe ipo siku yako ya mwisho kama unavyo fanya kwa wengine wenye haki ya kuishi kama unavyoishi wewe.

Kazi ya shetani ni kuibomoa imani na kuupoteza ufalme wa Mungu.

Naye asema hivi..

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 

Tusimame kama watoto wa Baba na Mtanzania mwananchi wa kawaida mwenye upendo na nchi yake.

Kwa pamoja tutokomeze ili janga kubwa linalo chepukia katika maadili yetu.

Tusipo kemea na kulipinga leo, kesho litakuwa ni chaka kubwa la mateso kwetu.

Wenu
Kennedy Kimaro
www.kennedytz.blogspot.com

Sunday, June 25, 2017

ANGALIENI MTU AWAYE YOTE ASIMLIPE MWENZIWE MABAYA KWA MABAYA

Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 
10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala. 
11 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. 
12 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; 
13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi. 
14 Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. 
15 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. 

UFALME WA MUNGU HAUJI KWA KUCHUNGUZA

Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; 
wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. 

Thursday, June 22, 2017

Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa matari na kinubi wamwimbie.
Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

Wednesday, June 21, 2017

MAFUNZO YA MAISHA YETU NI HAPA HAPA DUNIANI

Jamani ndugu zangu wapendwa, leo tarehe 21 june 2017 muda wa asubuhi nikiwa natoka nyumbani kuelekea Kazini nje ya geti machozi yaliyotoka kwa kile nilichokiona.

Siku zote mama watoto ndie unifungulia geti ili nitoke nje,  lakini leo niliamua kufungua mwenyewe.

Nilipofungua geti tu mara nikamuona jamaa mmoja akipita karibu na geti letu na kunitazama mara moja akarudisha uso wake mbele na kuendelea na safari yake.

Nilipigwa na mshangao kwa sekunde kadhaa, kumbukumbu zangu zikiniambia ninamfahamu huyo jamaa.
Yule jamaa alikuwa amebeba mfuko mkubwa ndani yake kuna chupa chakavu za plastiki au PET.

Ndugu yangu wee wacha tu. Kwa sauti kubwa nikamuita yule jamaa fulani fulani simama huku nikisema "ata kama upo katika mazingira magumu lakini mimi siwezi kuacha kukusalimia"

Akasimama na kurudi nyuma nilipo, kwa mshangao machozi  yakinitoka kidogo  dogo na simanzi ya huruma  inatawala juu yangu jinsi alivyo na mapito ya maisha anayopitia kwa sasa.

Najua bado unajiuliza maisha yake yalikuwa vipi na kwa nini machozi yanitoke.

Huyu kijana alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na nafasi nzuri ya kipato kizuri kwa mwezi.

Alikuwa akifanya biashara yake binafsi ya kupiga picha.

Alikuwa ni mwangaikaji katika kazi zake za kila siku.

Jirani mwema na mtanashati na mcheshi wa mienendo yake.

Angalia maisha yalivyo na kitendawili kwa binadamu.

Unayotenda leo ni yale utendayo sasa hapa duniani, na kesho ni siku yako mpya katika matendo yako utayoyatenda siku hiyo hapa hapa duniani.

Jifunze matendo mema kabla ujachelewa ili ujenge nafsi iliyo safi kwa imani uliyopewa na Mungu wetu.

Mwangalie huyu kijana jinsi alivyokuwa mwanzo na sasa jinsi maisha yake yavyoenda.

Ni tofauti na jana amekuwa kijana yule yule lakini tabia na mwelekeo umebadilika kabisa, toka mtanashati mpaka muokota chupa zilizotupwa mitaani.
Uchungu wa moyo wangu ndio kichocheo cha kuandika makala hii fupi.

Ndugu yangu Amini maisha ni fundisho tosha kwa wengine.

Na leo yako sio sawa na kesho yako.

Wako
Kennedy Kimaro
kimarokenny@gmail.com

Saturday, June 17, 2017

NJIA YA MTU MBAYA NI CHUKIZO KWA BWANA

Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake. 
Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali humpenda mtu afuatiaye wema. 

Friday, June 16, 2017

MIMI NIMEMWINIUA KATIKA HAKI

Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema Bwana wa majeshi.

Thursday, June 15, 2017

Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi;

Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi;
Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu;
Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. 

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu