Wednesday, June 21, 2017

MAFUNZO YA MAISHA YETU NI HAPA HAPA DUNIANI

Jamani ndugu zangu wapendwa, leo tarehe 21 june 2017 muda wa asubuhi nikiwa natoka nyumbani kuelekea Kazini nje ya geti machozi yaliyotoka kwa kile nilichokiona.

Siku zote mama watoto ndie unifungulia geti ili nitoke nje,  lakini leo niliamua kufungua mwenyewe.

Nilipofungua geti tu mara nikamuona jamaa mmoja akipita karibu na geti letu na kunitazama mara moja akarudisha uso wake mbele na kuendelea na safari yake.

Nilipigwa na mshangao kwa sekunde kadhaa, kumbukumbu zangu zikiniambia ninamfahamu huyo jamaa.
Yule jamaa alikuwa amebeba mfuko mkubwa ndani yake kuna chupa chakavu za plastiki au PET.

Ndugu yangu wee wacha tu. Kwa sauti kubwa nikamuita yule jamaa fulani fulani simama huku nikisema "ata kama upo katika mazingira magumu lakini mimi siwezi kuacha kukusalimia"

Akasimama na kurudi nyuma nilipo, kwa mshangao machozi  yakinitoka kidogo  dogo na simanzi ya huruma  inatawala juu yangu jinsi alivyo na mapito ya maisha anayopitia kwa sasa.

Najua bado unajiuliza maisha yake yalikuwa vipi na kwa nini machozi yanitoke.

Huyu kijana alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na nafasi nzuri ya kipato kizuri kwa mwezi.

Alikuwa akifanya biashara yake binafsi ya kupiga picha.

Alikuwa ni mwangaikaji katika kazi zake za kila siku.

Jirani mwema na mtanashati na mcheshi wa mienendo yake.

Angalia maisha yalivyo na kitendawili kwa binadamu.

Unayotenda leo ni yale utendayo sasa hapa duniani, na kesho ni siku yako mpya katika matendo yako utayoyatenda siku hiyo hapa hapa duniani.

Jifunze matendo mema kabla ujachelewa ili ujenge nafsi iliyo safi kwa imani uliyopewa na Mungu wetu.

Mwangalie huyu kijana jinsi alivyokuwa mwanzo na sasa jinsi maisha yake yavyoenda.

Ni tofauti na jana amekuwa kijana yule yule lakini tabia na mwelekeo umebadilika kabisa, toka mtanashati mpaka muokota chupa zilizotupwa mitaani.
Uchungu wa moyo wangu ndio kichocheo cha kuandika makala hii fupi.

Ndugu yangu Amini maisha ni fundisho tosha kwa wengine.

Na leo yako sio sawa na kesho yako.

Wako
Kennedy Kimaro
kimarokenny@gmail.com

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu