Saturday, November 29, 2008
Play cheza Bonyeza chini
Mtoto wa kiume amepewa fundo kwenye koo lake ili anapopatwa na matatizo au mwenzako anapopatwa matatizo uonyeshe ujasili wako kwako au kwa mwenzako. Inabidi ule ubini-adamu wako ufanyike pale kwenye tatizo bila kujali nini utapata au nini utapoteza
Kumbuka sifa zimegawanyika katika sehemu nyingi, na kila mtu anapata sifa kutokana na juhudi zake mwenyewe au kutokana na tafu toka kwa rafiki mwema asiye taka kusifiwa kutokana na alilolifanya kwa mwenzie.
Kumbuka umepewa fundo ili usiwe unapayuka kila unaloliona unatakiwa uwe Dume kwelikweli na sio mpayukaji kwa kile wewe unachokiona kipo katika mwelekeo usioupenda wewe na sio wenzio. Kumbuka maisha ni mzunguko na maisha ni kujifunza kila siku na ujue hakuna aliye kamilika kwa kila kitu, jua mengi tunajifunza wakati unafanya kazi ila kinachotakiwa ni je! Wanakijiji wenzio ni wale wenye upendo kwako au ndio wengi wenye roho ya korosho. Kuweni rafiki wema wanakiji wenzangu na si rafiki mnafiki ili mwenyezi mungu atupe zaidi mema kuliko chuki binafsi kati yetu hapa duniani
Wenu
rafiki nipendaye kuwa mwema na si mnafiki
Cheza wimbo huu hapa
Soma Risasi
Katika hali ya kushangaza, wavunja mbavu wa Kundi la Ucheshi la Orijino Komedi walikamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kutinga mahakamani hapo kwa nia ya kuwaigiza mawaziri wa awamu ya tatu, Basil Mramba na Daniel Yona...
| |||
Wakili maarufu kutoka Marekani John Cochran amekuja nchini Tanzania kumtetea Dina katika kesi ya mauaji inayomkabili na anafanikiwa kumwokoa na kifo cha kunyongwa baada ya kutumia kipengele cha umri alipokuwa wakati anaua, Dina alikuwa na miaka kumi na sita wakati huo. Kifungo chake kinabadilishwa na kuwa cha maisha jela! Ni siku ya masikitiko makubwa kwa watu wengi lakini kwa Dina ni ahueni kwani kwake ni bora kutumikia kifungo cha maisha akiendelea kuwaona watoto wake kuliko kunyongwa na kufa! Dk. Ian Duncan na watoto wa Dina wanashindwa kujizua na machozi kuwabubujika wanapomwona Dina akipakiwa ndani ya Karandinga la Polisi tayari kwa kupelekwa gerezani. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO… |
Posted by Unknown at 11/29/2008 10:04:00 AM
Friday, November 28, 2008
|
Posted by Unknown at 11/28/2008 11:49:00 AM
Subscribe to:
Posts (Atom)