Saturday, November 29, 2008

Soma Risasi

Katika hali ya kushangaza, wavunja mbavu wa Kundi la Ucheshi la Orijino Komedi walikamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kutinga mahakamani hapo kwa nia ya kuwaigiza mawaziri wa awamu ya tatu, Basil Mramba na Daniel Yona...

The Sex Slave -50

hadithi za Shigongo
Wakili maarufu kutoka Marekani John Cochran amekuja nchini Tanzania kumtetea Dina katika kesi ya mauaji inayomkabili na anafanikiwa kumwokoa na kifo cha kunyongwa baada ya kutumia kipengele cha umri alipokuwa wakati anaua, Dina alikuwa na miaka kumi na sita wakati huo. Kifungo chake kinabadilishwa na kuwa cha maisha jela!

Ni siku ya masikitiko makubwa kwa watu wengi lakini kwa Dina ni ahueni kwani kwake ni bora kutumikia kifungo cha maisha akiendelea kuwaona watoto wake kuliko kunyongwa na kufa! Dk. Ian Duncan na watoto wa Dina wanashindwa kujizua na machozi kuwabubujika wanapomwona Dina akipakiwa ndani ya Karandinga la Polisi tayari kwa kupelekwa gerezani.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Posted by Picasa

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu