Tuesday, November 25, 2008

Leo ni Leo waliokuwa mawaziri wawili wafikishwa mahakama ya kisutu

Leo katika mahakama ya kisutu ilikuwa ni mshangao wa wengi kwani

wale mawaziri wa zamani ndugu Basil P Mramba{fedha} na ndugu Daniel Yona {Nishati na madini}

walitinga ndani ya mahakama hiyo kwa makosa ya kutumia nafasi zao vibaya pili kuitia serikali hasara ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa watanzania. Hii ni changamoto kwa viongozi wote kuwa unapofanya utumbo kupitia nafasi uliyopewa na wananchi basi malipo ndio hayo.

Hiyo ni chachu kwa wale wote waliofanya makosa kama hayo kusimama katika sheria nakujibu kama kweli wao ni wasafi au ndio wale walio wengi katika jamii yetu.

Katika jamii yetu ya Tanzania walio wengi wamejipatia mali kwa rushwa na asilimia kumi katka mikataba mingi hapa Tanzania inayopelekea watu kulipwa mabilioni kwa faida binafsi

Mpaka sasa wamesomewa makosa 13, kazi kwao waionesha jamii wamesimama upande upi wa sarafu! Na sheria ifanye kazi yake kama inavofanya kwa walio wengi katika magereza mbali mbali wakitumikia vifungo vyao

Picha zote ni kutoka kwa Father Kidevu anayepatikana Hapa au tumia hii http://www.mrokim.blogspot.com/

Aksante sana


Posted by PicasaP

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu