Maombi yetu katika janga hili la Coronavirus (COVID-19)
Binadamu tupo njia panda na janga hili la coronavirus hapa duniani.
Imani yangu inaniambia niwe na nafasi ya ya subira kwani tupo katika kipindi cha mapito ya maumivu hapa duniani.
Najaribu kuvuta mawazo kile kinachoendelea kutokea katika nchi zilizo juu kiuchumi hapa duniani.
Angalia ugonjwa huu wa homa ya mafua ya Coronavirus unavyoangamiza watu hapa duniani.
Sisemi watu wanakufa bali sina la kusema ila nabaki nikiangalia jinsi ili janga la ugonjwa wa mafua ya Coronavirus (COVID-19) yanavyosambaa sehemu moja kwenda nyingine hapa duniani.
Tunaonekana wanyonge katika fikra zetu huku tukisimama pamoja kutafuta njia ya kutokomeza mafua ya corona hapa duniani.
Angalia Coronavirus (COVID-19) inavyo safiri nchi moja kwenda nyingine kwa spidi kubwa yenye kutufanya kuwa na uoga kutokana na watu wengi kupoteza maisha na uchumi kuyumba hapa duniani
Tena nchi zilizo mbele kiteknolojia na uchumu mkubwa ndizo zilizo na wagonjwa wengi wa. Coronavirus (COVID-19) hapa duniani.
Sina cha kusema na nanyamaza kimya huku nikizidisha maombi yangu kwa Yesu kristo ili afikishe maombi yetu kwa Baba mwenyezi Mungu kusikia vilio vyetu hapa duniani.
Maisha yetu yapo katika kuangaika na janga la Coronavirus (COVID-19) lililo mbele yetu kama fumbo lenye kusubiri jibu lake hapa duniani.
Kila kitu kina sababu yake kutokea nasi tunamuomba mwenyezi Mungu atuzawadie uwezo wa kutambua tupo wapi na tuelekee wapi kupambana na janga la Coronavirus (COVID-19) hapa duniani.
Amini ni yeye aliyetufanya sisi binadamu tuwe na ubongo wenye akili ya kufundishika tofauti na viumbe vingine hapa diniani
Basi sisi sote kwa umoja wetu tuongeze maombi yetu kwake ili janga la Coronavirus (COVID-19) lipate kumalizwa na kupata kinga yake hapa duniani.
Wako
Kimaro