Thursday, December 12, 2019

https://www.forbes.com/sites/peterdetwiler/2019/12/11/inverters-the-unsung-hero-of-the-global-emerging-energy-economy/

https://www.pv-magazine.com/2019/11/27/new-methodology-for-assessing-value-of-pv-in-uncertain-markets/?utm_source=Bibblio&utm_campaign=Internal

https://www.pv-magazine.com/2019/12/11/neural-networks-improving-solar-power-forecasting/

Saturday, September 21, 2019

SIMULIZI YA MZUNGUKO WA MAISHA YETU YA KILA SIKU

Leo tarehe 21 sept 2019 Jumamosi ilikuwa siku ya kawaida kwangu Kama jumamosi nyingine.

Niliamka muda ambao uwa ni kawaida yangu siku zote.

Nilichukua mswaki nikaweka dawa ya mswaki ninyotomia kila siku aina ya whitening.

Uwa natoka nje ili nijifanyie mazoezi kidogo kupasha mwili moto na kuweka viungo sawa.

Niliondoka nyumbani saa mbili na dakika kadhaa nikawa nipo nje ya muda ambao sio rafiki

Nilipofika maeneo ya jirani na kazini nilienda kutafuta chapati moja ili niweke na ndizi nilizowekea na mke wangu kipenzi.

Kulikuwa hakuna chapati kisa anayezikaanga mkaa ulikuwa aujakolea moto..

Nikawasha gari kuelekea kazini.

Pembeni kulikuwa na vibanda vya mama lishe zaidi ya kimoja.

Katika kibanda kimojawapo walikuwepo wafanyakazi wenzangu wawili.

Ilinibidi nipaki gari  karibu na walipopaki gari lao.

Nilipofika tukasalimiana nao uku nikivuta kiti na kukaa.

Wao walikuwa wakisubiri kifungua kinywa walicho kiagiza asubuhi hiyo.

Nikajeuka upande waliopo mama rishe na kuwauliza mtori upo.

Nilijibiwa na mmoja wao upo tele.

Nikawaambia lazima niuonje kwanza kabla ya kunywa.

Wakati nasubiria ili niuone uo mtori

Kumbe wenzangu nao walikuwa wanasubiri mtori pia.

Ukaletwa mtori wao bakuli mbili na chapati moja kwa kila bakuli.

Nami nikasema nipewe  mtori kama ulioletwa kwa wenzangu.

Wakati bakuli yangu yenye mtori na chapati inafika mezani,

Kwa mbali Mzee mmoja alikuwa anakuja upande wetu akiwa mnyonge na upole kidogo.

Nikanyanyua kijiko na kuonja ule mtori kama unafikia kiwango cha kufanana na mtori.

Nilipouonja testi yake ilikuwa mtori ni mwepesi sana wakati kawaida ya mtori ndizi zinakuwa nyingi kuliko maji.

Nikauliza ni shilingi ngapi bakuli moja na chapati moja.

Kwa mbali mama lishe akanijibu ni elfu moja na mia mbili hivi.

Wakati huo yule babu alikuwa amefika karibu yetu

Nilipomuona tu na onyonge wake, basi kama kawaida yangu huruma umetawala fikra zangu

Mungu akaniambia msaidie huyo mzee hili asubuhi iwe ya furaha kwake pia.

Bila kusita nikajeuka kwa  yule mzee na kumwambia karibu upate mtori huku unikitumia jina babu.

Yule Mzee  akacheka kwanza na kusimama pale alipo kwa sekunde chache.

Mzee akajeuka upande wetu na kuelekea katika  meza iliyo karibu yake.

Alivuta kiti na kukaa kusubiria aletewe mtori na mama lishe.

Ndipo nilpowajeukia mama lishe na kuwasisitiza walete mtori kwa Mzee.

Najua unashangaa kuona natoa hisani ya mtori kwa huyo mzee na nimepata wapi nguvu kama hiyo.

Nguvu ya Upendo kwa binadamu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe  inatokana na upendo wa Yesu kwetu.

Yesu litenda maajabu na kutufundisha mengi yenye hekima ili iwe mifano na mafunzo kwetu daima milele.

Katika safari zake nyakati hizo watu walikuwa wakimfuata ili wasikilize mafundisho yake.

Ndipo siku moja walipokusanyika watu wengi na kukosekana chakula cha kuwapa

Ndipo

Yesu alichukua vipande mikate na Samaki ili wote waliofika katika mkusanyiko wapate chakula.

Nguvu ya kuwalisha umati wa watu alionyesha Yesu ni nguvu ya Mungu baba kwetu ili sisi kupata msamaha wa dhambi zetu.

Nikatoa noti ya elfu kumi na kumpa mama lishe.

Ili iwe malipo ya mtori kwa sisi watatu na yule babu.

Mama lishe akanipa chenji yangu  nami nikaipokea na kuiweka mfukoni tayari kwa kuondoka eneo hilo.

Sisi tulielekea kazini kama kawaida yetu Ila muda huo tukawa tumechelewa kidogo.

Tulianza kazi kama kawaida, tulishambulia kazi zilizokuwa zimebaki jana yake na kuzimaliza zote.

Tukaendelea kufanya kazi zote za siku hiyo ya jumamosi.

Ilipokaribia saa tano nilienda kuchukua diary yangu ili nienda katika kikao cha kila siku.

Tulipotoka katika kikaoni tukaunganisha kikao kingine cha pili.

Kawaida ya kila jumamosi panakuwa vikao viwili tofauti.

Kumbuka muda unasonga mbele bila kumngojea yeyote hapa duniani.

Ilipofika saa saba ikawa nimemaliza majukumu yangu yote ya siku hiyo.

Nilianza kijitayalisha kurudi nyumbani kwa mapumziko ya jummosi.

Nikawa napanga nikapate chakula cha mchana aina ya ugali na makange kule ninapoenda kula kila jumamosi.

Unajua ugali ukiwa wa moto na mboga ni rosti ya nyama yenye pilipili kwa mbali iliyochaganyika na mbogamboga na matunda ni Burudani sana.

Mara nikakumbuka kuwa watoto wanaitaji vitabu kwa ajili ya shule na leo nina nafasi ya kwenda kuwatafutia.

Nikachukua simu yangu nakumpigia  mama wawili  mke wangu ili afanye mambo mawili.

1. Aje kuchukua begi langu la ofisni hapo barabarani, kwani sitapitia nyumbani kwa wakati huo.

2. Anitumie  picha za vitabu vinavyotakiwa katika WhatsApp  yangu.

Nilitoka maeneo kazini na usafiri wangu  mpaka kituo cha mafuta  kilicho karibu.

Nilienda hapo hili kuongeza mafuta kidogo na kuangalia tairi za gari kama zina upepo Wa kutosha, kwa sababu ni siku nyingi sijaongeza upepo katka tairi zote.

Nilifanikiwa kuongeza mafuta tu Ila upepo haikuwezekana kwa sababu kulikuwa na foleni nami nikaona natachelewa kufika kariakoo.

Ilibidi niondoke hapo na kuendelea na safari yangu ya Kariakoo.

Nilipofika karibu na nyumbani nilimkuta mama wawili njiani akinisubiri, nilimpa begi langu nami nikaendelea na safari yangu ya Kariakoo.

Nilipofika maeneo ya tangibovu ilinibidi niingie kituo cha mafuta. Ili niongeze upepo tairi zote.

Zoezi ilo lilifanikiwa hapo katika kituo cha mafuta cha oil com

Safari ilianza hapo mpaka taa za kuongoza magari kona ya kuelekea kawe eneo la lugalo kambi ya jeshi.

Kituo cha pili kikawa taa za kuwavusha wanafunzi maeneo ya makongo.

Hapa kuna taa kwa ajili ya wanaotembea kwa mguu kuvuka njia nne bila shida.

Mtu yeyeto akiwa upande wowote anabonyeza kitufe na taa nyekundu inafuata ili nagari yasemame kuwapa watu fulsa ya kuvuka bila matatizo.

Kituo cha tatu kikawa taa za kuongoza magari njia nne mwenge kushoto kuelekea kiwanda cha soda cha cocacola na upande wa kulia ni kwenda mlimani city.

Tunapotoka hapo tukanyosha moja kwa moja

Kituo kilichofuata ni taa za kuongoza magari BamagaTBC. kona ya kwenda sinza na upande wa kushoto studio za TBC.

Tulipotoka TBC tukafika taa za kuongaza magari zamani palikuwa. panaitwa maji mchafu au sasa  sayansi TTCL hapo taa zilikuwa kijani  tukapita bila kusimama.

Unajua bahati uonekana mapema asubuhi nilipofika moroko kwenye njia panda kushoto ni kuelekea msasani na kulia kwake ni barabara ya kinondoni.

Mimi nikiwa natokea Mwenge naelekea mjini hapo tukanyosha moja kwa moja.

Kwa sababu taa za kutongoza magari zilikuwa kijani hakuna kusimama hapo moroko traffic light.

Tulipofika taa za Namanga kona ya kwenda msasani tulipunguza mwendo kidogo na kusimama hapo kwa sekunde chache.

Taa zilipowaka kijani tukaenda taratibu mpaka taa za kona ya kwenda kanisa katoriki saint peter. kwa bahati nzuri taa zilikuwa kijani.

Nilipita hapo kwa mwendo wa kawaida Kama ni dereva utanielewa tu.

Tulipofika mataa ya njia panda ya kwenda Kinondoni palikuwa na askari wa usalama barabarani yeye alikuwa akiyaongoza magari yaliyokuwa yanatoka upande wetu na upande wa mjini.

Hapo spidi ilikuwa ya wastani hivi kwa sababu magari yalikuwa karibu karibu.

Unajua macho yanapenda kuangali bahari

Eneo hilo upande wa mkono wa kushoto ni bahari .

Basi upande wa kushoto ukishapita taa za kuongoza magari kabla ya daraja la salender bridge kuna ujenzi unaendelea katikati ya bahari.

Unajua serekali ya awamu hii wanafanya kazi kweli kweli.

Mungu awape nguvu ya kutoangalia nyuma Ili wasonge mbele kuendeleza maendeleo nchi yetu yawe ya kimataifa na mfano kwa wengine.

Kuna kazi inaendelea ya ujenzi wa daraja kubwa la kisasa linalokatiza baharini lenye urefu wa kutosha linaloigharimu serekari mabilioni ya pesa.

Ni changamoto ya maendeleo katika karne hizi za sayansi na kiteknolojia kama zawadi kwa watanzania kwani daraja la kwanza lilijengwa mwaka 1929 na  kutumika kwa takribani miaka 51.

Ndipo mwaka 1980 serekali wakajenga daraja la pili lenye heshima yake kwa wakati huo.

Mnamo mwaka 2014 waziri wa ujenzi wakati huo Mweshimiwa Mgufuli alitangaza serekali inategemea kujenga daraja kubwa la kisasa maeneo ya salander bridge

Umeonaaa pale penye maendeleo ya kweli lazima utajikuta unatoa maelezo yasio na mwisho.

Mara kushtuka mataa ya salander bridges.
Kushangaa kote ningepitiwa na kunyosha kwenda katikati ya jiji.

Hapo tulisimama kwa dakika chache kwa sababu aliyekuwa akiongoza nagari ni askari wa usalama barabarani.

Ikanibidi nikae upande wa kulia barabara ya Alli Hassani mwinyi ili niweze kuingia barabara united nation.

Dakika chache tukawa  tumeingia Barbara ya umoja wa mataifa.

Njia ilikuwa nzuri kwangu , najua unasema kwanini.

Gari ya kwanza ilikuwa ya kwangu kwa hiyo nilikanyaga mafuta ili niwe wa kwanza kufika taa za fire zimamoto..

Katika taa zimamoto njia panda kushoto unaenda katikati ya jiji, kulia unaenda Magomeni.

Kwa wakati huo taa zikawa kijani hapo utata usipokuwa mjanja utabaki katikati.

Kwani taa za hapo zipo ruksa kwa wote .

Tukapita wote.

Mimi ikabidi niende mpaka maeneo ya kariakoo upandwe wa shule ya uhuru ili niweze kupata parking ya uwakika.

Nilipata sehemu ya kupaki Gari ambopo uwa napaki kila niendapo Kariakoo.

Kama nilivyokupasha hapo nyuma nia yangu ya kuja huku ni kutafuta vitabu vya watoto.

Hiyo siku ilikuwa ni siku yangu ya kutembea nilitembea kupita kiasi.

Hapa nawasubiria google watoe timeline yangu ya mwezi wa tisa ili nione mzunguko wangu ulikuwaje.

Wakati Natoka Kariakoo sokoni kuelekea mzunguko wa msmbazi.

Nikiwa maeneo ya jengo DDC karikooo gafla kwa mbele mama mmoja aliyekuwa amembeba mtoto mdogo alianguka huku mtoto akiwa mikononi mwake.

Alipokuwa anatembea hapo bahati mbaya akalanyaga banda la ndizi na kuteleza akaanguka chini.

huyo mama alikuwa amefuatana na watoto wake wa kiume wawili si wakubwa sana Ila ni Kati ya miaka kumi na mwingine nane hivi.

Yule kijana mkubwa akakimbilia mama Yake na kumbeba yule mtoto mdogo ambaye wakati uo alikuwa akilia kwa sauti kubwa.

Watu waliokuwapo eneo hilo hakuna hata mmoja aliyejaribu kumpa msaada yule mama kwa muda wote.

Mungu akanipa nguvu nilikimbilia pale na kupata nguvu ya kuwasogeza watu waliomzunguka yule mama wakimshangaa bila kutoa msaada wowote.

Huwezi amini yule mama alikuwa hawezi tembea ananyonga mguu kwa maumivu makali na kulia kama mtoto mdogo.

Mungu akanimbia wewe ni mwanajeshi kwa wakati huu onesha nguvu yangu kupitua kwako.

Basi niliinama na kumuambia yule mama nipo hapa kwa ajili yako sima nikumbatie mimi begani ili nikupeleke pembeni kwani hapo upo njiani na watu ni wengi watakukanyaga.

Mungu ni wa ajabu nilipata nguvu nikamtoa yule mama pale njiani na kumuweka pembeni ya jengo la DDC karibu na duka moja lililokuwa wazi.

Nikamuliza yule mama nini tufanye au tumpeleke hospital.

Kabla ya ajato jibu swali lingine kwa yule mama
Unaishi wapi hapa Dad es salaam.

Yule mama akajibu mtoni kijichi

Daa ni mbali toka hapa tulipo Kariakoo.

Bila kupoteza muda pembeni yetu wapo madereva wa tax...

Nikamfuata mmojo wa wale madereva

Nilipomueleza kuna mgonjwa anaitaji msaada kupelekwa hospital iliyo karibu na anapokaa mtoni.

Yule dereva akaondoka bila jibu , alipokuwa akiondoka akaenda kuongea na mwenzake .

Naye alipokuja akaja na vikwazo vya kumwacha njiani kwani hiyo ni kesi.

Akili yangu ikakumbuka bajaji ndipo nilipouliza zipo wapi! walio karibu yangu wakainua kichwa kuangalia upande wa pili wa barabara ya msimbazi.

Ndipo nilipoanza kukimbia kuelekea sehemu  bajaj zilipopaki.               

Nilipofika hapo nikaanza kupatana bei ya kutoka kariakoo mpaka mtoni kijichi.

Ndipo dereva wa bajaji akakubali kwa elfu kumi na tano.

Nakumbuka nilimuambia nifuate huku.

Mimi nikatoka mbio kuelekea kwa mgonjwa wetu

Bajaj ilipfika nikamuomba mama mmoja aliyekuwepo katika eneo hilo kumnyanyua ili tupeleke katika bajaji.

Kawaida msimbazi eneo la DDC uwa na watu wengi kwa nyakati za mchana tens siku za jumamosi.

Ilibidi nipangue njia kwa sauti kubwa Sogea sogea kama mimi mwanajeshi sauti yangu ilisikika kaa pembeni pisha pisha  sogea wewe vipi kaa pembeni.

Na mungu ni mwenye nguvu watu wanasogea bila ubishi mpaka na wengine mpaka wajeuke nyuma wakimuoa yule mgonjwa wanapisha pembeni

Yule mama kwa mbali niliskia akisema asante Sana Mungu atakubaliki

Basi vitabu venyewe sikuvipata Ikabaki kurudi nyumbani.

Kama una maoni yoyote

kimarokenny@gmail.com au

+255769922003

Mwisho.

Kennedy Kimaro

Tuesday, July 9, 2019

VIFO VILIVYOTOKEA KWA WANA HABARI WA AZAM MEDIA

Sipati picha kwa majonzi yaliyomo ndani ya moyo wangu kutokana na ajali, iliyosababisha vifo vya watu saba miongoni mwao wafanyakazi watano wa Azam Media.

Najaribu kuvuta picha kwa vijana mafundi wachapakazi hodari jinsi ndoto zao na mipango yao katika taasisi ya habari chini ya movuli Azam Media Group.

Maisha ni sawa na universe ilivyo na umbo kubwa  na umbali husiogawanyika na namba yeyote.

Unaanza mipango yako vizuri bila woga lakini huwezi tazama mbele kuna nini.

Nikijaribu Najaribu kuinua macho yangu juu na kupeleka fikra zangu za ujana kwa vijana wenzangu Azam Media.

Basi nabaki katikati ya fikra na kunyamaza kimya huku simanzi za machozi zikinijia kwa mbali.

Maswali mengi yamejikita katika fikra za ubongo wangu kutokana na tukio hilo la ajali.

Mawazo mengi yanakuja mbele yangu, lakini sipati picha katika fikra zangu, nini kilichotokea na kupelekea kubaki kimya.

Sisi ni binadamu na yale yote yaliyotokea  tunayaona sisi tuliobaki  hapa duniani.

Lakini vijana hawa.

1. Salim J Mhando
2. Silvanus W Kassong
3. Charles Wandwi
4. Florence B Ndibalema
5. Said H Hassan

Tuwawashia mishumaa ya maombolezi kwa wote watano

Safari yao ya hapa duniani ndio imefika mwisho.

Majonzi na maumivu ya simanzi zinabaki kwetu tulio hapa duniani.

Nashindwa kuendelea kuandika chochote zaidi ya kuwaombea wale wote waliofariki.

Nanyamaza kimya na kuangalia dunia inavyo songa mbele kwa spidi.

Na
Kennedy Kimaro.

Wednesday, June 26, 2019

MTAZAMO WANGU KAMA MKAZI WA EAST AFRIKA.

Watu wenye tabia za ubaguzi na umimi kama hawa ni hatari sana. 

Dunia imekuwa kama kijiji katika karne hii kutokana na ushirikiano wa  kisayansi na teknolojia.

Inapelekea watu kuingia kona zote za dunia ili wawekeze na kutafuta kazi za kufanya kupata kipato na kuongeza kasi ya maendeleo na uchumi kupata nguvu ya  kusonga mbele.

Hapo inapelekea binadamu kujichanganya katika jamii mbali mbali na kusababisha wakenya kuweza kuchumbia au  kuoa mtanzania au mganda, vivyo hivyo kwa waganda na watanzania na dunia nzima.

Tena sio east Afrika tu, watu wanaoana toka sehenu mbalimbali hapa duniani mifano middle east, Europe, Asia, Russia, America

Ukianza kuwabagua wengine na kujifanya nyie ndie mwenye Fulsa ya  kustahili kupata kitu au haki fulani, hiyo tabia ni hatari sana katika kizazi hiki cha sayansi na teknolojia.

Chuki za namna hii ni sawa kupanda mizizi ya magugu maji katika maisha ya binadamu.

Ukiwa na tabia ya chuki na ubaguzi kama hii ni hatari sana, haiwezi ishia hapo. itaendelea kwa vizazi na vizazi.

Baadaye uacha picha yenye mfano mbaya kwa watoto wetu.

Tabia kama hizi zikijitokeza lazima zikemewe mara moja.

Tabia kama hizi zinajenga uchochezi utaokufanya  kesho kuanza kuwabagua hata ndugu unawaona sio wa karibu yako..

Siasa za namna ni hatari  sana katika jamii zetu na kizazi cha vijana wa sasa.

Tumpe sifa Nyerere kwa kutuepusha na mambo kama hayo.

Sisi wabongo hapa kazi tu.. njoo na fedha zako.

Wekeza kwetu ili uongeze ajila kwa watanzania.

Tunajikita katika sera za kuongeza viwanda katika nchi yetu bila ubaguzi kwa raia yeyote kutoka mahali popote.

Kinachotakiwa uje na sifa za kuwekeza ili uchumi wetu upande juu.

Hiyo ndio Tanzania ya sasa yenye picha ya maendeleo kwa wote.       😄🥺👆

Wako @Kimaro.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu