Friday, November 20, 2015

Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu

1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.

2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?Ushuhuda kuhusu Mwana wa Mungu

6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.

7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.

8 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

9 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

Thursday, November 19, 2015

Akawaita mkutanoni pamoja na wanafunzi wake, akawaambia

31 Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.

32 Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. 33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

34 Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.

Tuesday, November 17, 2015

Joab Ndugai achaguliwa kuwa spika wa Bunge la 11

Saturday, November 14, 2015

Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu.

1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.

3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;

4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.

5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.

7 Wapeni wote haki zao mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.Upendo

8 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.

Atendaye dhambi ni wa ibilisi. Kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.

8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.Pendaneni Ninyi kwa Ninyi

11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi;

Magaidi washabulia Paris Ufaransa

Magaidi wameishambulia Paris na watu kadhaa wamuwawa.
Milipuko imetokea katikati ya paris sehemu tatu tofauti.
Polisi wamesema takribani watu 26 wameuwawa.
Habari zaidi angalia France 24 ipo live na channel nyingine za kimataifa.

Polisi - Takribani watu 40 wamekufa katika shambulizi hilo.

Rais wa Ufaransa Hollande ametangaza hali ya Hatari.na mipaka yote kufungwa.

Na wengine wemetekwa ndani ukumbi Bataclan Concert hall

Mipaka yote ya France imefungwa na raia wote wametakiwa kuwa wamoja katika matatizo yanayotokea sasa.


Friday, November 13, 2015

President forms team to advise on anti corruption war

President forms team to advise on anti corruption war

Thursday, November 12, 2015

UNIFANYE KUSIKIA FADHILI ZAKO ASUBUHI.

8 Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi,Kwa maana nimekutumaini Wewe.Unijulishe njia nitakayoiendea,Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.

9 Ee BWANA, uniponye na adui zangu;Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,Kwa maana ndiwe Mungu wangu;Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,

Wednesday, November 11, 2015

Nathi Nhleko is addressing the Media: 11 November 2015

Rosetta Philae landing: one year

Makala ya siku tano za kwanza kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli Ikulu

Tuesday, November 10, 2015

Uganda's President Museveni begins campaigning

Monday, November 9, 2015

Africa 54

Trick-or-Treat with the President and First Lady

The President Meets with the Prime Minister of Israel

Kampeni ya Okoa Kenya

Friday, November 6, 2015

Swipe | Back To The Future And Tiny A.I. Cars

Thursday, November 5, 2015

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE

Wednesday, November 4, 2015

The 700 Club - November 4, 2015

ISS: 15 years orbiting the Earth - BBC News

Earth from Space: Special Edition

HUYU NDIO MAGUFULI 1

Tuesday, November 3, 2015

The air crash in the Sinai Peninsula

The current weather situation: John Sterley

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu