Wednesday, June 6, 2018

SAFARI YA MAPACHA MARIA NA CONSOLATA 1996 MPAKA 2018

JAMANI MAISHA NI HADITHI YENYE STORI INAYOANZA BILA WEWE KUJUA NA INAISHA BILA WEWE KUJUA.

KWANZA JIULIZE WEWE UPO UPANDE GANI WA HADITHI HII KATIKA MAISHA YAKO KILA SIKU.

PILI JIULIZE KUNA USHAWISHI WOWOTE ULIFANYIKA ILI UZALIWE KATIKA FAMILIA ULIYOPO SASA.

JIBU LITAKUWA HAPANA ILA MUNGU NDIYE ANAYEPANGA YOTE YAFANYIKE.

MUNGU ALI MUUMBA MTU AKASEMA NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU. KWA SURA YETU.
WAKATAWALE SAMAKI WA BAHARINI NA NDEGE WA ANGANI NA WANYAMA NA NCHI YOTE PIA.

HAPO NDIPO HADITHI NZURI YA MAISHA ILIPOANZA NA KUSABABISHA KIZAZI KU- TAWANYIKA DUNIANI KOTE.

HAPO MAISHA YAKAANZA NA KUKAWA NA WATU WENYE MUONEKANO TOFAUTI KUTOKA NA MAENEO WALIYOKUWA.

MAISHA YAKAWA YAPO YAKASABABISHA WATU KUWEPO KWA WAKATI NA YENYEWE YANAENDELEA TU DUNIANI.

MIMI NIPO NA NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA NAFASI MPAKA SASA.

UNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUKUPA NAFASI YA KUENDELEA KUWEPO MPAKA SASA.

SASA TUTAZAME NINI KILICHONISABABISHA  KUYAANDIKA HAYA MACHACHE KWAKO.

MNAMO MWAKA 1996 MAMA MMOJA TOKA  MKOANI IRINGA WILAYA YA MAKETE ALIBEBA MIMBA KWA MIEZI TISA KAMA KAWAIDA YA WANAWAKE.

ILIPOFIKA MUDA WA KUJIFUNGUA KAMA WAZAZI WENGINE.
NDIPO  ALIKWENDA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IKONDA MKOANI IRINGA ILI KUPATA HUDUMA ZA UZAZI..

ALIJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WAWILI WALIOUNGANA MWILI.

HADITHI YA WATOTO WAWILI WALIOUNGANA ILICHOMOKA HAPO NA WATOTO KUPEWA MAJINA YA MARIA NA CONSOLATA MNANO MWAKA 1996.

KANISA LILIWACHUKUA MARA MOJA MARIA NA CONSOLATA WAKAWA CHINI YA SHIRIKA LA KIKRISTO.

CHA KUPENDEZA KWA AKINA MARIA NA CONSOLATA WALIJIONA WAPO SAWA NA WATU WENGINE.

MAISHA YAO YA KUKUBALI MATOKEO ULEMAVU WAO MOYONI NDIO  UWEZO NAFSI YA IMANI  WALIYOPEWA NA MWEYEZI MUNGU.

MSIMAMO WA KUENDELEA NA MICHAKATO KUENDELEA  KUJIKITA KATIKA VITU VYA KIDUNIA.
IJAPOKUWA WAO NI WALEMAVU NI FUNDISHO KWETU LISILOKUWA NA MFANO.

MUNGU ALIWAPA MARIA NA CONSOLATA HEKIMA NA UWEZO WA KUWA WALIMU NA KUTUACHIA MFANO KWETU KUTOKANA NA MATENDO YAO.

INGAWA LEO HAWAPO TENA DUNIANI LAKINI BADO TUTAWAKUMBUKA.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA
WAPUMZIKA KWA AMANI.

KENNEDY MARO

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu