Wednesday, June 6, 2018

SAFARI YA MAPACHA MARIA NA CONSOLATA 1996 MPAKA 2018

JAMANI MAISHA NI HADITHI YENYE STORI INAYOANZA BILA WEWE KUJUA NA INAISHA BILA WEWE KUJUA.

KWANZA JIULIZE WEWE UPO UPANDE GANI WA HADITHI HII KATIKA MAISHA YAKO KILA SIKU.

PILI JIULIZE KUNA USHAWISHI WOWOTE ULIFANYIKA ILI UZALIWE KATIKA FAMILIA ULIYOPO SASA.

JIBU LITAKUWA HAPANA ILA MUNGU NDIYE ANAYEPANGA YOTE YAFANYIKE.

MUNGU ALI MUUMBA MTU AKASEMA NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU. KWA SURA YETU.
WAKATAWALE SAMAKI WA BAHARINI NA NDEGE WA ANGANI NA WANYAMA NA NCHI YOTE PIA.

HAPO NDIPO HADITHI NZURI YA MAISHA ILIPOANZA NA KUSABABISHA KIZAZI KU- TAWANYIKA DUNIANI KOTE.

HAPO MAISHA YAKAANZA NA KUKAWA NA WATU WENYE MUONEKANO TOFAUTI KUTOKA NA MAENEO WALIYOKUWA.

MAISHA YAKAWA YAPO YAKASABABISHA WATU KUWEPO KWA WAKATI NA YENYEWE YANAENDELEA TU DUNIANI.

MIMI NIPO NA NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA NAFASI MPAKA SASA.

UNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUKUPA NAFASI YA KUENDELEA KUWEPO MPAKA SASA.

SASA TUTAZAME NINI KILICHONISABABISHA  KUYAANDIKA HAYA MACHACHE KWAKO.

MNAMO MWAKA 1996 MAMA MMOJA TOKA  MKOANI IRINGA WILAYA YA MAKETE ALIBEBA MIMBA KWA MIEZI TISA KAMA KAWAIDA YA WANAWAKE.

ILIPOFIKA MUDA WA KUJIFUNGUA KAMA WAZAZI WENGINE.
NDIPO  ALIKWENDA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IKONDA MKOANI IRINGA ILI KUPATA HUDUMA ZA UZAZI..

ALIJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WAWILI WALIOUNGANA MWILI.

HADITHI YA WATOTO WAWILI WALIOUNGANA ILICHOMOKA HAPO NA WATOTO KUPEWA MAJINA YA MARIA NA CONSOLATA MNANO MWAKA 1996.

KANISA LILIWACHUKUA MARA MOJA MARIA NA CONSOLATA WAKAWA CHINI YA SHIRIKA LA KIKRISTO.

CHA KUPENDEZA KWA AKINA MARIA NA CONSOLATA WALIJIONA WAPO SAWA NA WATU WENGINE.

MAISHA YAO YA KUKUBALI MATOKEO ULEMAVU WAO MOYONI NDIO  UWEZO NAFSI YA IMANI  WALIYOPEWA NA MWEYEZI MUNGU.

MSIMAMO WA KUENDELEA NA MICHAKATO KUENDELEA  KUJIKITA KATIKA VITU VYA KIDUNIA.
IJAPOKUWA WAO NI WALEMAVU NI FUNDISHO KWETU LISILOKUWA NA MFANO.

MUNGU ALIWAPA MARIA NA CONSOLATA HEKIMA NA UWEZO WA KUWA WALIMU NA KUTUACHIA MFANO KWETU KUTOKANA NA MATENDO YAO.

INGAWA LEO HAWAPO TENA DUNIANI LAKINI BADO TUTAWAKUMBUKA.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA
WAPUMZIKA KWA AMANI.

KENNEDY MARO

Sunday, May 27, 2018

Mafunzo ya imani kwa binadamu kwa kuubiri ukweli.

Mara nyingi napenda kusikiliza maubiri ya neno la Mungu toka kwa wachungaji tofauti hapa duniani.



Lakini napenda mchungaji anayetumia maandiko ya biblia kama nguzo yake ya kuubiri amani.



Mungu ambariki na kuwaonyesha njia watumishi wake walio wengi kulisambaza nene lake. 



Ndio maana roho mtakatifu aligawa nguvu za lugha tofauti ili neno lisambae duniani kote.



Kazi ya kulisambaza neno la Mungu pande zote duniani ni kazi ya kila mmoja wetu.



Kuna kitu kimoja ambacho kinanionya kutojaji imani ya dini ya binadamu mwingine yeyote, kwa sababu yeye au mimi tuna utashi wa kuwa upande wa imani wowote bila kulazimishwa na mtu yeyote.



Imani ni njia ya binadamu kujenga mahusiano kati yake na Mungu.



Imani ndio njia yenye nafasi ya matumaini kwa kila mtu kufanya mahamuzi ya kujijenga katika mahusiano yenye ushawishi wa nafsi yake na Mungu.



Tulipewa nafsi yenye imani ili kulitangaza neno lake Mungu kutoka katika masoma au mafundisho yaliyopo katika vitabu vitakatifu katika biblia.



Vitabu vitakatifu vinavyotumika kufundisha yale yaliyo na hekima ili kutufungulia upendo wa kweli toka kwa Yesu kristo.



Upendo wa mafundisho ya Yesu kristo ni njia yenye mafunzo yake kwa upeo na busara na amani.



Yesu alikuja na kutufundisha yale yaliyo mema ili kutufungulia njia ya faraja katika safari ngumu hapa duniani.



Mafundisho yake yote yalikemea mabaya na kukataa kurudia maneno mabaya.



Mungu alikemea matendo mabaya kwa kutufundisha kutenda yaliyo mema.



Mfano kitabu cha waamuzi mlango wa 13 kinatufundisha hivi...



MLANGO 13



1 Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini. 



2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto. 



3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. 



4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; 



5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti. 



6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala hakuniambia jina lake; 



7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake. 



8 Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa. 



9 Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye. 



10 Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile. 



11 Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi. 



12 Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? 



13 Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari. 



14 Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. 



15 Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako. 



16 Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana. 



17 Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza? 



18 Huyo malaika wa Bwana akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu? 



19 Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia. 



20 Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi. 



21 Lakini malaika wa Bwana hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa Bwana. 
22 Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemwona Mungu. 



23 Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu. 



24 Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni

Friday, April 6, 2018

IMANI ILIYO NA UPENDO

UPENDO UNAOTOKA KWA MTU NI TABIA YA NAFASI KATIKATI MOYO WAKE.
UPENDO SIYO KITU CHA KULAZIMISHA. UPENDO NI  IMANI ILIYO YA KWELI KATI YAKO NA MUNGU.

Sunday, February 18, 2018

Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

MLANGO 20

1 Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu

3 Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; 

4 na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
 
5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. 

6 Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? 

7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu
 
8 Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. 

9 Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari

10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari

11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba, 

12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

13 Naye akamjibu mmoja wao,
akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari

14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 

15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho

Saturday, February 17, 2018

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu