Wednesday, June 26, 2019

MTAZAMO WANGU KAMA MKAZI WA EAST AFRIKA.

Watu wenye tabia za ubaguzi na umimi kama hawa ni hatari sana. 

Dunia imekuwa kama kijiji katika karne hii kutokana na ushirikiano wa  kisayansi na teknolojia.

Inapelekea watu kuingia kona zote za dunia ili wawekeze na kutafuta kazi za kufanya kupata kipato na kuongeza kasi ya maendeleo na uchumi kupata nguvu ya  kusonga mbele.

Hapo inapelekea binadamu kujichanganya katika jamii mbali mbali na kusababisha wakenya kuweza kuchumbia au  kuoa mtanzania au mganda, vivyo hivyo kwa waganda na watanzania na dunia nzima.

Tena sio east Afrika tu, watu wanaoana toka sehenu mbalimbali hapa duniani mifano middle east, Europe, Asia, Russia, America

Ukianza kuwabagua wengine na kujifanya nyie ndie mwenye Fulsa ya  kustahili kupata kitu au haki fulani, hiyo tabia ni hatari sana katika kizazi hiki cha sayansi na teknolojia.

Chuki za namna hii ni sawa kupanda mizizi ya magugu maji katika maisha ya binadamu.

Ukiwa na tabia ya chuki na ubaguzi kama hii ni hatari sana, haiwezi ishia hapo. itaendelea kwa vizazi na vizazi.

Baadaye uacha picha yenye mfano mbaya kwa watoto wetu.

Tabia kama hizi zikijitokeza lazima zikemewe mara moja.

Tabia kama hizi zinajenga uchochezi utaokufanya  kesho kuanza kuwabagua hata ndugu unawaona sio wa karibu yako..

Siasa za namna ni hatari  sana katika jamii zetu na kizazi cha vijana wa sasa.

Tumpe sifa Nyerere kwa kutuepusha na mambo kama hayo.

Sisi wabongo hapa kazi tu.. njoo na fedha zako.

Wekeza kwetu ili uongeze ajila kwa watanzania.

Tunajikita katika sera za kuongeza viwanda katika nchi yetu bila ubaguzi kwa raia yeyote kutoka mahali popote.

Kinachotakiwa uje na sifa za kuwekeza ili uchumi wetu upande juu.

Hiyo ndio Tanzania ya sasa yenye picha ya maendeleo kwa wote.       😄🥺👆

Wako @Kimaro.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu