Monday, October 26, 2020

Elisha Elia. https://t.co/9q0JFLJ6Dv

#BURIANIELISHAELIA

Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho. Vita umevipiga, imani umeilinda, mwendo umeumaliza. 

Tutakuezi, tutakukumbuka kwa mengi yasiyopimika uliyotuachia Elisha Elia. https://t.co/9q0JFLJ6Dv

Thursday, April 2, 2020

TUNAMKUMBUKA ENGINEER MARINI MWANA HABARI WA TBC ARIDHIO.

NAKUMBUKA SAFARI YA MWANA HABARI KIJANA MARINI H MARINI ENGINEER.




SINA MENGI ILA NINA MACHACHE JUU YAKE NA UCHAPA KAZI WAKE.


KINACHONIFANYA NITETE KIDOGO JUU YAKE NI NGIVU YAKE YA KIJIJENGA YEYE MWENYEWE NA WENZAKE KWA UJUMLA.


NAKUMBUKA HENZI HIZO TVZ NA BAADAE TVT MPAKA TBC NA SASA TBC ARIDHIO.

KINACHONIFANYA NIWE KARIBU YAKE NI PALE ANAPOSIMAMA NA MSIMAMO WA MAENDELEO KWA UJUMLA KAMA MWANA HABARI MAKINI.

JARIBU KUMKUMBUKA MARINI PALE ANAPOKUWA KATIKA VIPINDI AU MATANGAZO YA KITAIFA YA MOJA KWA MOJA.
UWA MAKINI KUJENGA HOJA ZINAZOKUBALIKA KATIKA JAMII

KINGINE KILICHO MAWAZONI MWANGU NI VIPINDI VYAKE VYENYE KAULI MBIU ZA DODOMA.
ALIFANYA VIPINDI VINGI KUTOKA DODOMA NA KUTUGEUZA FIKRA KWAMBA DODOMA KAMA MAKAO MAKUU YA SEREKALI INAWEZEKANA.

KIKUBWA NI MAHOJIANO YAKE NA WABUNGE MOJA KWA MOJA TOKA DODOMA.
ALIWEZA VAA SURA YA SEREKALI YA SASA NI NINI INANATAKA JUU YA DODOMA NAYE AKAWA KIPAZA SAUTI CHA SEREKALI KWAMBA DODOMA KUNAFANYIKA MAENDELEO MUHIMU KAMA MAKAO MKUU YA TANZANZIA

SINA MENGI JUU YAKE ILA YANA JIELEZA YENYEWE PALE UNAPOMTAJA MARINI WA TBC ARIDHIO.
ILA NI MOJA NADHANI KAMA ENGINEER MARINI MARINI ANGEKUWEPO ANGELIFANYIA KAZI LITIMIE.

NALO NI TBC KUENDELEZA MUUNGANO NA TVZ.
MUDA WA HABARI LAZIMA WAJIUNGE LIVE NA TVZ KWA DAKIKA TANO KUPATA YANAYOJIRI ZANZIBAR

PIA PALE INAPOPATIKANA TBC ARIDHIO NA TVZ LAZIMA IWEPO 

MFANO KATIKA MASAFA YA SATELLITE UNAPO IPATA TBC ARIDHIO NA TVZ LAZIMA IPATIKANE HAPO HAPO.

HAPO TUTA MUENZI ENGINEER MARINI KWA KUMBUKUBU YENYE HESHIMA KWAKE

MUNGU AFANYE YOTE YALIO MEMA JUU YAKE 
WAKO
KIMARO

Monday, March 23, 2020

Maombi yetu katika janga hili la Coronavirus (COVID-19)

Binadamu tupo njia panda na janga hili la coronavirus hapa duniani.

Imani yangu inaniambia niwe na nafasi ya ya subira kwani tupo katika kipindi cha mapito ya maumivu hapa duniani.

Najaribu kuvuta mawazo kile kinachoendelea kutokea katika nchi zilizo juu kiuchumi hapa duniani.

Angalia ugonjwa huu wa homa ya mafua ya Coronavirus unavyoangamiza watu hapa duniani.

Sisemi watu wanakufa bali sina la kusema ila nabaki nikiangalia jinsi ili janga la ugonjwa wa mafua ya Coronavirus (COVID-19) yanavyosambaa sehemu moja kwenda nyingine hapa duniani.

Tunaonekana wanyonge katika fikra zetu huku tukisimama pamoja kutafuta njia ya kutokomeza mafua ya corona hapa duniani.

 Angalia Coronavirus (COVID-19)  inavyo safiri nchi moja kwenda nyingine kwa spidi kubwa yenye kutufanya kuwa na uoga kutokana na watu wengi kupoteza maisha na uchumi kuyumba hapa duniani

Tena nchi zilizo mbele kiteknolojia na uchumu mkubwa ndizo zilizo na wagonjwa wengi wa.  Coronavirus (COVID-19) hapa duniani.

Sina cha kusema na nanyamaza kimya huku nikizidisha maombi yangu kwa Yesu kristo ili afikishe maombi yetu kwa Baba mwenyezi Mungu kusikia vilio vyetu hapa duniani.

Maisha yetu yapo katika kuangaika na janga la Coronavirus (COVID-19)  lililo mbele yetu kama fumbo lenye kusubiri jibu lake hapa duniani.

Kila kitu kina sababu yake kutokea nasi tunamuomba mwenyezi Mungu atuzawadie uwezo wa kutambua tupo wapi na tuelekee wapi kupambana na janga la Coronavirus (COVID-19)  hapa duniani.

Amini ni yeye aliyetufanya sisi binadamu tuwe na ubongo wenye akili ya kufundishika tofauti na viumbe vingine hapa diniani

Basi sisi sote kwa umoja wetu tuongeze maombi yetu kwake ili janga la Coronavirus (COVID-19)  lipate kumalizwa na kupata kinga yake hapa duniani.

Wako
Kimaro





Wednesday, March 11, 2020

CORONA IMETANGAZWA KUWA JANGA DUNIANI

CORONA NI IANGA LINGINE DUNIANI

Ebu tumuombe Baba Mwenyezi Mungu atusaidie kwa hili janga

Tuanze sasa kimya kidogo wapendwa..

Baba mwenyezi Mungu mwenye uwezo na nguvu kuliko yeyote..

Tunakuomba utusamehe yale yote tuliyoyafanya kwa kutokupendeza wewe...

Baba tusamehe na utupe nguvu ya kupambana na janga hili la corona linalotaka kuiangamiza duniani yote.

Baba kemea na uangamize corona kwa sauti ya neno moja tu, ili binadamu tujikinge na kusonge mbele na maisha yenye imani juu yako 

Baba wape nguvu wanasayansi duniani kote ili wagundue kinga na dawa ya kuipoteza corona kusambaa duniani.

Baba wewe unajua nini kilichotokea mpaka corona kufika hapo.

Basi sisi wanao tunakuomba ili  utuonyeshe matumaini kwetu. Tuweze kupambana na janga hili la corona ili dunia iendelee kama ulivyopanga.

Amina.

By 

Kimaro


  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu