Tuesday, June 23, 2009

Post toka kwa Michuzi,Mabishano ni kutokana na blogger kusema twitter ni mpya

libeneke la twitter
kuna hili libeneke jipya la twitter ambapo ukijunga unakuwa umejitengenezea kaglobu kako ka mawasiliano ya papo kwa papo na wadau wengine. mie tayari memba na nawakaribisha wadau mjiunge. ni libeneke la kisasa na watu mashuhuri kama vile obama wamo.
nenda
kisha fuata maelekezo. ni simpo kichizi
© Michuzi Monday, June 22, 2009 Permalink Mtumie Rafiki Yako


Maoni: 12


  • Tarehe June 22, 2009 1:18 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    sasa michuzi kwa kuwa umejiunga basi ungeweka link watu tuweze kuku follow.

    please you can follow my updates too, kupitia http://www.twitter.com/reedzsolution

    karibuni katika twitter updates.

  • Tarehe June 22, 2009 1:34 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    hili kweli libeneke jipya,nimechungulia nimewaona pia ffu!? nao wamo! itabidi nami nijiunge leo.asante sana Misupu mzee wa libeneke

  • Tarehe June 22, 2009 2:42 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    ur late!ndo leo waijua twitter,,

  • Tarehe June 22, 2009 2:57 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Twitter is not for everybody...soma ijue kwanza kabla haujajiunga

  • Tarehe June 22, 2009 3:27 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    kwani reference adi iwe obama???

    so what that twita twita sijui

    aaagh

  • Tarehe June 22, 2009 3:31 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    mbona umechelewa mzee?
    tutembelee na sisi basi!

  • Tarehe June 22, 2009 5:52 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    HATA OBAMA YUPO.....so what? Grow up!

  • Tarehe June 22, 2009 6:07 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    YAANI TWITTER HUKU IMESHAKUWA NI KITU YA ZAMANI HADI MTOTO WA PRIMARY ANAYO SASA HUKO NDO MNATANGAZIANA LEO, NDO DAR TAMBARARE HIVYO?

  • Tarehe June 22, 2009 6:09 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    huku kila mtru anayo, yoyote yule unayemjuwa wewe hapa duniani mtu maarafu anayo na unaweza kuchat nao kuamzia akina MADONNA, BEYONCE HATA OBAMA

  • Tarehe June 22, 2009 7:02 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    nendeni zenu nyinyi mnaoshangaa, kwani ni vitu vingapi ambavyo viko huko na ni vya kawaida kabisa lakini huku bongo havijafika? acheni kujishaua na ushamba wa kuwa nchi za wageni na kudharau kwenu,..mkataa kwao ni mtumwa..mngeeleza tu umuhimu,uzuri au ubaya wa hicho kitu kwa kuwa nyie tayari mnacho na mnakifahamu..sio " ooh, mmechelewa, ndo mnajua leo, hicho kitu hata mtoto wa nursery huku anacho" OVYOOO!

  • Tarehe June 22, 2009 7:21 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    I second you mdau June 22, 2009 2:57 PM. Twitter sio kwa ajili ya kila mtu. Uzungu usitutawale sana, haya mapinduzi ya mtandao yasitupotezee muda wa kujituma makazini na katika shughuli za kila siku, mtaishia kuwa mafollowers tu, by the way who will be interested in knowing what r u doing now, yes you... tena wewe, ulieko mabonde poromoka...tuwaache wapambe wa kina tom cruise waangalie na kufatilia maisha ya macelebroty yao...? I've never come accross such a selfish idea in my life kama twittter...A simple sms wil do the job, mpaka niwashe pc nilog in, ndio nikuulize tena kwa 140 characters?? aah wapi, wadau endeleeni tu na mapinduzi yenu, bora niende library kuazima kitabu nikasoma nijiendeleze elimu yangu kuliko kuspend time kufatilia maisha ya kina so called "OBAMA", sijui blaah blah...
    Muda tunaotumia kwenye social networking ungetumika katika mambo ya maana ingekuwa ni jambo la mbolea sana...watu mpaka kazini wanaibia muda wanaolipwa kwa kutandawika na mablog sijui SN....Wazungu utamaduni wao umezungukwa na u-mimi, ndio maana social networking sites zinakuwa kwa kasi,na ni media power, inatengeneza upuuzi huu kwa watu, wakati wengine wanakuwa mabilionea, can u imagine mark zuckerberg- eti sasa hivi bilionea... na watu tunamtazama tu, na kupoteza muda kuspend time sehem ambayo muda wetu anauuza... Someni terms na condition za FB ndio mtaelewa nazungumza nini....Yes natumia FB kwa matumizi ya nadra sana, hasa kuwasiliana na nisioweza kuwapata kungine.. lakini kuna watu wanaupdate facebook ac zao kila saa, picha kede kede, hawajui kama fb wanauza sura zenu na info.. halaf mnashangaa spam emails zinapotoka... wazungu wanazipapatikia social networking sites kwasababu they r too selfish to interact...Maskani zimejaa kibao, vibaraza vipo tele, who will care kukaa mbele ya kioo kuulizana unafanya nini, wakati ukigeuka kushoto jirani kakusabahi, ukigeuka kulia unaona watoto wanacheza mdako, yaani africa yetu hii ni raha tupu kwa swala zima la kujichanganya, tunapendana, tunajaliana, tunasalimiana kila mahali (isipokuwa wachache wenye vijiba na maradhi ya roho)....Mizungu ni ndani tu na kazi... sana itaenda pub kulewa...
    #
    #
    Mdauz

  • Tarehe June 23, 2009 6:48 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Mdau hapo juu umenikosha sana. Naungana na wewe kabisa. Tanzanians tuamke,sio kuregister tu kwenye kila blog as if hakuna vitu vingine vya maana vya kufanya. FB,myspace,twitter etc. Ni kweli tunafaidika? Umeme wenyewe issue. Utakuta mtoto kapata hela ya nusu saa kwenye internet cafe anahangaika na FB badala ya kucheki mambo ya academics au walau hata world news. Mnatafuta wachumba?

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu