Friday, August 7, 2015

MAISHA YA KILA SIKU HAPA DUNIANI -SEHEMU YA 1

Nakumbuka mbali sana
Katika Dunia hii kuna tabia za aina tofauti.

Angalia maisha yetu ya kila siku, yapo ya kupendeza na ukiangalia upande wa pili ni chuki na dharau tu.

Mara nyingine tunajiuliza sisi tupo upande gàni katika maisha aya!

Dunia imeumbwa katika misingi ya imani katika maeneo tofauti.

Je binadamu tutasimama katika msingi upi?

Sisi binadamu asilimia kubwa tunasimama katika upendo ndani ya matendo yetu hapa Duniani.

Wewe ukichukia ukitutenga au ukitubagua na kutuweka katika kundi unaloliona wewe hatuna kinyongo na wewe ila tunakuombea kwa Mungu akupe ufahamu na mwanga wa kujitambua katika matendo ya kila siku.

Kila wakati nafikiria nini kinatokea katika maisha ya kizazi hiki cha sayansi na teknolojia.

Wengi wetu tunajiona sisi tunajua kuliko wengine.

Kumbe Mungu ameweka mipaka ya kutojua wazo la mtu mwingine mpaka aseme mwenyewe.

Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Mara nyingi tunawaona watu tofauti wakijiweka katika makundi tofauti
katika maisha.

Mfano wewe ukitaka kufanya kitu kinachofanana na wao ni tabu tupu.

Je kama imani zisingekuwepo ingekuwa vipi?

Leo watu wengine hawana thamani kwa wengine kwa sababubu wao ni wao na sisi ni sisi.

Tunatakiwa kujenga Dunia yenye upendo na si chuki.

Mungu aliyajua yote haya na ndio maana binadamu hatujui nini kitotokea, bali tunajua pale linapotokea na tendo kukamilika.

Leo wanasayansi wanafanya utafiti kujua muda ulianza vipi?
Leo Nasa imeweza kuweka chombo anga za juu chini ya obiti ya Dunia I S S
INTERNATION SPACE STATION.
Chombo ambacho wanaanga wanaishi ndani yake na kufanya tafiti mbali mbali za kisayansi..
Ni ushirikiano wa mataifa mbali mbali.

Na chombo kingine cha anga za juu toka Nasa kimeweze kufika katika sayari ya Pluto iliyo mbali zaidi.
Imechukua takribani miaka tisa mpaka kifike uko.

Hizo ndio kazi ya binadamu inayofanyika kisayansi na teknolojia.

By kennedytz.blogspot.com
       7-8-2015

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu