Sunday, October 18, 2015

Kwa kuwa nafurahia Wokovu Wako.

Naye Hana akaomba, akasema,Moyo wangu wamshangilia BWANA,Pembe yangu imetukuka katika BWANA,Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;

2 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;Kwa maana hakuna ye yote ila wewe,Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.

3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;Majivuno yasitoke vinywani mwenu;Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.

4 Pinde zao mashujaa zimevunjika,Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.

5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba,Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.

0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu