Tuesday, July 17, 2007

HUYU NDIYE ALIYETANGULIA AMINA NAKUMBUKA BAMBATAA YA MAMA NONINO


Namfahamu Mh. Amina Chifupa tangu akiwa mwanafunzi wa Makongo Sekondari na hasa alipoanza kutangaza na kituo maarufu cha redio cha Clouds. Lakini hasa nilimfahamu sana Mh. Amina Chifupa wakati nikisoma naye chuo cha uandishi wa Habari cha ROYAL ambacho sasa kinajulikana kama ROYAL COLLEGE OF TANZANIA ambapo tulikuwa darasa moja na mimi kuwa kiongozi wake.Kwa kifupi kabisa naweza kusema kwamba, kuingia bungeni kwa Mh.Amina Chifupa kuliendelea kunipa mwanga wa ni aina gani ya mtu Amina ameamua kuwa. Alionyesha ujasiri mkubwa katika umri mdogo na hasa alipolivalia njuga suala la Madawa ya kulevya.Hamasa kubwa alioionyesha kwa vijana sina shaka kwamba ametuachia mtihani mkubwa wa kumuenzi hasa katika mtiririko wa shughuli ambazo alikuwa amejipangia kuzitekeleza kwa niaba ya vijana kama muwakilishi jasiri, aliyedhamiria, mwenye moyo wa machungu ya dhati na asiye woga kujua hatima ya kinachomkera.Taifa la Tanzania limepoteza mrithi wa jamii, Vijana wamepoteza nguzo na chachu ya hamasa, Wazazi wamepoteza mlezi na mrithi lakini kubwa zaidi umma umepoteza mwelekeo na mtazamo sawia.Serikali yetu inayo kazi kubwa ya kumuenzi Mh. Amina Chifupa na pengine haitasaidia kumuenzi kwa kumuandika kwenye vitabu, kumjengea mnara na mambo kama hayo.......Serikali imuenzi amina katika vita aliyoianzisha dhidi ya udhalimu wa madawa ya kulevya ambacho ndicho chanzo cha kuwa na vijana mazezeta.....Mh. Amina alikereka sana na uharibifu usio huruma dhidi ya vijana. Nawapongeza radio Clouds ambayo Mh. Amina aliitumikia kabla ya majukumu ya kitaifa kwa kumuenzi kwa maombolezo kiofisi lakini huu uwe mwanzo tu, hakika akina Masoud Kipanya, Gadner Habash, Joseph Kusaga, Luge Mutahaba na timu nzima ya redio hiyo itafanya kitu kikubwa sana ambacho kitabakia kumbukumbu ya kudumu juu ya Amina Chifupa."Hakika Mwanadamu atakufa na hakika ikifika haipingiki" Hukumu ya kiini hasa cha kifo cha Mh. Amina tumuachie Mweny-enzi Mungu mwenye haki juu ya vyote vilivyomo.MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA AMINA CHIFUPA.


  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu