Saturday, August 4, 2007

Dumia Isiyo na Njaa

Maono yetu ni ulimwengu ambao hauna njaa na ukosefu wa lisha bora- ulimwengu ambamo kila mtu anaweza kuhakikishiwa kuwa atapata chakula anachohitaji ili awe na lishe bora na mwenye afya. Maono yetu ni ya ulimwengu ambao mbali na kumpa kila mtu maslahi na heshima yake kama mja, utavilinda vitu hivi. Huu ni ulimwengu ambapo watoto watakua, wajifunze na kunawiri, huku wakiishia kuwa watu katika jamii walio na afya nzuri, wenye kuitumikia na kuijali.
Ijapokuwa mafanikio katika kupunguza matatizo ya njaa ya lishe bora yameonekana ulimwenguni kote, bado tungali nyuma katika kufanikiwa kuwa na ulimwengu ambao watu wake hawana njaa. Tunaona elimu na taarifa za masuala yaliyofungamana na njaa ulimwenguni, usalama wa chakula na lishe bora kama masuala muhimu katika kufanya maono haya ya kilimwengu yafaulu. Kwa hali hii, tunazielekeza juhudi zetu kwa vijana na walimu wao. Je, endapo kila mwaka, kwenye siku kuu ya Chakula Ulimwengu (tarehe 16, Oktoba) watoto ulimwenguni kote watafahamishwa kwa pamoja vifaa vinavyofanana vya kufunzia kuhusu njaa na utapiamlo pamoja na yale yatakikanayo kufanywa, wataweza kukua wakitambua jinsi ulimwengu wetu unavyotegemea mambo mengine? Je, endapo watafundishwa masomo kutoka sehemu tofauti tofauti za ulimwengu,kutoka tamaduni na hali mbalimbali wakakuwa tayari kufanya kazi pamoja ili kutatua matatizo ya njaa na usalama wa chakula? Je, kunazo njia ambazo kwazo kizazi cha vijana chaweza kukuzwa ili wawe wananchi wanaotegemewa na walio wa kilimwengu?
Tunaamini kwamba majibu kwa maswali haya yote ni “NDIYO” kama walimu mpo katika hali nzuri ya kuweza kuwafanya vijana wawe ni watu wanaojali na wanaojitolea kijiunga katika vita dhidi ya njaa. Ubunifu, mawazo fikira, pamoja na maguvu ya vijana huwakilisha rasilmali muhimu ya kuendelea kukuza jumuiya na mataifa yao. Nyinyi, walimu wao, mwaweza kusaidia katika kuleta mageuzi kupitia kwa ujulishaji, kubadilishana maarifa, kuhimiza ushiriki, na kuwaonyesha vijana kuwa wanalo jukumu muhimu katika kufaulisha kuwepo kwa ulimwengu usio na njaa.
Tungependa kuwapa moyo kujiunga na walimu pamoja na wanafunzi ulimwenguni kote ili kujihusisha katika shughuli za Kulisha Akili, Kupambana na Njaa.

Njaa na Ukosefu wa Lishe Bora Duniani
Journée mondiale de l'alimentation
Washiriki katika du Projet Kulisha Akili, Kupambana na Njaa
Shukrani
Kudhamini
Wasiliana nasi
Pata faili la mtindo wa PDF

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu