Wednesday, May 28, 2008


Jhikoman afanya makamuzi ya Kufa mtu Finland

Mwanamziki wa Tanzania Jhikoman kutoka katika mji wa kihistoria Bagamoyo aka bwaga moyo! 25-05-2008 ameweza kukonga nyoyo za melfu ya washabiki,waliofurika katika

tamasha la Global Village mjini Helsinki,huko Finland,

Mwanamziki huyo wa Tanzania aliweza kuwatia kiwewe maelfu ya washabiki wa mziki katika onyesho hilo na kuipeperusha bendera ya Tanzania kisawa sawa katika njia ya mziki,Jhikoman ndiye aliyepata bahati ya kuweka katika bango la matangazo la onyesho hilo(kama inavyoonekana)Pichani, mwanamziki huyo amefanya onyesho hilo kuwa kivutio

cha maelfu ya watu.

Jhikoman anaendelea na ziara ya kikazi huko Finland na kuzidi kuipeperusha bendera ya Tanzania.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu