Monday, July 28, 2008

The Ngoma Africa Band kupelekana mchaka mchaka na maelfu ya washabiki Frankfurt


Bendi ya Mziki wa dansi The Ngoma Africa band aka The Golden Voice of East Africa!
Inatarajiwa kupanda jukwaani 9-08-2008 katika maonyesho makubwa ya African and Caribbean Cultural Festival yatakayo fanyika katika mji wa mapesa ya euro!
Frankfurt City,kwenye viwanja vya Robesotck Park,nchini Ujerumani.
Bendi hiyo mashuhuri kwa kuwapeleka puta na kuwadatisha akili maelfu ya washabiki
kwa mdundo wake ambao umetajawa kuwa ni "Extraordinary"bongo dansi kutoka
Uswahilini Tanzania,imejikuta inafunika katika maonyesho makubwa kwa kuwatia kiwewe
washabiki na mziki wao dansi wa bongo.
Wakati CD yao "Apache wacha Pombe"imefanikiwa kuhitangaza Tanzania kimziki katika
kiwango cha kimataifa,wakali wetu hawa Ngoma Africa band juzi juzi walistua ulimwengu
kwa kufyatua kali !nyimbo yao mpya iliyo beba Jina la "Baba wa Kambo" ambayo imemteua mwandishi wa habari Mhidini Issa Michuzi kuwa hakimu wa kuhamua Zogo
la Ngoma Africa na "Baba wa Kambo" kali hiyo mpya wamemkabidhi hakimu mteuzi hili
hatoe haki.
Ukiachia onyesho la Frankfurt,hapo tarehe 29-08-2008 Ngoma Africa watapanda jukwaani
katika onyesho lingine kubwa la AfriKa Festival litakalo fanyika katika viwanja vya Altona,katika mji wa Hamburg,Ujerumani,ambako maelfu ya wasabiki wanamsubiri Ras Makunja aka bw.Kichwa ngumu na kikosi chake machachari hili wapate ngoma za kiuhakika!
Siku ya 30-08-2008 Ngoma Africa wataendeleza LIBENEKE katika mji wa Krefeld ambako watatumbuiza katika onyesho lingeni kubwa la mziki na utamaduni wa mtu mweusi
the AFrika Fest-Krefeld,Mwanamziki mashuhuri Ebrahim Makunja aka Ras Ebby makunja"bwana Kichwa ngumu" alimaarufu MM mtunzi mchokozi! mzee wa kurusha madongo atakiongoza kikosi chake hiko chenye wanamziki machachari akiwemo yule
mchizi wa kuchalaza solo Christian Bakotessa aka Chris-B,pia bwana Said "Jazbo" Vuai,
Richard Mkutima,Maxme na wengi wengineo waliomo ndani ya tahasisi hiyo "the Ngoma Africa band" yenye tabia ya kuwatia kiwewe washabiki na kuporomosha mdundo wenye beat zinawatisha wanamziki wa bendi nyingine wanaoshiriki katika maonyesho!
Mara nyingine uporomosha nyimbo zenye maonyo,kushutumu,kufundisha au kuishauri jamii...penginepo nyimbo ambazo ndani yake kuna vijembe!!! na madongo(lawama) nzito
ambazo mara nyingi uzua mjadala,nyimbo ambazo zinawafanya kuonekana kuwa ni bendi
yenye majukumu makubwa ndani ya jamii.
Maporomota wa maonyesho mengi ya World Music wamehitaja bendi hiyo kuwa ni bora kwa kuwa mziki wake wa dansi wa Tanzania unakubalika na kuwatia kiwewe washabiki!
Lakini tu mara nyingi gharama za ulinzi ndizo nzito kutoka na wingi wa washabiki ,
Labda tuwatikie kila la heri Ras makunja na ndugu zake The Ngoma Africa Band na bongo dansi lao
Posted by Picasa

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu