Monday, May 18, 2009

Kigogo anayewaharibu wanafunzi ANASWA
DEREVA WA PIKIPIKI AUWAWA KINYAMA
BEN KOMBA Kutoka /Pwani/5/18/2009 12:25:36 PM

Mkazi wa Bagamoyo BW.PETER MWAKAMBAYA mwenye umri wa miaka 28 amekutwa ameuwawa na watu wasiojulikana, baada ya kukodishwa na mwanamama aliyevalia baibui katika maeneo ya Pera wilayani humo.
Marehemu MWAKAMBAYA ambaye alikuwa dereva wa pikipiki zinazokodishwa Mjini Chalinze, Alikodishwa siku ya Alhamisi jioni na mwanamama anayesemekana kuvalia baibui akimtaka ampeleke Pera kwa ajili ya kufuatilia mzigo wake wa Mirungi kutoka katika basi.
Mjomba wa marehemu ambaye hakupenda jina lake litajwe ameiambia RFA Mjini Kibaha, kuwa baada ya kumuua marehemu kwa kumnyonga na kumvunja miguu mara mbili maeneo ya ugokoni na pajani, hali kadhalika na mikono pamoja na kumpiga na kitu kizito maeneo ya kichwani na kumpora pikipiki.
Marehemu PETER MWAKAMBAYA alizikwa jana Mjini Chalinze na mazishi yake kuhudhuriwa na watu wengi walionekana kustushwa na mauaji hayo ya kikatili ambayo yametokea mara nne katika kipindi cha mwaka huu, hali ambayo inawatia hofu madereva wa pikipiki.
Naye mkuu wa wilaya ya Bagamoyo BW.MAGESSA MWILONGO, akizungumza wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Pwani uliofanyika katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo, amelaani mauaji hayo na kuyaita ya kinyama na hayawezi kuendelea kuvumiliwa.
BW.MWILONGO amesema atachukua hatua za makusudi akishirikiana na vyombo vya ulinzi wa usalama kuhakikisha hali hiyo inakoma mara moja ili kurudisha heshima ya utu wa mwanadamu.
Mwisho

0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu