Wednesday, December 7, 2016

NI MTAZAMO WANGU SI MTU MWINGINE YEYOTE

AMINI MAISHA YAKO NI LAZIMA YAWE NA SABABU YA KUSAIDIA JAMII HAPA DUNIANI.

UJACHELEWA AMKA SASA. JITAMBUE KWA NINI UPO HAPA DUNIANI.

NAFSI YAKO INAYO MCHANGO GANI KATIKA DUNIA HII

JENGA NAFSI YAKO KAMA ZAWADI ULIZOPEWA WEWE NA MUUMBA WA VYOTE.

FUNGUA MACHO YAKO SASA NA UTAMBUE NGUVU YA NAFSI YAKO NA SABABU YAKE.

TAZAMA MBELE NA UJITAMBUE WEWE NA WENGINE WENGI WALIOPO KATIKA DUNIA HII KWANINI HAWAFANANI NA WEWE.

FUNGUA MAWAZO KATIKA NAFSI YAKO NA UTAMBUE MALENGO YALIYO KATIKA MAWAZO YA NAFSI YAKO.

SIMAMA IMARA NA KUJIULIZA UNA MUDA GANI WA KUTIMIZA MALENGO YALIYO KATIKA MAWAZO YA NAFSI YAKO.

TENA TAZAMA MBELE NI WANGAPI WANATEGEMEA MAFANIKIO KUTOKANA NA UWEZO WA FIKRA ZILIZO KATIKA MAWAZO YA NAFSI YAKO.

Itaendelea
Umeonaa√
Kk

BASI JENGA MAMBO MEMA YENYE KUMTUKUZA MUNGU KWA KUFANYA YALIO MAZURI KWA JAMII YETU.

TIMIZA YALE YANAYOTOKA KATIKA NAFSI YAKO ILI JAMII IPENDEZWE NA KAZI ZA MIKONO YAKO

PINGA NA KEMEA MIPANGO YA SHETANI KWA KUCHELEWESHA SAFARI YA MAENDELEO YAKO

SIKU ZOTE TAZAMA MBELE NA SI NYUMA KWANI NYUMA NI KWA SHETANI NA MBELE NI KWA MUNGU.

KEMEA MACHUKIANO KATIKA JAMII JENGA UPENDO KATIKA MAISHA YAKO

KUMBUKA MUNGU NDIYE KILA KITU KATIKA NAFSI YAKO.

SIMAMA IMARA KAMA WEWE NA SI KAMA YULE KWANI NAFSI ZENU NI TOFAUTI KAMA ALAMA ZA VIDOLE VYENU.

USIMCHUKIE MWENZAKO KWANI YEYE NI CHACHU YA MAENDELEO YAKO.

KELELE ZAKE NDIO UFUNGUO WA  KUSONGA MBELE KATIKA MAISHA YAKO

MWACHIE MUNGU KWA KILA BAYA NA CHAFU LINALOTOKEA MBELE YAKO KWANI LINA SABABU YA KUTOKEA KWA WAKATI HUO.

JIFUNZE KUNYAMAZA KIMYA NA KUCHELEWA KUJIBU NENO LENYE UTATA KWANI SHETANI KAZI YAKE NI KUBOMOA KILA ZURI LINALOTOKEA HAPA DUNIANI.

Itaendelea
Umeonaa√
KK

TUNATAKIWA KUJENGA JAMII YENYE UPENDO WA KWELI KATIKA MZUNGUKO WA MAISHA YA KILA MWANA JAMII.

ILI KUENDELEZA YALE YOTE MAZURI YANAYOFANYWA NA BINADAMU HAPA DUNIANI.

MUNGU ALIKUPA NAFSI YAKO IWE YA KWAKO NA KWA MANUFAA YA WOTE WENYE UHAI HAPA DUNIANI.

BASI JIKUBALI MWENYEWE NA UTAZAME MBELE KWA NGUVU ILIYO JENGWA NA MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA VITU VYOTE HAPA DUNIANI

AMINI KATIKA MSAADA WAKE MUNGU NDIO NGUVU YETU YA PUMZI YENYE UHAI INATUFANYA TUISHI HAPA TULIPO LEO

Itaendelea
UMEONAA
Kk

MAISHA NI SAFARI YENYE VITUO VINGI TOFAUTI KWA KILA PUMZI INAYOTOKA KWAKO. TAMBUA KUNA WAKATI WA FURAHA NA WAKATI WA MAJONZI KWA KILA KUMBE CHENYE UHAI HAPA DUNIANI.

KAA CHINI FANYA TAFAKARI KWA MAPANA KATIKA NYAKATI ZOTE UNAZOPITIA KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU HAPA DUNIANI.

MUNGU NI MWEMA KUPITA KIASI. AMEKUPA MUDA WA KUANGAIKA NA MUDA WA KUPUMZIKA ILI UPANGE NA UPANGUE UNAYOPITIA KILA SIKU NDIO MAANA DUNIA INAJIZUNGUSHA YENYEWE KATIKA MUHIMILI WAKE NA INALIZUNGUKA JUA NA KUPATA MCHANA NA USIKU

HAPO BINAADAMU ANAPATA MASAA YA KUFANYA KAZI NA MUDA WA KUPUMZIKA ILI MAISHA YAENDELEE

IPE NAFSI YAKO NGUVU ILIYO PEWA NA MUUMBA KWA KUCHAMBUA MAZURI NA MABAYA. NARUDIA KUSEMA WAKATI MWINGINE CHELEWA KUTAMKA AU KUAMUA JAMBO ILI USIMAME IMARA KATIKA MAAMUZI YA NAFSI YAKO KILA SIKU.

KUMBUKA SAFARI YA MAISHA YAKO NI NDEFU KWA UPANDE MMOJA NA FUPI KWA UPANDE MWINGINE.

ITAENDELEA
UMEONAA
K KIMARO

TUPIA JICHO SAFARI YA MAISHA YAKO IMESIMAMA UPANDE GANI. TAZAMA WEWE KAMA WEWE UNAMSIMAMO GANI JUU YA MAENDELEO YAKO BINAFSI.

TUPIA FIKRA ZAKO KWA NDANI ZAIDI NA  MSIMAMO WAKO KWA JIRANI YAKO UNABEBA UPENDO AU CHUKI NA ZARAU KWA WENGINE.

TAZAMA UPENDO NA MATENDO YAKO JUU YA MSAMAHA KWA MTU ALIYEKUKOSEA BAADAE AK AKUOMBA MSAMAHA KWA TENDO ALILOKOSEA KWAKO UTAFANYA NINI JUU YAKE.

KUMBUKA MUNGU AMEMFANYA BINADAMU AWE NA NAFSI YA KIPEKEE KATIKA MAISHA YAKE YA KILA SIKU.

MFANO UNALOLIWAZA WEWE NI LAKO WEWE.
UNALOLIFANYA WEWE NI LAKO NA NINALOLIFANYA MIMI SASA NI WAZO LANGU MIMI MWENYEWE KENNEDY LEPATA KIMARO.
NA WEWE WAZO LAKO LITABAKI KUWA LAKO MPAKA UTAPOLISEMA KWA MWINGINE NDIO LINAKUWA WAZI.

TAZAMA FIKRA ZAKO JUU YA KUFUATILIA MAMBO YA WENGINE NA KUFANYA NDIO KAZI YAKO YA KILA SIKU.

KUMBUKA JENGA UWEZO WAKO KWA KUFANYA YA KWAKO NA KUYAENDELEZA  YAKO KUWA MFANO KWA WENGINE.

MARA NYINGI KIPIMO CHA KUSAMEHE HAPO HAPO NI NGUVU YA IMANI YA  UPENDO ILIYOJENGWA KATIKA NAFSI YA BINADAMU WALIOPO KATIKA DUNIA HII.

BINAADAMU WENGI TUNAPENDA KULAUMU KAMA KUNA MTU AMEKUKOSEA WAKATI IMANI INATUFANYA KUTENDA MSAMAHA WA KWELI KATI YA YETU.

NI KOSA KUCHUKUA UGOMVI  AU MAPUNGUFU YA MWINGINE NA KU YATAWANYA KWA WENGINE NA KUFANYA NDIO KAZI LA SIKU KUTANGAZA KWA MWENZAKO ILI ROHO YAKO IPATE SIFA ZA KIDUNIA.

KWA IMANI NINAYOAMINI MIMI KUNA ANDIKO LINA SEMA HIVI.

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba wenu wa mbnguni atawasamehe nyinyi.  Bali msipo wasamehe watu makosa yao, wala Baba hatawasamehe nyinyi makosa yenu.

KODOA MACHO YAKO KWA UMAKINI UONE JINSI NENO MSAMAHA LILIVYO NA NGUVU KATIKA VITABU VITAKATIFU.

ITAENDELEA
UMEONAA
KENNEDY KIMARO

HAPO UMEJIONEA JINSI GANI BINAADAMU ANASIMAMA KWA IMANI YENYE MAFUNDISHO TOSHA YA KUMTOA BINADAMU KATIKA TABIA TATA NA KUMPELEKA KATIKA TABIA NJEMA YENYE KUBEBA MSAMAHA WA YOTE MABAYA ALIYOKUWA AKIYAFANYA NYAKATI HIZI.

MANDIKO YAMESIMAMA KATIKA KILA KITU KINACHO FANYIKA KWA BINAADAMU HAPA DUNIANI.

MANDIKO NI NGUVU NA KINGA YA KILA BAYA KWA BINAADAMU.

INGAWA BINAADAMU WANAPITA KATIKA MAPITO TOFAUTI KWA SABABU YA KITU KINACHOITWA MAISHA.

KUMBUKA MAISHA NI SIRI YA BINAADAMU WA SASA KATIKA DUNIA HII

LAZIMA UPITIE PITO FULANI LINALOLETA  FURAHA AU UZUNI PIA LINAPELEKEA MAFUNDISHO KWA WENGINE.

NDIO MAANA YA MAISHA NI SAFARI YENYE VITUO TOFAUTI KILA SIKU YA MAISHA YAKO.

ITAENDELEA
UMEONAA
KENNEDY KIMARO

KWELI KABISA MAISHA NI SAFARI YENYE VITUO VINGI TOFAUTI.

KITU KIMOJA CHENYE KUSHANGAZA NI MTAZAMO WA NAFSI YA KILA BINAADAMU HAPA DUNIANI.

FANYA MAZURI KWA ASILIMIA MIA MOJA  LAKINI BADO NI TATIZO

INABIDI TUKAE KIMYA NA MUNGU WETU KWANI MAISHA NI SAFARI.

KILA KITU KINA CHANZO NA SABABU YA MAPITO AU MAJARIBU YA MATENDO YETU KILA SIKU.

CHA KUPENDEZA NI LAZIMA UWE NA MOYO WA KIKUBALI MATOKEO AU KUKUBALI MSAMAHA WA UPANDE MMOJA.

LAZIMA UJIKUBALI NA UWAKUBALI WALE WANAOISI IMEWAGUSA KWA UPANDE MMOJA.

Kama andiko hili

Mimi nilipanda, Apolo akatia maji. Bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.

TUNAJIFUNZA NINI NA SOMO APO JUU

0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu