Tuesday, December 13, 2016

MAISHA YA LEO NA KESHO KWA KIJANA WA LEO

UKINIONA NATABASAMU KWA MBALI HUKU  NACHEKA CHINI CHINI

NAJUA UTANIULIZA KWANINI NINAFANYA HIVYO

JIBU LAKE NAKUMBUKA MSEMO WA ZAMANI ULIKUWA UNASEMA HIVI

KUWA MWANANGU UYAONE YA DUNIA

NAJUA BADO UNAJIULIZA KWA NINI NAYASEMA HAYO.

BASI TWENDE NA MIMI UTAJUA KWA NINI NILISEMA "KUWA MWANANGU UYAONE DUNIA"

DUNIA YENYEWE IPO SAFARINI AMBAYO ISIYO NA MWISHO ILA KILA KIUMBE KINA MWISHO

KAWAIDA DUNIA INALIZUNGUKA JUA PIA INAJIZUNGUSHA YENYEWE KATIKA MUHIMILI WAKE.

CHA AJABU NJIA UNAYOPITIA DUNIA TOFAUTI KILA WAKATI KWA MAHESABU YA MUUMBA MWENYEWE

TENA AMEVIPANGA VITU VINAVYO FANANA NA DUNIA KATIKA ANGA ZA JUU NA PIA VINALIZUNGUKA JUA KWA MAHESABU YA AJABU NA TECHNOLOJIA ISIYO NA MFANO WAKE

HAPO NDIO UNAPATA KITU KINACHOITWA MAISHA YANAYOPATIKANA KWA KILA KIUMBE KILICHO NDANI YA DUNIA HII TUNAYOISHI SASA

KATIKA MAISHA UTAPATA KITU KINACHOITWA LEO NA KESHO UKIFANYA MAHESABU UTAPATA LEO NA KESHO

JIBU LAKE MAISHA YALIPO ANZA TANGU  UKIWA TUMBONI KWA MAMA YAKO MPAKA KUZALIWA KWAKO HAPA DUNIANI NA MAISHA YA YA LEO

AU WEWE UNASEMA JUU YA LEO NA KESHO.

HEBU TWENDE NA MIMI ILI TUJUE  MTAZAMO WA MAWAZO YANGU YAMESIMAMA WAPI KWENYE HIYO LEO NA KESHO.

NAREJEA KUSEMA YOTE NI YANGU NI SIO KWA MTU MWINGINE KWANI YEYE ANAO MTAZAMO WAKE.

TUANZE NA LEO

TAZAMA LEO KAMA KIJANA ALIYEKUWA NA KUTIMIZA MIAKA 18 ITAKAYOKUPA NGUVU YA KUFANYA MAMBO YAKO KAMA YEYE KIJANA WA LEO

TAZAMA PALE MZAZI ANAPOKUWA NA WASIWASI WA MATENDO UNAYOTENDA KILA SIKU AMBAYO KWA MTAZAMO WANGU NDIYO NYAKATI ZA LEO KWA KIJANA

EBU TAZAMA VINGAPI UNAVIFANYA KWA HESHIMA ZA PANDE ZOTE KATIKA FAMILIA YAKO.

KUMBUKA WEWE BADO UPO CHINI YA WAZAZI KWA UPANDE MMOJA NA UPANDE MWINGINE UNAWAZA KUJENGA MWELEKEO WAKO KAMA KIJANA LEO

SASA KAZI INAKUJA PALE WAZAZI WAKO ALIPOKUWA UNAISHI NA WAZAZI WAKO WALIKUPA MAFUNDISHO YA IMANI NA KIDUNIA ILI KUISHI KATIKA DUNIA YENYE TABIA TOFAUTI

TENA WATU WANAKUANGALIA UWEZO WAKO WA IMANI NA ELIMU YA KIDUNIA UMESIMAMA UPANDE GANI.

MARA NYINGI MISINGI HIYO MIWILI NDIO ITAKUPA MWELEKEO WAKO KATIKA NYAKATI ZA LEO.

Tutaendelea
KENNEDY KIMARO

MSINGI WA KWANZA NI IMANI

IMANI NI MSINGI AMBAO UNAKUFANYA KUWA NA MATENDO YANAYOLETA TABIA NJEMA ILIYO NA UPENDO WA KWELI KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU.

IMANI INAKUFANYA UWE NA UTIIFU KWA MUNGU WAKO.

MUHIMU KWA KIJANA WA LEO NI KUJENGE UHUSIONO BORA KATI YA FAMILIA TOFAUTI.

NENO FAMILIA SIO UDUGU WA UZAO WAKO BALI MKUSANYIKO WA WATU MNAOISHI KWA IMANI KUPITIA MUNGU BABA ILI KUJENGA UPENDO WA KWELI

KIJANA SHUPAVU WA JINSIA YOYOTE LAZIMA USIMAME IMARA KATIKA IMANI NA UPANGAJI WA MAMBO YAKO UNAYOYAFANYA KILA SIKU.

KUMBUKA KIJANA  MWENYE KUTENDA MATENDO YENYE TABIA NJEMA NA MWENENDO WA HESHIMA  KWA KUMPENDA MUNGU NA JAMII ILIYOMZUNGUKA.

YEYE NDIYE KIONGOZI BORA KATIKA JAMII.

TABIA YA KIJANA SIO NYUMBANI TU UNAPOKUWA MASOMONI KAMA MWANAFUNZI NDIPO UNAJIFUNZA MAMBO MENGI YENYE TABIA ZA WATU TOFAUTI UWAPO SHULE AU CHUO.

KWANINI CHUO NA SHULENI

KWA SABABU SEHEMU AMBAYO HUYU KIJANA WA LEO KAMA MWANAFUNZI UWA ANAJIFUNZA TABIA ZILIZO NZURI AU ZENYE MAADILI YASIO FAA KWA JAMII KUTOKANA NA KUWEPO KWA VIJANA TOFAUTI TOKA MAKAZI TOFAUTI.

MARA NYINGI SHULENI AU CHUO UWA PANA CHANGAMOTO KWA KIJANA KUWA NA MSIMAMO WENYE MANUFAA ILI BAADAE ASIMAME YEYE MWENYEWE

WAKATI MWINGINE VIJANA WANAJIKITA KATIKA MATENDO MABAYA  KAMA
UTUMIAAJI WA MADAWA YA KULEVYA NA MAMBO YASIYO KUBALIWA NA JAMII KWA UJUMLA.

SHULE NYINGI UWA ZINAWAJENGA VIJANA KATIKA MISINGI YA KUSIMAMA WAO WENYEWE ILI WAWEZE KUJITEGEMEA KUTOKANA NA MASOMO WANAYOWAFUNDISHA.

VIJANA LEO WANA CHEPUKA KATIKA MASOMO YA AINA TOFAUTI ILI BAADAYE WAWE WATU MUHIMU KATIKA JAMII KAMA

WAANDISI AU WANASAYANSI AU MADAKTARI AU WAHASIBU NA VIONGOZI KATIKA SEKTA TOFAUTI ZA JAMII.

Itaendelea
Kennedy Kimaro

0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu