Thursday, December 15, 2016

MAISHA YA LEO NA KESHO KWA KIJANA SEHEMU YA PILI

MSINGI WA KWANZA NI IMANI

IMANI NI MSINGI AMBAO UNAKUFANYA KUWA NA MATENDO YANAYOLETA TABIA NJEMA ILIYO NA UPENDO WA KWELI KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU.

IMANI INAKUFANYA UWE NA UTIIFU KWA MUNGU WAKO.

MUHIMU KWA KIJANA WA LEO NI KUJENGE UHUSIONO BORA KATI YA FAMILIA TOFAUTI.

NENO FAMILIA SIO UDUGU WA UZAO WAKO BALI MKUSANYIKO WA WATU MNAOISHI KWA IMANI KUPITIA MUNGU BABA ILI KUJENGA UPENDO WA KWELI

KIJANA SHUPAVU WA JINSIA YOYOTE LAZIMA USIMAME IMARA KATIKA IMANI NA UPANGAJI WA MAMBO YAKO UNAYOYAFANYA KILA SIKU.

KUMBUKA KIJANA  MWENYE KUTENDA MATENDO YENYE TABIA NJEMA NA MWENENDO WA HESHIMA  KWA KUMPENDA MUNGU NA JAMII ILIYOMZUNGUKA.

YEYE NDIYE KIONGOZI BORA KATIKA JAMII.

TABIA YA KIJANA SIO NYUMBANI TU UNAPOKUWA MASOMONI KAMA MWANAFUNZI NDIPO UNAJIFUNZA MAMBO MENGI YENYE TABIA ZA WATU TOFAUTI UWAPO SHULE AU CHUO.

KWANINI CHUO NA SHULENI

KWA SABABU SEHEMU AMBAYO HUYU KIJANA WA LEO KAMA MWANAFUNZI UWA ANAJIFUNZA TABIA ZILIZO NZURI AU ZENYE MAADILI YASIO FAA KWA JAMII KUTOKANA NA KUWEPO KWA VIJANA TOFAUTI TOKA MAKAZI TOFAUTI.

MARA NYINGI SHULENI AU CHUO UWA PANA CHANGAMOTO KWA KIJANA KUWA NA MSIMAMO WENYE MANUFAA ILI BAADAE ASIMAME YEYE MWENYEWE

WAKATI MWINGINE VIJANA WANAJIKITA KATIKA MATENDO MABAYA  KAMA
UTUMIAAJI WA MADAWA YA KULEVYA NA MAMBO YASIYO KUBALIWA NA JAMII KWA UJUMLA.

SHULE NYINGI UWA ZINAWAJENGA VIJANA KATIKA MISINGI YA KUSIMAMA WAO WENYEWE ILI WAWEZE KUJITEGEMEA KUTOKANA NA MASOMO WANAYOWAFUNDISHA.

VIJANA LEO WANA CHEPUKA KATIKA MASOMO YA AINA TOFAUTI ILI BAADAYE WAWE WATU MUHIMU KATIKA JAMII KAMA

WAANDISI AU WANASAYANSI AU MADAKTARI AU WAHASIBU NA VIONGOZI KATIKA SEKTA TOFAUTI ZA JAMII.

Itaendelea
Kennedy Kimaro

KIJANA WA LEO BAADA YA KUMALIZA CHUO AU SHULE.

HAPA NDIPO MAJARIBU YA MAISHA NA KITENDAWILI CHA MAISHA KINAPONZIA

MARA NYINGI MTAZAMO WA MAISHA INATEGEMEA UNATOKEA FAMILIA GANI 

KAMA UNATOKA FAMILIA YENYE UWEZO KIDOGO NI NAFUU KATIKA KUINGIA MAISHA YA KIJANA WA LEO

KAMA UNATOKA KATIKA FAMILIA MASIKINI  HAPO CHANGAMOTO ZA KUANZA MAISHA NI NGUMU 

NYAKATI NYINGINE HUYU KIJANA WA LEO ANACHOKA NA KUJIKITA KATIKA MIENENDO MIBAYA YENYE KUTISHA KWA KIJANA WA LEO.

KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA ZINAONESHA VIJANA WENGI HAWANA KAZI 

HEBU TUANGALIE KATIKA GOOGLE SEARCH TUONE WANASEMAJE SUALA LA AJIRA KWA VIJANA WA AFRIKA.

"Ukosefu wa ajira ni tatizo la ujumla katika Afrika, kinachotakiwa ni lazima kuwe ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kulishughulikia. ... Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika Afrika kusini mwa Sahara, vijana wenye ukosefu wa ajira wanafikia karibu asilimia12 kutokana na takwimu za .Apr 1, 2016

NAFIKIRI UMEFUNGUA MAWAZO KIDOGO KUJUA KIJANA WA LEO ANAVYO ELEKEA KUWA NA MAJUKUMU MAGUMU 

AJIRA INAVYO KUWA TATA KATIKA AFRIKA KWA UJUMLA KWA KIJANA WA LEO.

Itaendelea

KENNEDY KIMARO

16-12-2016

AJIRA INAPOKUWA NGUMU KWA KIJANA WA LEO

KWANZA KIJANA MWENYE MISINGI BORA YA IMANI UWA HAKATI TAMAA KATIKA MIANGAIKO YAKE YA KUTAFUTA KAZI

HICHO KINAKUWA KIPINDI CHA MAPITO KWA KIJANA WA LEO.

MARA NYINGI HUYIU KIJANA WA LEO UWA ANAPATA MAJARIBU MENGI.

WAKATI WA KUTAFUTA KAZI UTAPITA KILA KONA YA MJI NA UTASOMA HABARI ZA KUTATAFUTA NAFASI ZA KAZI KWA NGUVU ZAKO ILI MAISHA YAENDELEE.

WAKATI WA MIANGAIKO NA BAADA YA KUFANYA INTERVIEW MAENEO TAFAUTI BILA KUCHOKA.

KILA UENDAKO KWENYE INTERVIEW UTAKUTANA NA SWALI MOJA LENYE KUMCHOSHA MAWAZO KIJANA WA LEO.

SWALI LENYE NI HILI

Je unao uzoefu wa miaka mingapi kazini. 

Wakati huyu kijana wa leo, ndio katoka chuo au shule miezi kazaa iliyopita.

JIBU TOKA KWA KIJANA WA LEO NI HILI HAPA CHINI.

Nilipokuwa chuo nilikuwa nikifanya mazoezi ya kikazi sehemu inayoendana na masomo yangu.

Uzoefu wangu ni elimu yangu na nilichokisema hapo mwanzo. 

WAKATI KIJANA WA LEO ANAPOKUWA AKISUBIRI MAJIBU YA MAJARIBIO YA KAZI 

NDIPO WANAPOJITOKEZA WATU WA KATI AU VIJANA WA MJINI NA KUSEMA WANAWEZA KUMSAIDIA KUPATA AJIRA.

HUYI KIJANA WA MJINI NI MTU WA AINA GANI. 

NI MTU WA KATI KAZI YAKE NI KUPATA FEDHA BILA KUWAJIBIKA AU UTAPELI KWA JINA LA MJINI.

HAPA KIJANA ANAKUWA NJIA PANDA 

INAYOWEZA KUMTAMANISHA KUWA KIJANA WA MJINI 

AU KUVUTA SUBIRA ILI APATE AJIRA ILI MAISHA YAENDELEE KWA AMANI YENYE UPENDO WA KWELI.

MARA NYINGINE UWEZO WAKE WA ELIMU NI CHACHU TOKA KWA VIJANA WA MJINI WA KUTAKA KUMTUMIA KAMA MTU WA KATI KWA KAZI NYINGINENE ZENYE KUITAJI MSOMI.

IMANI NDIYO MSINGI WA KUTOJIINGIZA KATIKA KAZI ZISIZO FAIDA NA DHAMANA KWA JAMII.

Itaendelea 

Kennedy KimaroZ 

18/December/2016


KIJANA ANAYETOKA FAMILIA YENYE UWEZO YUPO KAZINI ILI MAISHA YAENDELEE.

MARA NYINGI VIJANA TOKA FAMILIA ZENYE UWEZO WANAYO BAHATI YA KUPATA AJIRA MAPEMA KUTOKANA NA UWEZO WA ELIMU ZAO TENA WANAPATA AJIRA KATIKA MAKAMPUNI BINAFSI AU IDARA ZENYE KUESHIMIKA KATIKA JAMII KUTOKANA NA NGUVU YA FAMILIA ZAO.

HUYU KIJANA ANAPOANZA KAZI ANAFANYA KAZI KWA BIDII NA UWEZO WAKE WOTE KATIKA KIPINDI CHA UANGALIZI ANAKUWA MWAMINIFU NA KUKIZI MATAKWA YANAYO SABABISHA KUPEWA AJIRA YA KUDUMU.

LAKINI KUTOKANA NA IMANI DUNI NA USHAWISHI WA KIDUNIA KIJANA MWENYE FIKRA YA  KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA ANABADILIKA KUWA NA SURA YA RUSHWA NA UFISADI.

KIJANA TOKA FAMILIA YENYE UWEZO ANAPOKUWA MZOEFU KAZINI KWA KUJUA NJIA ZA MKATO MARA NYINGI MSHAHARA WAKE SIO BAJETI YAKE YA MATUMIZI BALI PESA ANAYOIPATA KWA RUSHWA PEMBENI NDIO MSHAHARA WAKE WA MATUMIZI.

HUYU KIJANA WA LEO MWENYE MWELEKEO WA TAMAA YA UTAJIRI WA KIFEDHA NA KUWEKEZA MITAJI MIKUBWA KAMA WANAVYOMILIKI FAMILIA YAKE KIJANA ANAKUWA NJIA PANDA AMBAYO.

INASABABISHA NYAKATI NYINGINE KUJIKITA KATIKA MAMBO TOFAUTI YANAYOMSHAWISHI KUFANYA VITU KINYUME NA UTARATIBU WA SHERIA ANAFANYA VITU VINAVYO PIGWA VITA KATIKA JAMII KAMA.

RUSHWA UPENDELEO KWA WATU WASIOSTAILI NA KUWANYIMA HAKI WANAOSTAILI ILI KUMPATIA NGUVU YA KUPATA PESA KWA NJIA ZISIZO SAHIHI.

KUJIINGIZA KATIKA MAISHA YENYE UHUSIANO WA RUSHWA NA UNYANYASAJI KWA WENGINE  KUPITIA MADARAKA YAKE ALIYOPEWA KUSAIDIA JAMII NA TAIFA LAKE.

VIJANA WENGI WA JAMII HII UFUKUZWA AU KUSIMAMISHWA KAZI KUTOKANA NA FIKRA ZAO ZA UTAJIRI WA HARAKA KATIKA MAWAZO YAO.

LAKINI KWA UPANDE MWINGINE VIJANA WENGINE TOKA FAMILIA ZENYE UWEZO WANAKUWA NA UWEZO MKUBWA KATIKA UTENDAJI NA KUTOA MSAADA KWA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA.

MARA NYINGI UNAKUTA VIJANA WANAOTOKEA KATIKA FAMILIA ZENYE UWEZO HAWANA TAMAA NDOGO NDOGO KATIKA KUPOKEA RUSHWA YA FEDHA AU UNYANYASAJI NA UBINAFSI KATIKA KAZI ZA JAMII 

UTAKUTA VIJANA HAWA WAMEBOBEA KATIKA MSINGI WA IMANI UNAWOWAJENGA KUWA NGUVU NA UWEZO WA KUFANYA KAZI KATIKA JAMII NA TAIFA LAKE.

FAMILIA ZENYE UWEZO ZINAPENDA KUWEKEZA KATIKA IMANI ILI FAMILIA IWE NA MSINGI WENYE KUESHIMIKA KATIKA JAMII NA TAIFA.

HAPO KIJANA WA LEO ANAPOKUWA NA MWELEKEO WA WAZAZI KATIKA IMANI BASI YEYE UWA NA NGUVU ULIYO MSAADA WA MWENYEZI MUNGU KATIKA KUSIMAMA KWENYE IMANI YA KWELI ILI KUIJENGA JAMII ILIYO BORA.

NDIO MAANA VIJANA WOTE WALIO. KATIKA MSIMAMO WA KIMUNGU BASI IMANI YAO INAWAPA NGUVU YA KUFANYA YALIYO MEMA NA YANAYOKUBALIKA KATIKA KIJAMII NA TAIFA KWA UJUMLA.

Itaendelea 

Kennedy Kimaro 

26/December/2016

Wewe kama kajana wa leo simama na imani uliyopo sasa, au badilika na ufuate kile nafsi yako inavyokutuma kwa wakati uliopo sasa.

Kumbuka nafsi yako ni lazima ijengwe katika imani inayomwamini muumba wa mbingu na vitu vinavyoonekana na visivyoonekana.

Kataa kabisa na kamwe usifanye nafsi yako iwe nafsi ya mwenzako, kamwe kataa nguvu za kishetani kukuongoza katika imani potofu.

Kumbuka kila ufanyacho wewe, kitabaki kuwa chako na kitakupa sifa ya matendo yako wewe binafsi. 

Yawe mabaya au mazuri ni yako wewe binafsi daima milele.

Na hakuna atayepunguza au kuongeza lolote kwako, kwani wewe umepewa roho yenye kuwakilisha uhai wako hapa duniani.

Mwache yeye ajenge matendo yake kama yeye binafsi.

Kwani na yeye anapaswa kukuachia wewe ujenge yako yaliyo mema kwa ramani ya maisha yako kwa kutumia viongozi wateule wa Mungu.

KIJANA WA LEO TAZAMA MBELE KWA NGUVU YA IMANI ILI IKUSAIDIE KUSIMAMA IMARA MUDA WOTE.

NARUDIA TENA KUSEMA HILI 

HAPO ULIPO SASA NDIPO ULIPO WEWE MWENYEWE KAMA NAFSI YAKO INAVYOKUTUMA KUFANYA KITU CHOCHOTE. 

BASI IPE NAFSI YAKO NGUVU YA MUNGU IKUTUME KAMA WEWE NA IMANI YAKO MWENYEWE.

KILA KITU UNACHOAMUA BASI KIWE CHA IMANI AMANI NA UPENDO WA KWELI NDANI YAKE.

NARUDIA TENA SIKU ZOTE CHELEWA KUAMUA KITU CHENYE UTATA KWA KUNYAMAZA KIMYA 

PILI SIKILIZA WENGINE WANASEMAJE 

TATU CHANGANYA NA YAKO ILI UPATE LILILO JEMA NA LENYE UPENDO WA IMANI NA AMANI NDANI YAKE. 

TAMBUA SIFA YA IMANI YAKO IPO KWAKO NA KWA MUNGU NDIO MAANA WEWE UNAJUA YAKO YALIO KATIKA MAWAZO YAKO

LAKINI MUNGU TAYARI ANAJUA KILA LILILO KATIKA MAWAZO YAKO KABLA WEWE UJAWAZA 

INAMAANA MUNGU ANAJUA KILA KITU JUU YAKO.

UJACHELEWA KIJANA WA LEO TAZAMA MBELE MAISHA YA KWA IMANI MOJA TU NAYO NI MUNGU AMBAYE YUPO LEO NA MILELE DAIMA.

Itaendelea 

Kennedy Kimaro 

28/12/2016
0 Maoni yako/Post comments here:

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu