Tuesday, August 14, 2007

NAOMBENI KURA ZENU-A.Y

click kwenye picha kupata picha kubwa

http://www.ay.co.tz/index.php
Tukirejea katika habari zitolewazo na mtandao huu,habari ya tarehe 13 Julai 2007 yenye kichwa cha habari “USIJARIBU YA A.Y KUWANIA TUZO ZA KISIMA” sasa muda wa kupiga kura umewadia.Kwa mujibu wa maelezo ya A.Y ni kuwa kwa kipindi hiki amepewa maelekezo ya jinsi ya kupiga kura ukiwa nchini Kenya.Na kwa wale ambao wako nje ya nchi ya Kenya watapewa maelezo mapema iwezekanavyo.
“Mwimbo wangu wa USIJARIBU umechaguliwa kushindaniwa katika categories mbili…BEST SONG TANZANIA na BEST VIDEO TANZANIA katika KISIMA MUSIC AWARDS ya nchini KENYA,Kwa mashabiki wangu wote walio ndani ya Kenya nawaomba wajitokeze kwa wingi kwa kunipigia kura tuweze kuchukua tuzo hizo.
Ukitaka kunipigia kura kwa njia ya simu ya mkononi andika kwenye sms KISIMA 16a kisha tuma katika namba 8001 hapo utakuwa umeichagua USIJARIBU kuwa the best song toka Tanzania. Pia andika KISIMA 17b kisha tuma katika namba 8001 hapo utakuwa umeichagua USIJARIBU kuwa the best video kutoka TANZANIA.Najua siku zote hamniangushi katika kila jambo tunalolifanya kwa ushirikiano.
Na kwa wale washabiki wangu wa nchi yangu TANZANIA na majirani zetu UGANDA,BURUNDI na RWANDA na wengine ambao mpo popote duniani pia nitawapa maelekezo ya jinsi ya kupiga kura kwa kutumia website.Nasubiri maelekezo ya waandaaji wa Tuzo hizo,ASANTENI SANA NA NAUHESHIMU SANA NA KUUTHAMINI SANA MCHANGO WENU. Alimalizia A.Y katika maelezo yake kwa washabiki wake kupitia vyombo vya habari.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu