Wednesday, November 14, 2007

Kikwete amteua Zitto kwenye kamati ya mikataba ya madini


Richard ndani ya sky news













*Itaongozwa na Jaji Mark Bomani,


* Pia wamo Cheyo, Mwakyembe


* Yapewa miezi mitatu kumaliza kazi


* Zitto asema atafanya kazi kwa maslahi nchi



Na Tausi Mbowe



RAIS Jakaya Kikwete amemteua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya uangaliaji upya mikataba ya uchimbaji wa madini nchini.
Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe kumi na mmoja itakuwa chini ya uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani.
Wengine katika Kamati hiyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.
Wajumbe wengine ni Mbunge wa Msalala (CCM),Ezekiel Maige, Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ilisema kuwa pamoja na mambo mengine, kamati hiyo pia itakuwa na kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.
Kamati hiyo iliyopewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi yake pia inajukumu la kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo.
Pia Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini.
Kuundwa kwa Kamati hiyo kunafuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule yakuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi huko Uingereza na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi Februari mwaka huu.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Kabwe alifungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi hapo Januari mwakani. Hatua hiyo ya Bunge iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa makundi mbalimbali wakihoji sababu za kumfungia mbunge huyo kijana.
Hivi karibuni wakati Rais Kikwete akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika Ukumbi wa Kizota , mjini Dodoma aliahidi kuunda kamati hiyo itakayojumuisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kuangalia mikataba mipya ya madini.
Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na uteuzi huo, Zitto Kabwe alisema kwamba amepokea uteuzi huo wa Rais Kikwete na atafanya kazi kwa maslahi ya Watanzania.
"Nimepokea kwa mikono miwili uteuzi, naahidi kufanya kwa umakini wa hali ya juu," alisema alisema Zitto na kuongeza kwamba uamuzi wa Rais unaonyesha jinsi alivyokomaa kidemokrasia tofauti na wabunge 274 wa Chama cha painduzi (CCM )walioko bungeni.
Tuma maoni kwa Mhariri


Misemo na nahau

"Bahati ni upepo sasa upo kwangu"

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu