Sunday, November 11, 2007

Rukwa kupatiwa umeme toka Zambia karibuni












2007-11-11 10:04:19 Na Juddy Ngonyani, Sumbawanga

Si muda mrefu kuanzia sasa wakazi wa mkoa Rukwa wataacha kutumia vibatari kufuatia tangazo la TANESCO kwamba inafanya jitihada za kuwapatia umeme kutoka Zambia. Wengi wa wananchi hao wataanza kufurahia televisheni na kutizama video, wataachana pia na kutumia pasi za mkaa na redio za betri, baada ya TANESCO kufanya mazungumzo na mamlaka za Shirika la Umeme Zambia (ZESCO) juu ya uwezekano wa kuwapatia umeme huo.� Ahadi hiyo ya matumaini ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Meneja wa TANESCO mkoani Rukwa, Bw. Mahende Mugaya. Alisema hatua hiyo inatokana na gharama za kuunganisha umeme kutoka gridi ya taifa mkoani Mbeya hadi Sumbawanga kuwa kubwa kuliko ile ya kuutoa Zambia hadi Sumbawanga.� Bw. Mugaya alisema gharama ya kuunganisha umeme kutoka Mbeya hadi Rukwa ambao ni umbali wa kilomita zaidi ya 300 ni Sh. bilioni 48, lakini hakutaja za Zambia.� Na kwamba bilioni 48 hazihusishiupembuzi yakinifu, ujenzi wa kituo kikuu cha umeme na fidia kwa wananchi. Kaimu Meneja alisema katika kukabiliana na tatizo hili shirika lina mpango wa kukifufua na kukiimarisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta kilichopo Majengo mjini ili kiwe kituo cha dharura endapo kuna matatizo kwenye njia kuu ya umeme kutoka Zambia. Mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mwakani na kukamilika mwaka 2009. Kukamilika kwa mradi huo kutakuwa ni ufumbuzi wa tatizo sugu la kukatika kwa umeme kwa wateja wa Rukwa ambao hawana uhakika wa nishati hiyo kwa muda mrefu.
SOURCE: Nipashe

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu