Thursday, December 20, 2007

ni mwaka mmoja wa HabariLeo


::Maskani>habari
Habari za KitaifaHabari nyingine zaidi!
Ni mwaka mmoja wa HabariLeo
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Thursday,December 20, 2007 @00:03
GAZETI pekee la serikali la Kiswahili la HabariLeo linalochapishwa na Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), kesho linatimiza mwaka mmoja tangu lilipoanzishwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Meneja Masoko wa TSN, Christina Geleja, kwa niaba ya Mhariri Mtendaji, sherehe hizo zitafanyika katika jengo la TSN Mtaa wa Samora, Dar es Salaam, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Alisema sherehe hizo zitaambatana na maelezo kuhusu maendeleo ya Kampuni na mafanikio ya gazeti hilo, kuzindua shindano la wasomaji wa HabariLeo, utoaji wa zawadi kwa wauzaji bora wa HabariLeo, hotuba ya mgeni rasmi na burudani maalumu.

Gazeti la HabariLeo lilianzishwa Desemba 21, 2006, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2005 hadi 2010, ambayo katika eneo la vyombo vya habari, pamoja na mambo mengine, iliahidi kuanzisha gazeti la Kiswahili la Serikali.

Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyezindua gazeti hilo kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma, asubuhi ya Desemba 21, 2006, ikiwa ni mwaka mmoja tangu atawazwe kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Tanzania.

Mbali ya kumiliki gazeti hilo, TSN pia inamiliki magazeti ya Kiingereza ya Daily News na Sunday News, ambayo ni magazeti yanayoaminika nchini katika lugha ya Kiingereza. Pia ndiyo magazeti kongwe nchini.

Kutokana na shughuli hiyo, Mtaa wa Samora kuanzia makutano ya Mtaa wa Mkwepu na hadi makutano ya Barabara ya Azikiwe, utafungwa kwa muda kupisha shughuli hiyo.
Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
Posted by Picasa

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu