Wednesday, November 21, 2007

Zitto Kabwe adai wanaopinga uteuzi wake wanatumiwa












Zitto Kabwe adai wanaopinga uteuzi wake wanatumiwa Zitto Kabwe adai wanaopinga uteuzi wake wanatumiwa
Wakati mgogoro kuhusu uteuzi wa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe katika kamati ya madini ukiendelea kufukuta ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mbunge huyo amesema baadhi ya watu wanaotoa kauli ya kupinga kuwako katika kamati ya kupitia upya mikataba ya madini wanatumiwa na makampuni ya madini bila kujua.
Akizungumza katika kipindi cha jana asubuhi cha Jambo Afrika kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TVT), Zitto alisema kuna baadhi ya watu wanatumiwa na makampuni ya uchimbaji madini bila kujua, kwani makampuni hayo hayataki kuchambuliwa kwa mikataba yao kwa sababu inawanufaisha wao zaidi kuliko Watanzania.
Nadhani baadhi yetu tunatumiwa na maadui zetu bila kujua, tunatumiwa na makampuni ya uchimbaji madini bila kujua, wao hawataki mikataba yao ichambuliwe kwani inawanufaisha wao zaidi kuliko sisi, alisema Zitto.
Alisema hoja ya kupitia upya mikataba ya madini ni Ilani ya Chadema na yeye ndiye aliwasilisha bungeni sasa ikiwa Rais kaamua kuunda kamati katumia ilani ya chama chao kuna kosa gani yeye kuwemo.
Zitto pia aliwapinga wanaosema hamati hiyo haina nguvu kisheria kwa kuwa haikuteuliwa na Bunge, kwa maelezo kwamba hoja zao hazina nguvu.
Alisema kimsingi, Rais ni mkuu wa nchi hivyo ana uwezo kumwita mtu yeyote na hata kamati aliyounda ina mamlaka hayo.
Hoja kwamba kamati iliyoundwa na rais kupitia mikataba ya madini haina nguvu kisheria haina nguvu, kwani yeye ndie Amiri Jeshi Mkuu na kamati hiyo ina uwezo na uhuru wa kumuita yoyote na kumhoji ili kupata ushahidi, alisema Zitto.
Alisema sio mara ya kwanza kuteuliwa katika kamati ya rais na sasa anashangaa ni kwanini uteuzi wa hivi karibuni umezua mjadala mkubwa. Zitto amewahi kuteuliwa katika Kamati ya kukusanya maoni ya uundwaji Shirikisho la Afrika Mashariki.
Hata hivyo, alisema kuwa anasubiri Kamati Kuu ya chama chake ikae Jumaamosi ijayo na kutoa kauli ambayo ataiheshimu. Maamuzi ya Kamati Kuu ndio maamuzi yangu, ikisema nitoke nitatoka, alimalizia Zitto.
Awali katika majadikliano hayo Mbunge wa Tarime (Chadema) Chacha Wangwe ambaye amekuwa akipinga uteuzi wa Zitto alisema kamati hiyo haina nguvu kisheria kwani hoja ya kuundwa kwake ilitoka katika mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio bungeni kama wapinzania walivyokuwa wanataka.
Alisema Kamati haiwezi hata kutangaza matokeo yatakayopatikana bali itapeleka ripoti kwa rais.
Katika hatua nyingine, ratiba ya ziara ya kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji wa madini nchini katika nchi mbalimbali duniani, itatangazwa rasmi wiki ijayo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji Mark Bomani aliliambia Mwananchi jijini Dar es Salaam jana kuwa wanatarajia kutangaza ratiba hiyo Jumanne wiki ijayo, lakini hakuwa tayari kueleza nchi anayokwenda.
Wakati huo huo; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anawasili nchini leo kuongoza Kikao Cha Kamati Kuu ya chama hicho (CC) itakayojadili uteuzi wa Mbunge wake Zitto Kabwe katika Kamati ya Madini.
Pia Kamati ya Ufundi ya Muungano wa Vyama vya Upinzani imekutana kuzungumzia suala hilo.
Kamati hiyo ambayo iko chini ya mwenyekiti, Benedict Mutungilei wa TLP, imekutana na kujadili suala la mbunge huyo kuwapo katika Kamati hiyo na kutoa mapendekezo yake kwa wenyeviti wa vyama vilivyo katika muungano huo.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo iliyokutana juzi na jana ni Hussein Mmasi kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Sam Luhuza na Ndelakia Kessy wa NCCR-Mageuzi, Erasto Tumbo na John Mrema kutoka Chadema.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu