Saturday, November 24, 2007

Mwacheni Zitto Kabwe afanye kazi












Mwacheni Zitto Kabwe afanye kazi
Na Gladness Mboma


HII inashangaza pale ambapo baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) wanapompinga mwenzao, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete katika Kamati ya Taifa kuangalia mustakabali wa Taifa wa rasilimali ya madini. Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameunda Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini Nchini kwa kuwateua Mwenyekiti na wajumbe 11 watakaofanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu. Kamati hiyo inashirikisha wanasiasa kutoka chama tawala na wale wa upinzani wakiwemo wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali na wataalam kutoka sekta mbalimbali Moja ya mambo yaliyosababisha majadiliano na mabishano makali ndani ya CHADEMA ni uteuzi wa kamati au tume hiyo ya kutazamia upya mikataba ya madini iliyowekwa kati ya wawekezaji na Serikali iliyoteuliwa na Rais Kikwete. Rais Kikwete aliweka wazi suala la kuundwa tume hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliomalizika hivi karibuni mkoani Dodoma. Katika mkutano huo Rais Kiwete alitoa ahadi hiyo baada ya matukio mengi ya kukashifiana baina ya viongozi wa Serikali na baadhi ya vyama vya upinzania hasa ujulikanao kama Muungano wa Vyama vinne vya Upinzania. Malumbano hayo ya kukashifiana yalikuwa yamezidi katika upande wa vyama vya upinzania, yakidai kuwa Serikali ilikuwa haifaidiki na rasilimali yake. Kutokana na kuruhusu mikataba ya uchimbaji madini hapa nchini iliyowapendelea zaidi wawekezaji na Taifa kuambulia faida ndogo na kusababisha hasara. Kashfa hiyo ilipamba moto hasa baada ya watendaji wa Serikali kwa maana ya mawaziri na viongozi wengine wa ngazi za juu katika taasisi muhimu na nyeti kutajwa hadharani kuhusika na vitendo vya rushwa. Zaidi ya jambo lililofumua malumbano na kashfa hizi ni sakata la mikataba ya madini na hasa mkataba wa madini wa Buzwagi ambao Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi kudaiwa kuusaini akiwa nje ya nchi na kwamba haukuwa na maslahi kwa Serikali. Aliyeibua hoja hiyo hakuwa mwingine bali ni Bw. Kabwe ambaye aliyatoa wazi bungeni na kumletea matatizo yaliyosababishia kusimamishwa na kutojishughulisha na shughuli zozote za Bunge, adhabu ambayo kwa sasa imemalizika. Baada ya kusimamishwa kwa Bw. Kabwe, vyama hivyo vinne vya upinzani vilianza kuzunguka nchini kuelezea umma wananchi kuhusiana na mkataba huo, na kuelekeza shutuma mbalimbali serikalini. Ni kweli vyama hivyo viliweza kuwateka wananchi kutokana na jinsi walivyokuwa wakieleza na kutoa vielelezo mbalimbali vilivyosababisha baadhi ya wananchi kuamini, walichokuwa wakisema. Baada ya malumbano hayo ya muda mrefu Rais Kikwete bila hiana aliunda tume ambayo imewashirikisha pia viongozi wawili wa vyama vya upinzani. Tume hiyo ambayo ni watu makini iliwafurahisha Watanzania wengi na watu kufurahia uteuzi huo ambao ni wa kidhati uliofanywa na Rais wetu makini na kuzidi kumuongezea heshima. Kilichowafurahisha zaidi Watanzania ni pale Rais Kikwete alipoteua pia viongozi kutoka vyama vya upinzania na hasa ukizingatia kuwa wapinzani hao ni kati ya wasemaji wazuri katika vyama vyao. Lakini pamoja na uteuzi huo kinachoshangaza ni kwamba baadhi ya wapinzani hao hao waliotaka kuundwa kwa tume ya aina hiyo wanataka kukwepa majukumu yao kama Watanzania, sasa wanataka Bw. Kabwe ajitoe kwa maelezo kuwa akiingia katika kamati hiyo atazibwa mdomo. Bw. Kabwe ninayemfahamu mimi na anayefahamika kwa Watanzania wote kutokana na ukakamavu wake na mwenye uchungu na nchi yake kamwe hawezi kuzibwa mdomo kama wasemavyo baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kikiwemo chama chake. Malumbano hayo hayalengi kulinufaisha Taifa, bali ni kuleta mgawanyiko ndani ya Taifa. ============ Upinzani wa kisiasa unatakiwa kuimarisha demokrasia na kuchochea maendeleo katika nchi husika, iweje leo hii Rais anateua mmoja wapo katika kambi hiyo ili aweze kutoa mchango wake kwa manufaa ya Taifa anazuiwa? ============= Sasa vyama vya upinzani mnakoelekea ni kubaya inaelekea nchi hii amuitakii mema, ni kwa nini mnapingana na yale ambayo yamefanywa na Rais wetu kwa manufaa ya nchi? Je, Rais asingeteua tume hiyo mpaka sasa mngekuwa mmezusha jambo gani, tufike mahali sasa tusiwe vyama vya upinzani vya kuleta fujo, Watanzania hawafurahishwi na uamuzi mnaofanya. Inasikitisha kuona baadhi ya watu tunaowategemea kuwa wamekomaa kisiasa wanataka kurudisha nyuma maendeleo ya nchi na kuanzisha malumbano yasiyokuwa na faida kwa Watanzania. Nilitegemea baada ya Rais kumteua Bw. Kabwe mngemwombea ili aweze kuifanya kazi yake vema badala yake mnamkatisha tamaa kana kwamba alichofanya Rais Kikwete ni kunyume. Kinachotakiwa ni kuiachia tume hiyo ya watu makini kufanya kazi yake kwa umakini tupate kujua kilichotokea na aliyesababisha ni nani na si vinginevyo, kwani hatutafika popote tukiendekeza malumbano.


Uchunguzi dhidi ya mtoto wa Rais Karume wapelekwa serikalini

Na Tausi Ally
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imekamilisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Wakili wa Kujitegemea, Fatuma Karume na kupelekwa uongozi wa juu serikalini.
Fatuma ambaye ni mtoto wa Rais wa Zanzibar, Aman Karume anadaiwa kumtolea maneno makali Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Addy Lyamuya.
Akizungumza ofisini kwake jana, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi alisema tayari taarifa hizo zimetumwa uongozi wa juu wa serikali kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Hakimu Mwangesi alisema kuwa, baada ya uchunguzi kufanyika, imebainika kuwa wakili huyo alifanya fujo mahakamani.
� Kwa maoni yangu na maelezo ya mashahidi walioshuhudia tukio, wamebaini kuwa ni kweli Karume alifanya fujo mahakamani, � alisema Hakimu Mwangesi.
Hakimu Mwangesi, alisema Hakimu Lyamuya hakuweza kumchukulia hatua wakili huyo, kwa madai kuwa, alipigwa na butwaa kutokana na kutoamini wala kutegemea kama wakili huyo angemtolea maneno makali na ya vitisho.
Alisema taarifa kwamba Hakimu Adolf Mahay anahusika na tuhuma za rushwa kama inavyodaiwa na Karume ni za uongo na kwamba hajapokea maelekezo yoyote kutoka ngazi ya juu serikalini za kumsimamisha kazi hakimu huyo.
Naye Hakimu Mahay alipohojiwa kuhusiana na tuhuma hizo, alisema hawezi kuongea chochote kwa kuwa si mwanasiasa na kwamba angekuwa amehusika na rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wangemkamata na kumchukulia hatua za kisheria.
�Na hili la Kisutu kuwa inanuka rushwa ni maoni yao wenyewe walioandika, ninachojua mimi Kisutu ni nzuri na inapinga rushwa,� alidai Hakimu Mwangesi.
Kuhusu kesi hiyo kupangwa kwa hakimu mwingine, Mwangesi alisema hivi anatafuta ushauri kwa kuwa mtoto huyo wa Karume, alisema kuwa mahakimu wote wanakula rushwa.
Alisema pia anasubiri barua ya Karume endapo ataandika kuondoa kesi hiyo katika mahakama hiyo au la kwani Novemba 21, mwaka huu wakati amkipelekea malalamiko dhidi ya Hakimu Lyamuya, alimwambia kwamba ataiondoa.
Novemba 22, mwaka huu, Hakimu Lyamuya aliwasilisha malalamiko Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) dhidi ya wakili huyo wa kujitegemea akimlalamikia kwa kumfokea mahakamani na kumtolea lugha ya vitisho.
Taarifa za kupokewa kwa malalamiko hayo TLS zilithibitishwa na Rais wa Chama hicho, Joaquin ambaye alisiditiza chama kinajukumu la kumtetea au kumuadhibu mwanachama endapo atabainika kukiuka maadili ya taaluma hiyo.

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu